Hatimaye JWTZ yaingia Kibiti, Ikwiriri na Mkuranga kudhibiti na kutafuta wauaji wa Polisi na RAIA

Tatizo lakibiti bila wanakibiti wenyewe kutoa ushirikiano ktk majeshi yetu litawasumbua sana askari wetu mm naamini kabisa hawa wanaofanya mauaji haya nwatu tunakula nao,kulala nao,nakushinda nao tukishirikiana wote kwa pamoja kutokomeza swala hili inawezekana
 
!
!
Nguvu gunia akili kijiko.
Nina wasiwasi na wewe unaweza kuwa mmoja wa wauaji hao hivyo unajaribu kudiscourage hyo movement ili uendelee na uhalifu wako!kwa hiyo kwa akili yako ndogo kama nukta unaona mauaji yalofanyika ni madogo ukilinganisha na nguvu inayoenda kutumika?!usinichefue ujue watu tushachafukwa tumeshapoteza ndg zetu kule!!mmxxiiiiuuu
 
Jwtz tangu lini wakafanya vita na wachawi??? Njia hiyo haitaondoa tatizo kamwe. Mimi ningeshauri kuunda kikundi kama cha hao wauaji wa kibiti. Ningeua kimyakimya yeyote anayeonekana kushangilia mauaji ya kibiti na ningeacha vikaratasi vyenye jumbe kama zilezile za wauaji washenzi. Lengo ni ku confuse hao wanaowasifia waanze kuwachukia na kuwataja wauaji ambao ni jamaa zao
 
Kweli kama tuna polis wanakamata wandamanaji na vibaka bora iwe hivyo ila wauaji wenyewe wafanikiwe kukatwa jspo wazima ili watueleze masaibu ya haya wanayofanya
 
Jwtz tangu lini wakafanya vita na wachawi??? Njia hiyo haitaondoa tatizo kamwe. Mimi ningeshauri kuunda kikundi kama cha hao wauaji wa kibiti. Ningeua kimyakimya yeyote anayeonekana kushangilia mauaji ya kibiti na ningeacha vikaratasi vyenye jumbe kama zilezile za wauaji washenzi. Lengo ni ku confuse hao wanaowasifia waanze kuwachukia na kuwataja wauaji ambao ni jamaa zao
hii approach ingekoleza tatizo zaidi ya kulitatua
 
Kutwanga maji kweny kinu...
Sasa wanaenda kupigana vita na nan?? Wauaji wasio onekan? Sio vita Iyo... Hawa watu hawaonekani hawajulikani...
Wanashtukiza...
Mashambulizi kama haya duniani n magumu sanaa...
 
Kwa uelewa wako tiss haipo jeshini? Acha kuangalia movie za kikorea na CIA za kimapenzi

Tafadhali sana mwache Joblee!. Tena usimguse kwa saabbu humfahamu. Ulimwona lini akiangalia film za kikorea za mapenzi? Kama uko frustrated usilete frustrations zako kwa Joblee. Ametoa mawazo yake tena kwa upole na unyenyekevu, wewe unamjibu kwa lugha ya kipumbvue ni kwa vile ufahamu wako uk chini.

Joblee yuko sahihi. Jeshi kama jeshi hawana uwezo wa kupambana na invisible enemy. Ndiyo sababu Joblee amesema habari ya matumizi ya intelijensia kwanza ili kubailni ukubwa na upana wa tatizo, ndipo nguvu zitumike!.

Sasa wewe unapomshapua mwenzako ambaye essentially ana hoja ya maan akuliko wewe, huoni kama wewe ndye mpuuzi tu unayeishi kwa hadith za kusadikika?

Ungelikuwa na ufahamu, ungekumbuka operation tokomeza ilivyomaliza watu tena innocents kwa kutokana na matumizi ya mabavu na mitutu bila intelijensia.

Tafadhali sana jifunze kuelewa hoja kabla hujatoa comments kwa sababu mwisho wa siku unaonekana insecure na ignorant!.

Tena usirudie kufanay ujing kwa Joblee kwa kuwa atakuabisha tu!
 
Wanajeshi wako vizuri kwa kupambana na visible enemies, sasa hao wanakwenda kupambana na invisible enemies... Nadhani Ngudu zetu wa TISS wangefaa zaidi.. Tofauti na hapo Game bado litaendelea
Nataraji kuona malalamiko mengi sana, ya wanajeshi kuua hata wasiohusika, hii ilikua inahitaji akili na sio nguvu, hapa ndio tunagundua TISS hawayawezi majukumu yao
 
Wale jamaa wa JWTZ hiyo ndio kazi yao yaani roho ilikuwa inawauma walipokuwa bench hawaitwi sasa ngoja uone shughuli
 
Nataraji kuona malalamiko mengi sana, ya wanajeshi kuua hata wasiohusika, hii ilikua inahitaji akili na sio nguvu, hapa ndio tunagundua TISS hawayawezi majukumu yao

Joblee yuko sahihi kabisa. Hii kazi ilikuwa ni yakufanyika na TISS badala ya majeshi na mizinga kwa kuwa ni vita ambayo adui hana label usoni. Adui ambaye huwezi kumtambua kwa lugha, umri, mavazi wala sura ala alama yoyote ile!. Joblee yukok sahihi kabisa katika hili. Tatizo ni kwamba TISS yetu iko busy na vyama vya siasa badala ya maadui wa nchi yetu kama hawa wa Kibiti. Joblee anachosema sasa ingawa jehsi limekwenda, lifanye kazi zaidi katiak intelijensia ili watu wasio na makosa wasidhurike!
 
wameingi mzigoni na silaha za kivita kupigana na nani hasa?

hakuna repoti yoyote ambayo imesha tolewa na wanausalama kua labda porini kuna kundi la wauwaji hivyo tunaenda kupambana nalo

swali linabaki kuwa wanaenda kupambana na nani?
Intellejensia ya jeshi ni nzuri zaidi kuliko unavyofkilia sizani kama watatumia nguvu peke yake..uzuri wa hawa jamaa huwa hawana siasa nyingi kwenye utaifa wamefundishwa cha kwanza in uzalendo
 
Hatimaye Serikali imepeleka kikosi cha JWTZ huko Pwani kudhibiti mauaji na kutafuta wauaji.

Kikosi hicho cha JWTZ kina wana jeshi wenye uzoefu mkubwa wa kivita na makomandoo kiasi.

Lengo kuu ni kuleta amani mkoa wa Pwani ktk maeneo hayo ambayo usalama wake umekuwa wa mashaka.
Kati ya TPDF na polisi nani ana ustadi wa uchunguzi katika mabo ya inteligensia ya raia? Sana sana watakwenda kuone raia. Hatuhitaji mabavu, tunahitaji akili kujua wauaji!
 
Na amani haisitawishwi na silaha bali maridhiano ya haki,na swali wao jeshi wanakwenda kupigan na nani?lazima wanazuoni walitakiwa kufanya utafiti wa kina na kuja na suluhisho la maridhiano ya kweli

Maridhiano kati ya nani na nani?

Au wewe mkuu unawafahamu hawa wauaji wa ndugu zetu kule Kibiti ni akina nani?

Unaweza kutusaidia wanachotaka ambacho unashauri kifanyiwe maridhiano?

Hao wanaitwaje ili tuwatafute na kukaa nao mezani kwa maridhiano unayoyataka?

Kama mnamadai yenu ni kwa nani? Mbona mnaua watu wasiokuwa na hatia ili mradi tu wawe na uhusiano wa karibu na serikali bila kujali vyama wala dini zao? Mnataka nini hasa kutoka kwa nani?

Unaweza kuwashauri wakajitambulisha hadharani kama ni majasiri na wana madai ya kwlei na wanayemdai ili wafanye hayo maridhiano. Ungelikuwa wewe ungefanya maridhiano na hewa?
 
ni heri jwtz kutumika kulinda usalama huko rufiji,kilwa na kibiti kama wanavyofanya kule drc congo na sudani....

ingawa mapambano ni magumu kwa kutowatambua hao magaidi.... ambao utumia silaha za moto dhidi ya raia asiyebeba ht kisu.
Mbona huku kilwa hatuna shida we baba tumeingiaje hapo????
 
Hapo zaidi ya kuwatia hofu wananchi lkn hakuna lolote la maana.

Hiyo ni vita ya watu wasiofahamika dhidi ya watu wanaofahamika. Lzm wasiofahamika washinde.

Ili washindwe lzm mbinu za intelligence colection, analysis na kuwatambua wahusika na makazi yao vifanyike la sivyo no progerss
 
Back
Top Bottom