Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Naona kuna utata katika habari ya kwenye gazeti la mwananchi (hard paper vc online). ninaomba kunukuu sentensi zifuatazo kisha tujiulize ukweli ni upi:
Mwananchi online: "Habari zinasema kuwa Masauni alitakiwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake, lakini aligoma na kujitetea dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008"
Mwananchi hard Paper lililo mtaani: "Habari zinasema kuwa Masauni alijiuzulu saa mbili usiku baada ya kubanwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008.
Swali: ukweli ni upi?
Habari ya kwanza imewekwa jana usiku 9.52 pm, bila shaka ilinyofolewa kutoka kwenye computer kabla ya kuwekwa kwenye page. Baadaye habari ilipofanyiwa update (ya masauni kujiuzulu) ndiyo ikawekwa kwenye page na kupelekwa mtamboni!