Hatimaye Jerry Muro ashinda kesi yake

A Luta Continua! The struggle continues!
Down with the corrupt - Iko siku yatawakuta kama ya Laurent Gbagbo -
Pole Bwana Jerry!
 
hatimaye Mwandish wa habari Jeri Muro ameachiwa huru.mwandishi huyo aliyekuwa anafanya kazi TBC alikuwa anakabiliwa na kesi ya kudai rushwa...

sababu za kuachiwa ni zipi.......................hawawezi kumkatia rufaa?
 
sababu za kuachiwa ni zipi.......................hawawezi kumkatia rufaa?

Habari hii ni breaking News, habari kamili tusubiri kesho vyombo vya habari vitakapolonga kinogaubaga, tuwe na subira, ila cha msingi mpigania haki hatimaye haki imeshinda.
 
mdau mwenyekujua hakimu alisemaje kuhusu kumuachia kwake huru maana tusianze kushangilia kibubusa

Jerry Muro aachiwa huru na kesi yake imefutwa

Mtangaza wa Shirika la habari Tanzania TBC, Jerry Muro kesi yake imefutwa na yeye ameachiwa huru pamoja na wenzake. Hizi ni habri ambazo zimetufikia hivi punde kutoka Mahakama ya Hakimu mkazi wa Kisutu jijini Dar es Salaam. Jiunge nasi kesho ili upate habari kamili.

Chimbuko la habari: Gazeti la Mwananchi habari kwa ufupi
 
Jembe lingine limerudi ulingoni!! Taratibu ndo mwendo na katika kutembea watu hukumbana na vizingiti kibao lakini haviwafanyi kuacha kutembea!! So i hope, J Muro hatoacha harakati zake! God Bless u!
 
Kama MURO atafanya walau kasherehe ndogo kumshukuru mungu asisahau kumualika hasimu wake mkubwa kamanda KOVA. Huyu nafikiri ndiye aliyekuwa kinara wa mpango mzima maana nilijiuliza sana kwa nini kama alipewa taarifa za uhakika za MURO kutaka kwenda kuchukua rushwa kwa WAGE alishindwa nini kuwataarifu PCCB WAKAFANYE KAZI YAO akaamua kwenda front mwenyewe na kutumia pesa kibao za kuitisha press conference faster ili kuhakikisha anamchafua kila kona ndani na nje ya nchi?
 
Mtu anaomba rushwa, anakamatwa na wala rushwa, uchunguzi unafanywa na wala rushwa, ushahidi unatolewa na wala rushwa, mwendesha mashtaka mla rushwa na hakimu mla rushwa pia. Mnatarajia hukumu iweje hapo?

Angalia isije ikawa:

Kutoka 20:16 Usimshuhudie jirani yako uongo.

Kumbukumbu la Torati 5:20 Wala usimshuhudie jirani yako uongo.

Mithali 24:28 Usimshuhudie jirani yako pasipo sababu, Wala usidanganye kwa midomo yako.
 


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewaachia huru kwa mashitaka yote matatu yaliyokuwa yakiwakabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jarry Muro na wenzake wawili.


Hakimu Frank Moshi, alisema anawaachia washitakiwa hao kwasababu upande wa mashitaka umeshindwa kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi shaka.


Muro, Edmond Kapama pamoja na deogratius Mgasa walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba na kutaka kupokea rushwa ya Sh milioni 10 toka kwa aliyekuwa Muhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo Michael Wage.


Mashitaka yao yalikuwa ni ya kula njama, kuomba rushwa na kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU shitaka linalowakabili Mgasa na kapama.


Muro baada ya kutoka mahakamani alitangaza kwa wanahabari kuwasamehe wabaya wake wote ambao ni viongozi wa serikali baadhi na baadhi ya maafisa wa polisi na kuwataka waandishi wa habari kushikamana kuendelea kuibua uozo unaoendelea bila woga.


Katika hukumu, hakimu Moshi alisema baada ya kuangalia ushahidi mahakama ilikuwa na maswali ya kujiuliza kama upande wa jamuhuri uliweza kuthibitisha mashitaka dhidi ya washitakiwa ambapo shitaka la kula njama kwa nia ya kuomba rushwa ambalo linawahusu washitakiwa wote, ushahidi ulikuwa wa Wage.


Shahidi huyo wa tatu wa jamuhuri lisema alikutana na Muro kwenye mgahawa wa Califonia ambapo mawasiliano kati yao yaliendelea kwa njia ya simu ya mkononi.


Ushahidi huo ulikuwa hafifu kwasababu upande wa mashitaka haukuweza kuwasilisha karatasi ya mawasiliano kati yao kutoka kwenye kampuni ya mtandao wa simu (printout).


Vile vile alisema picha za CCTV iliyowasilishwa mahakamani ilikuwa ni kivuli kisichoonyesha sura za watu badala yake wangeleta CD kuonyesha kwenye video ili watu waweze kutambulika kwa urahisi.


Mawasiliano ni jambo la msingi kwasababu ili kula njama ni lazima mawasiliano yafanyike hivyo kuna mapungufu makubwa katika shitaka hilo.


Dereva aliyemwendesha wa Wage alidaiwa kuwa na Wage pale mgahawa wa Califonia walipokutana na Muro, alitakiwa kuletwa athibitishe kama Wage na Muro walikutana upande wa mashitaka hawakumwita shahidi huyo.


Katika shitaka la kuomba rushwa lilowakabili wote katika ushahidi wake Wage, alieleza Muro na wenzake walimtaka awapatie Sh milioni 10 watamsaidia kwenye tuhuma zinazomkabili lakini hakuwa nazo akawapa sh milioni moja mbali na ushahidi huo hakuna ushahidi mwingine wa serikali unaoonyesha kuwa walipokea fedha hiyo.


“Mahakama ilitegemea kuwe na ushahidi wa mawasiliano kama haupo wa kuona lakini hayo yote hayakufanyika,” alisema hakimu Moshi.


Muro alikamatwa ndani ya gari, mahakama haielewi ni kwanini kulikuwa na haraka hiyo kwanini asingeachwa wakakutana na Wage. Kwa upande wa hotel ya Sea Cliff ni sehemu ya watu yoyote anaweza kwenda.


Washitakiwa Mgasa na Kapama hakimu Moshi alisema hawakukamatwa eneo la tukio walikamatwa na kuunganishwa na halikufanyika gwaride la kuwatambua na cheti kuletwa mahakamani.


Shitaka la linalowakabili Mgasa na Kapama la kujitambulisha maafisa wa TAKUKURU mahakama ilisema halikuthibitishwa lina mashaka. Alisema washitakiwa walijitambulisha kwa moja anaitwa Dr na mwingine Musa.


Upande wa mashitaka ulitakiwa kufatilia mtaani kama majina hayo washitakiwa walikuwa wakiyatumia lakini hilo halikufanyika.


“Wage kama msomi ngazi ya uhasibu aliwezaje kukubali mtu ajitambulishe kwa mdomo kama afisa wa TAKUKURU bila kuonyeshwa vitambulisho na akakubali mahakama inapata mashaka”.


Aliongeza hakimu huyo hakuna vielelezo na ushahidi wa kuthibitisha bila kuacha shaka hivyo wanaachiwa huru kwa mashitaka yote.


Alisema Moshi risiti, pingu na miwani havikuwa na mgogoro katika kesi na kwavile vilipatikana kwa risiti basi arudishiwe muhusika na upande unataka kukata rufaa wana ruhusiwa. Wakili kiongozi wa kesi hiyo Boniface Stanslaus alisema taafifa atampelekea Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ataamua kama watakata rufaa.


Washitakiwa walifikishwa mahakamani Februari 5 mwaka jana kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu mkazi, Gabriel Mirumbe. Courtesy MICHUZI BLOG.
 
[h=3]JERRY MURO MARA BAADA YA KUFUTWA KWA KESI YAKE : Courtesy: MICHUZI BLOG.[/h]


Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.



Jerry Muro na mke wake wakitoka mahakamani.

Mmoja kati ya watuhumiwa waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya shilingi milioni kumi, Edmund Kapama akitoka katika chumba cha Mahakama huku akina na furaha kwa kuwa huru.

Nipo huru sasa.

Pascal Kamara wakili wa Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari nje ya mahakama ya kisutu.

Pokea Mvinyo Baba.



 
Siamini kama maneno haya yanatoka kwenye key board unayotumia Mwita na umetumia mikono yako na ubongo wako kuyaandika
Jerry hana hatia kwa mashtaka aliyofunguliwa
Kisheria hata TBC walifanya makosa kwa kuwa hakustahili kufukuzwa kazi (kama amefukuzwa) maana mtu anakuwa guilty of the offence baada ya mahakama kudeclare hayo kuwa ana hatia na hapo ndipo walipaswa wao wamfukuze kazi.
Ila iwapo amefukuzwa kazi kabla mahakama haijamdeclare kuwa guilty of the offence kisheria ni kosa
Na Jerry kwa sasa hana hatia ni mtu huru na hajapatikana na kosa alilostakiwa nalo na ana uhuru wa kuajiriwa na kupata ajira popote pale
Sema kama kuna sababu nyingine kama kudanganya elimu au makosa mengine ya Jerry as Jerry ila ana haki zote kama raia ikiwepo ya kuajiriwa

Kifupi ni kwamba Muro alikuwa anadeserve kupata nusu mshahara wake mpaka kesi itakapo kwisha. Na inasemekana baada ya Tido kuondolewa ndio murugenzi mpya akampiga chini na kwa maana hiyo Muro anayo haki ya kuishtaki TBC na kupata mpunga wa neema
 
Back
Top Bottom