Hatimaye Masauni - UvCCM Ang'atuka

Tulipokwambieni mnatumiwa tu na manya'nganyi kwa faida ya matumbo yao mlituona maadui wa nchi na watafuta vyeo, haya sasa mmeona mlipofikishwa CCM si chama chenu vijana wa Zanzibar, hasa Unguja, ni chama cha manyan'ganyi na majizi yanayotumia vibaraka wao Zanzibar kuifisidi nchi, hamjachelewa rudini kundini tuendeleze mapambano.

warudi kundini wapi cuf?huko nako ndo kabisa hakuna demokrasia cuf is belong to one person seif sharif hamad ,wanaongozana kisultani kisultani
 
Suluhu ya haya matatizo ni kuweka mgombea binafsi. Kama mtu hakubaliani na mienendo ndani ya vyama vyote vya siasa, basi anaamua kutojiunga navyo na akiamua kugombea apewe haki yake ya kugombea.

Ukichunguza sana, kila chama kina matatizo yake, lakini vyama vingine migogoro na misuguano ndani ya chama imezidi kiasi kwamba inakuwa ni kero.
 
Nasubiri kusikia kile kitakachozungumzwa na Masauni mwenyewe pamoja na viongozi wa jumuiya na chama chake. Kwa sasa mengi tunayosoma na kusikia yanatoka katika pande hasimu za sakata hili.
 
Jamani tusipotoke kwenye jambo la msingi hapa..Suala la Masauni kuachia Ngazi ni Lazima..Kwanini alidanganya umri? Hivi watanzania tutaendelea kuvumilia haya madudu hadi lini? Kwanini tunaruhusu kupotoshwa na siasa? Tuachilie mbali suala la kuvuruga Umoja (Hatuna uhakika nalo) vipi suala la umri? Tunamtetea mtu mwongo? Mi nadhani ingekuwa busara kumhoji na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria Masauni..kama ni maandamano wangeandamana kukipinga chama kwa kuruhu madudu haya-kuruhusu Uongo...
 
Tulipokwambieni mnatumiwa tu na manya'nganyi kwa faida ya matumbo yao mlituona maadui wa nchi na watafuta vyeo, haya sasa mmeona mlipofikishwa CCM si chama chenu vijana wa Zanzibar, hasa Unguja, ni chama cha manyan'ganyi na majizi yanayotumia vibaraka wao Zanzibar kuifisidi nchi, hamjachelewa rudini kundini tuendeleze mapambano.

333
. Forgery is the making of a false document with intent to defraud

or to deceive.
337
. Any person who forges any document is guilty of an offence
which, unless otherwise stated, is a felony, and he is liable, unless owing to the
circumstances of the forgery or the nature of the thing forged some other punishment is

provided, to imprisonment for seven years.MASAUINI can now be charged with this offence .
 
Jamani tusipotoke kwenye jambo la msingi hapa..Suala la Masauni kuachia Ngazi ni Lazima..Kwanini alidanganya umri? Hivi watanzania tutaendelea kuvumilia haya madudu hadi lini? Kwanini tunaruhusu kupotoshwa na siasa? Tuachilie mbali suala la kuvuruga Umoja (Hatuna uhakika nalo) vipi suala la umri? Tunamtetea mtu mwongo? Mi nadhani ingekuwa busara kumhoji na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria Masauni..kama ni maandamano wangeandamana kukipinga chama kwa kuruhu madudu haya-kuruhusu Uongo...
Kwani hawa CCM wamejua leo kuwa Masuni amezidisha umri, CCM waache bra! bra! kama wako serious kiasi hicho kwa watu wanaotoa data za uongo ili wapate uongozi ndANI YA CHAMA, MBONA HAWAWASHUGHULIKII Wabunge walioforge vyeti vya elimu!?
 
Jamani tusipotoke kwenye jambo la msingi hapa..Suala la Masauni kuachia Ngazi ni Lazima..Kwanini alidanganya umri? Hivi watanzania tutaendelea kuvumilia haya madudu hadi lini? Kwanini tunaruhusu kupotoshwa na siasa? Tuachilie mbali suala la kuvuruga Umoja (Hatuna uhakika nalo) vipi suala la umri? Tunamtetea mtu mwongo? Mi nadhani ingekuwa busara kumhoji na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria Masauni..kama ni maandamano wangeandamana kukipinga chama kwa kuruhu madudu haya-kuruhusu Uongo...

Madudu mangapi ya ccm yametokea na wamenyamaza, watu wangapi wamedanganya umri na wamejua wamenyamaza, kuna sababu nyingine hilo la umri ni danganya toto tu, wameshidwa kufikisha mafisadi mahakamani wanaahangaika na vitu havina hata maslahi, akifikishwa mahakamani sisi wananchi wa kawaida tutafaidika nini?
 
SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Hamad Masauni Yussuf kuachia ngazi wadhifa huo, baadhi ya vijana wa jimbo la Kikwajuni warejesha kadi za CCM kutokana na kutoridhishwa na suala hilo.

So huu mkwara wa mwezi Aprili umegeuka kuwa kilio?

6.jpg


Sehemu ya msafara wa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Hamad Yussuf Masauni, ukipita kuelekea matawi ya umoja huo ya Kaskazini Unguja, alipokuwa katika ziara ya kutembelea mikoa mitatu ya Unguja ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa vijana wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2010.

4.jpg


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (VCCM) Taifa, Hamad Yussuf Masauni, akipandisha bendera katika tawi la vijana la kijiji cha Dole Mbuyuni katika Mkoa wa Mjini Magharibi alipokuwa katika ziara ya kutembelea mikoa mitatu ya Unguja ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa vijana wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2010, Aprili 2010.

5.jpg

7.jpg


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (VCCM) Taifa, Hamad Yussuf Masauni, akiwasili katika tawi la umoja lililopo kijiji cha Dole Mbuyuni katika Mkoa wa Mjini Magharibi alipokuwa katika ziara ya kutembelea mikoa mitatu ya Unguja ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa vijana wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2010. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo Zanzibar, Mohamed Hassan Moyo.

2.jpg


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (VCCM) Taifa, Hamad Yussuf Masauni, akiangalia viungo vinavyozalishwa na vijana wa umoja huo katika kijiji cha cha Dole Mbuyuni katika Mkoa wa Mjini Magharibi alipokuwa katika ziara ya kutembelea mikoa mitatu ya Unguja ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa vijana wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2010, juzi (Aprili 2010)

1.jpg


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (VCCM) Taifa, Hamad Yussuf Masauni, akisakata ngoma ya asili ya Kibati, wakati alipotembelea kijiji cha Dole Mbuyuni katika Mkoa wa Mjini Magharibi alipokuwa katika ziara ya kutembelea mikoa mitatu ya Unguja ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa vijana wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu 2010.
 
Unapotokea mgongano wa viongozi kwenye vyama vya upinzani watawala watasema ati ni "vyama vya upinzani haviishi migogoro"; na inapotokea uchaguzi wa vijana kwenye chama cha upinzani ukawa na matatizo basi wanasema "chama kinawaonea au vigogo wa chama wanaonea watu wengine". Tatizo ni kuwa:

Inapokuja CCM viongozi wakigongana hadi kuitana kwa majina tunaambiwa ni demokrasia; viongozi wakitumuana kwa shutma mbalimbali wanasema "ni nidhamu ya chama".

Je yawezekana kuwa kweli katika shamba hili wanyama wote wana haki isipokuwa wengine wana haki zaidi? Yawezekana vipimo vinavyotumika kupimia upinzani vinapogeuzwa kutumiwa dhidi ya CCM inakuwa ni vurugu?
 
Hizi ndio siasa za bongo,fitna tupu hakuna lolote.Sasa wekeni mpiga kampeni wa Bn,hili awe mwenyekiti.Wakazi wa znz dawa sio kurudisha kadi halafu kuwapa kura,kaa na kadi usiwape kura.
naogopa cctv.

Kughushi nyaraka kwa minajili ya kudanganya umri ili upate uongozi ni ufisadi na ni kosa la jinai. Hivyo hatua iliyochukuliwa kwa huyu fisadi wa umri ni sahihi kabisa na kinachotakiwa ni kumfikisha mahakamani ili afungwe jela. Kinachoshangaza kwa hiki chama cha mafisadi ni kuwa mafisadi wengine ndani ya chama hawachukuliwi hatua zozote. Nadhani ndiyo sababu ya watu kulalamika juu ya fitna dhidi ya huyu fisadi kijana. Kwani hata No. 1 alijiuza kwa wapiga jura kwamba ni kijana.
 
Kuna jambo moja ambalo ningependa wenzangu tuwe tunaliangalia kila tukio linapotokea. Tujifunze kutazama zaidi, tuhamishe macho yetu kutoka katika mtu au watu wanaohusika na kuzama kwa mampana katika maudhui yanayolizunguka tukio.

Swala la UVCCM linachekesha na vilevile linatukumbusha namna tunavyoongozwa na mazoea. Tanzania tunapata bahati saana kujifunza kwa mifano tena iliyo hai. Hili swala la watu kutafuta nafasi, cheo au uongozi kwa mbinu yoyote ile limekua ni donda ndugu.

Pia tatizo jingine ninaloliona apa ni ufinyu wa fikra na umakini wa watu wengi. Hata hawa wajumbe wa UVCCM nao wana matatizo makubwa, kama wanachagua uongozi uliokosa sifa then they are part of the problem and they have to go as well. They have failed as well.

Kufumbia macho maovu ni dhambi kubwa na mshahara wake huwa mnene na wenyewe kuambatana na bonasi nono, yaani kudumaa kwa mambo na uwajibikaji. Kuna watu pale bungeni wamethibitika kuwa na vyeti bandia, kuna watu huko kwenye maofisi na wanavyeti hadi majina feki. Tatizo ili ni kama mzizi wa mwarobaini, limeenea kote nchini na hili la Masahuni ni tone katika bahari hii pana.

Kama kweli tumeamua kuchukua hatua, tuhakikishe sasa hili swala linakuwa ni vita ya kila mtu mahali alipo, tuondokane na viongozi, watumishi na wafanyabiashara feki (wenye vyeti na nyaraka za kugushi).

Ningependa kuona na sheria inachukua mkondo wake tena kwa uwazi na kasi. Maaana imeishaonekana kuwa mtu ameghushi vyeti. Tazama benki zinavyochukua hatua pale mteja anayegushi hundi. Polisi hufika mara mojja na kumbeba mtuhumiwa na mara moja taratibu za kesi huanza.

Sitashangaa kusikia idara husika zikitupiana mpira kuhusu jinai iliyo mbele yetu.
 
Hapa kuna mambo yanawachanganya watu:

Baadhi ya Wazanzibari wanamtetea Masauni pamoja na kwamba kafanya kosa la jinai kwa kufoji kuhusu umri wake na wakati huo huo wakiwalaumu waliokuwa kinyume na kitendo cha kijinai cha Masauni.

Unapopinga maovu kwa kushabikia maovu mengine ndipo hakuna mtu atakayekuelewa! Tena huyu Masauni afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za kufoji umri, sio kama JK alivyosema eti "ni kijana mchapakazi, atapewa kazi nyingine!" Sheria ni msumeno, ikate kote kote!
 
...sio kama JK alivyosema eti "ni kijana mchapakazi, atapewa kazi nyingine!" Sheria ni msumeno, ikate kote kote!

Anaandaliwa U-DC huyu. JK amesema atapangiwa kazi nyingine! Si unajua vyeo vingi vya kuchaguliwa NCHI hii watu wanaghushi, wanahonga, wananunua kura kuvipata?
 
MSIKILIZENI MWENYEKITI WAO SASA - KWELI THIS GUY IS A JOKE!!!!!!!

JK: Masauni kajimaliza mwenyewe

Wednesday, 19 May 2010

kikweteutabiri.jpg

Jakaya Kikwete

MWENYEKITI wa CCM Rais Jakaya Kikwete, amepiga msumari wa mwisho kwa aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Hamad Yusuph Masauni, akisema alijimaliza mwenyewe kwa kutokuwa mkweli kuhusu umri wake na watu wasitafute mchawi.

*ADAI HATUA ALIYOCHUKULIWA KAMA YA NAPE, BENNO MALISA
*ASEMA NI USHUJAA KUWANG'OA VIGOGO


Leon Bahati, Iringa

Kauli hiyo ya mwenyekiti wa CCM taifa ilizidi kummaliza kijana huyo ambaye tayari alijikuta katika tuhuma nzito za kughushi umri ili achaguliwe mwaka 2008.


Rais Kikwete aliweka bayana hilo mjini hapa wakati akifunga mkutano tete wa Baraza Kuu la UVCCM, ambao ulifanya vigogo wawili wa juu wote kutoka Tanzania Zanzibar, ambao ni Masauni na Naibu Katibu Mkuu Nassoro Moyo, kujiuzulu.


Mwenyekiti huyo wa CCM, awali katika hotuba yake hakutaka kuzungumzia kwa undani sakata hilo, lakini baada ya kumaliza aliruhusu maswali na ndipo baadaye akauliuza wajumbe:,
"Hivi mlielezwa vizuri kilichomfanya Masauni ajiuzulu?"

Baada ya swali hilo ukumbi ulipuka kwa wajumbe kusema:,
"hatujuiii...hatujuiii...hatujuiii."

Jibu hilo lilimfanya Rais kuanza kufafanua kwa kifupi na kuwambia wajumbe:, " Kilichomponza Masauni ni kutokuwa mkweli kuhusu umri wake...Alikuwa na tuhuma za kughushi umri uliomwezesha kushinda uchaguzi mwaka 2008."


"Tulipochunguza ilibainika ni kweli alighushi, wakati wa uchaguzi alisema alizaliwa mwaka 1979, lakini ukweli alizaliwa mwaka 1973 na alianza darasa la kwanza mwaka 1979."


Rais Kikwete alisisitiza:, "Kwa hiyo hakuna aliyeonewa, aliyefitini na wala watu wasitafute mchawi katika hili. Hatua kama hii ilikwishafanyika kwa watu kama akina Nape (Nnauye)." Nape naye alienguliwa katika uchaguzi wa UVCCM uliopita.


Alisema taratibu za UVCCM mtu akishakuwa na umri wa zaidi ya miaka 31, hawezi kugombea nafasi kutaka kuchaguliwa kwani anakuwa amepoteza sifa inayohusika.


Mwenyekiti huyo wa CCM awali, aliwaonya vijana hao wa UVCCM kuacha magenge kwani watajimaliza wenyewe badala yake mambo yao yapatiwe ufumbuzi ndani ya vikao na taratibu za jumuiya na chama.


Mkuu huyo wa chama na nchi, alifafanua kwamba kama malalamiko yakipita katika njia na taratibu za chama ni rahisi kupatiwa ufumbuzi kuliko kuyaanika hadharani kama ilivyofanyika.


Hata hivyo, Rais Kikwete alimfariji kijana huyo mpole na mzito kufanya maamuzi magumu na haraka, akisema kwakuwa ni makakamavu na mchapakazi atapangiwa kazi nyingine hapo baadaye.


Katika hatua nyingine,
Rais Kikwete amewataka wana CCM kujiandaa kujibu mashambulizi ya wapinzani kuhusu tuhuma za ufisadi ambazo alisema anaamini, watazitumia kama mtaji wakati wa uchaguzi.

Awali, Makamu Mwenyekiti wa UVCC ambaye anakaimu nafasi ya Masauni, Benno Malisa, alisifia maamuzi ya kung'oka vigogo wenzake akisema ni ishara ya jumuiya kukomaa.


Malisa alitamba kwamba kitendo hicho kimeonyesha ushujaa ndani ya UVCCM na ni ishara ya ukomavu na ukuaji wa jumuiya.


Kwa wiki moja sasa, UVCCM walianza kurushiana makombora ya tuhuma nzito ambazo zilimtaja Masauni kwamba alighushi umri, taarifa ambazo zilisambazwa kwa njia ya waraka katika maeneo mbalimbali.


Gazeti hili ndilo la kwanza kuandika kuhusu wingu zito lililokuwa limetanda na kugubika mkutano huo wa vijana, huku duru zake zake za kisiasa za kuaminika, zikiweka bayana kwamba ilikuwa ni lazima kung'oka ama Moyo au Masauni au wote wawili, kitu ambacho kimetokea.


Yanayoshangaza:

1. Hawa vijana mazuzu kabisa, yaani m'kiti wao anajiuzulu wao hata sababu hawaijui na wala hawaulizi mpaka mkutano unafungwa.

2. Mwenyekiti badala ya kusema mkondo wa sheria utachukua mkondo wake kuhusu kughushi kwa Masauni anamwahidi kazi nyingine. Is this guy serious???????

3. Mwenyekiti anawataka wanaccm kujiandaa na mashambulizi ya tuhuma za ufisadi badala ya kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua mafisadi. Huyu mkulu anajua anachofanya lakini???
 
Tena huyu Masauni afikishwe mahakamani kujibu tuhuma za kufoji umri, sio kama JK alivyosema eti "ni kijana mchapakazi, atapewa kazi nyingine!" Sheria ni msumeno, ikate kote kote!
Mkuu,

Rais katoa kauli hii? Tena kwa mtu mwenye kufanya makosa yaliyo wazi? I still do not believe this!
 
Yanayoshangaza:

1. Hawa vijana mazuzu kabisa, yaani m'kiti wao anajiuzulu wao hata sababu hawaijui na wala hawaulizi mpaka mkutano unafungwa.

2. Mwenyekiti badala ya kusema mkondo wa sheria utachukua mkondo wake kuhusu kughushi kwa Masauni anamwahidi kazi nyingine. Is this guy serious???????

3. Mwenyekiti anawataka wanaccm kujiandaa na mashambulizi ya tuhuma za ufisadi badala ya kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua mafisadi. Huyu mkulu anajua anachofanya lakini???
Mkuu Nyambala,

Shukrani kwa point hizi na kuileta habari hiyo hapa.

Hivi rais anapotoa kauli za namna hii ikiwemo ile ya kubariki rushwa (takrima) hakuna hatua zozote za kumchukulia? Nothing can be done at all?

Hata siamini anataka wapinzani washambuliwe ati kisa ni tuhuma za ufisadi, hivi kweli rais anatoa kauli ya namna hii hadharani badala ya kutufahamisha ni hatua gani zinaendelea kuchukuliwa?

TIRED!
 
Mkuu,

Rais katoa kauli hii? Tena kwa mtu mwenye kufanya makosa yaliyo wazi? I still do not believe this!

Anao watu hadi ndani ya Cabinet yake wanaotuhumiwa kughushi vyeti. Amechukua hatua gani? Hii ndio Tanzania bwana! Zaidi ya tunavyoijua.
 
Kweli nchi haina uongozi, huyo Masauni ilitakiwa awe polisi kuhojiwa kwa kugushi cheti.

Sasa rais anamponza kwa kumwambia akitulia atapangiwa kazi nyingine. Muda sio mrefu atakuwa mkuu wa wilaya huyo.

Kwenye umoja wa vijana kumejaa watu waliogushi. Kuna wilaya moja mwenyekiti wa UVCCM mwaka 2008 aliandika kwamba ana miaka 28 wakati shule ya sekondari alimaliza mwaka 1988. Hapo ina maana alimaliza form four akiwa na miaka 8.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom