Hatimaye aliyemchinja yule kada wa CHADEMA Arumeru akamatwa!

Status
Not open for further replies.
ritz Rejao, MAFILILI njoni huku mkaitetee ccm dhidi ya tuhuma za mauaji ya mwenyekiti wetu!

Subutu!!... kama utawaona utaniambia.hawa majangili wanatupora uhai,hadi fedha za kodi hawaachi kitu,hata hao ulio wataja utakuta wanatumia kodi yetu kuja hapa jamvini kukanusha mambo ya msingi
 
Last edited by a moderator:
Huyu adhabu yake inatakiwa awe anabakwa kila siku huko gerezani.
 
Hapa jeshi la polisi limefanya kazi yake iliyoainishwa kwenye Katiba ya Nchi.Nitafurahi zaidi wakifuatilia wale waliowanyonga wale vijana wanne.Wakipatikana wauaji hao tutazuia mauji ya kipuuzi kwenye jamii yetu na kuongeza confidence na uchumi wetu.


Polisi wanafanya kazi vizuri sana pale ambapo mafisadi wakubwa hawakuhusika!
Kama kawaida, watuhumiwa wa chini ndio polisi inaweza kuwakamata!

Mawaziri na wakurugenzi waliouwa maelfu ya watanzania kwa ufisadi mbona hawakamatwi?
Wangapi wanakufa kwa ajali zinazotokana na uzembe wa TBS?
Wangapi wanakufa kwa vyakula na madawa feki?
Wangapi wanakufa kwa malaria kwa kukosa dawa?
Wangapi wana/takufa kwa kansa ya moshi wa magari mabovu na msongamano wa magari Dar?
Wangapi wanakufa kwa kuuawa na majambazi?
Wangapi wanakufa kukosa kwa maji?

Hata hivyo nawapongeza kwa kumkamata huyu jamaa.
Na pongezi zitakuwa na maana zaidi watakapokataa maelekezo ya mafisadi na kufichua yote yaliyotokea
 
MTUHUMIWA HUYO ALMAARUFU KWA JINA LA (CHEWAJA)ALIKUWA NI MPANGAJI KATIKA NYUMBA YA MAREHEMUNI (waliishiwote myumba moja) NI MZALIWA WA SINGIDA,MKAZI WA ARUMERU MASHARIKI,AMEKAMATWA DODOMA AKIWA KWA MGANGA WA KIENYEJI,AWATAJA ALIOSHIRIKIANA NAO KATIKA MAUAJI HAYO MMOJA WAPO NI KADA WA CCM NA PIA NI MWANYEKITI WA KIJIJI,VILIO VILITAWALA BAADA YA MTUHUMIWA HUYO KURUDISHWA KIJIJINI CHINI YA ULINZI MKALI WA JESHI LA POLISI KUONYESHA OLIKOFICHA VIFAA VYA MAUAJI WANANCHI WAPANDWA NA HASIRA WATAKA KUMUUA ASKARI WAZUIA,SILAHA ZAKUTWA SHAMBANI KWA MWENYEKITI ZIKIWA ZIMEFUKIWA CHINI AMBAPO BAADA YA KUFUKUA WALIKUTA BUNDUKI MBILI,KISU PANGA,NA MASHINE YA KUKATIA MITI ILIYO TUMIKA KUMCHINJIA MAREHEMU ALIFANYA MAUAJI HAYO KWA UJIRA WA SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI MBILI(SH.2.000,000/=)YASEMEKANA HATA UKO SINGIDA ALIKIMBIA KESI YA MAUAJI.

source:MIMI MWENYEWE LIVE KUTOKA KATIKA TUKIO.

huyu jamaa alitumia machine ya kukata mti kuchinja binadamu mwenzie wakati alikuwa na bunduki.....ni bora nagemtia risasi tu
 
MTUHUMIWA HUYO ALMAARUFU KWA JINA LA (CHEWAJA)ALIKUWA NI MPANGAJI KATIKA NYUMBA YA MAREHEMUNI (waliishiwote myumba moja) NI MZALIWA WA SINGIDA,MKAZI WA ARUMERU MASHARIKI,AMEKAMATWA DODOMA AKIWA KWA MGANGA WA KIENYEJI,AWATAJA ALIOSHIRIKIANA NAO KATIKA MAUAJI HAYO MMOJA WAPO NI KADA WA CCM NA PIA NI MWANYEKITI WA KIJIJI,VILIO VILITAWALA BAADA YA MTUHUMIWA HUYO KURUDISHWA KIJIJINI CHINI YA ULINZI MKALI WA JESHI LA POLISI KUONYESHA OLIKOFICHA VIFAA VYA MAUAJI WANANCHI WAPANDWA NA HASIRA WATAKA KUMUUA ASKARI WAZUIA,SILAHA ZAKUTWA SHAMBANI KWA MWENYEKITI ZIKIWA ZIMEFUKIWA CHINI AMBAPO BAADA YA KUFUKUA WALIKUTA BUNDUKI MBILI,KISU PANGA,NA MASHINE YA KUKATIA MITI ILIYO TUMIKA KUMCHINJIA MAREHEMU ALIFANYA MAUAJI HAYO KWA UJIRA WA SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI MBILI(SH.2.000,000/=)YASEMEKANA HATA UKO SINGIDA ALIKIMBIA KESI YA MAUAJI.

source:MIMI MWENYEWE LIVE KUTOKA KATIKA TUKIO.

CCM ni kawaida yao.. Japokuwa nawashangaa sana lakini pia niungane na watanzania wengi kuwalaani... Kila siku naiombea CCM idumu ili ishuhudie Kuapishwa kwa Kiongozi kutoka Chadema kuwa Rais wa Tanzania..
 
NI NANI NDANI YA SERIKALI YA CCM ANAYEUA VIONGOZI WA UPINZANI PAMOJA NA WAFUASI WETU NCHINI KILA UCHAGUZI UNAPOFANYIKA POPOTE PALE??

Sisi wananchi wanachama wa upinzani hivi sasa tunahitaji Tume Huru isiofungamana na CCM, CHADEMA wala CUF, ije ichunguze mauaji ya viongozi viongozi wa vyama vya upinzani nchini pamoja na wafuasi wetu KILA UCHAGUZI UNAPOFANYIKA nchini.

Tume hiyo itakapoundwa na 'jumuiya ya kimataifa' kama vile EAC na au ICC, ichunguze sura chafu za mauaji ya aina hii tangu chaguzi za kule Pemba, Unguja, Igunga na Arumeru Mashariki. Kati ya majibu tunayotaka kujua ni je MAUAJI HAYA AMBAYO ZINA DALILI ZOTE ZA KUITWA 'MAKOSA YA JINAI DHIDI YA UTU WA BINADAMU' (Crime Against Humanity) zimetendeka nchini mwetu kwa ufadhili wa serikali au la??

Katika uchunguzi huo vile vile viangaliwe baadhi ya kauli tata na HATARISHI mno zilizowahi kutolewa na na baadhi ya viongozi serikalini kabla ya matukio haya kutendeka, mikutano waliokua nayo ya siri sehemu mbalimbali ya Jamhuri yetu hadi huko huko vijijini kulikotendeka mauaji ya kutisha.

Naam, nasema pia ni vema tupate ukweli na ukweli mtupu juu ya nani au kundi gani hilo ambalo limekua likiwachinja WaTanzania kiasi hiki. Wananchi tupate kujua maana na uwepo wa JESHI LISILO RASMI LA GREENGUARD na kazi zake nchini pamoja na mmiliki wake kule wanakowajibika.

Watu tunaposema kwamba serikali ya CCM inaishi kwa mtaji wa damu ya WaTanzania walalahoi ili sauti zetu zisikike na wala HAKI KATIKA UCHAGUZI wowote ule usipatikane, wenzenu huwa tunajua tunachokisema.

Mauaji ya viongozi wa kisiasa kambi ya upinzani pamoja na wafuasi wetu usiposhugulikiwa kiundani zaidi kwa njia ya kutumia chombo huru kisheria, WaTanzania bado tutakua hatujapata dawa ya kudumu kisheria ili jambo hili lisijirudie nchini mwetu tena.

Zana HATARI zinazodaiwa hapo juu kutumika kuchukua uhai wa Ndg Mbwambo ni aina za zana zisizozoeleka kwa mwananchi wa kawaida hasa waishio vijijini kama kule alikouaua marehemu.

Ujira wa shilingi Tsh 2,000,000/- ni kiasi cha fedha ambacho hakuna mwanakijiji tu wa kawaida anayeweza kuikusanya kisha akaitumie kwenye kulipia ujira kwa 'Israeli Mtoa Roho' kivile. lizotumi.

Ushiriki wa kiongozi wa kiserikali kwa maana ya Mwenyekiti wa Kijiji sasa ndio kabisaaaa inavuruga kabisa mambo hapa kwamba Mbwambo hakuuwaua kwa kubabatizwa tu na walevi barabarani bali ni kwamba jambo hilo linahitaji kufunuliwa zaidi kama kweli au laa haikupangwa, kupewa baraka, kugharamiwa na kutekelezwa na serikali ya CCM.

Mhe Tundu Lissu, Marehemu Mbwambo wa AruMeru Mashariki, Ismail wa Arusha, na yule ndugu yetu mkazi wa Mburahari aliyechinjwa Igunga, Mwenyekiti wa CUF Kibaha pamoja na wananchi kibao waliopoteza maisha mikononi mwa
Jeshi la Nape na Mwigulu Nchemba na maelekezo ya wakubwa wake, roho hizi zinalilia HAKI NA KUTETEWA NA CHADEMA leo hii na wala si kesho.
 
Huyo jamaa ni hatari kuliko sumu! Anatakiwa akatwe korodani zake zitupiwe mbwa!
 
Anaua kwa kutumia msumeno? Huyu jamaa hatari! Nipeni dk 10 tuu na yeye, atasema vyote! Looh
 
Nahisi hao jamaa walikuwa na bifu binafsi, pengine mambo ya chama hamna kabisa hapo!

Inawezekana business au mademu!
 
Hivi huyu mtu ana dini kweli? Well, wengine kumwaga damu kwao ni abada.
 
Inasikitisha sana sasa tunaanza kuamini kuwa watakaoleta machafuko Tanzania ni CCM hapa akuna ubishi kabisa kwani tumeona wenyewe na tunaendelea kuona kama mwenyekiti alishiriki hii ni kwamba CCM imeshiriki kwa namna moja katika mauaji haya jamani tunaipeleka wapi nchi yetu.

Ningependa kujua mtoaji mil 2 ni nani na sielewi kuondoa uhai wa mtu kungesaidiaje kisiasa na na hasa mtu 1 ?
 
Hata mimi naunga mkono mwajiri atafutwe akamatwe na inabidi amtaje kwani haiwezekani ni huyo Mwenyekiti wa CCM?
 
Jamani huu ndio mpango wa CCM kwa sasa! Wanakodi wahuni kuwapiga wanaowapinga kwa hoja ili kuzuia wimbi la mabadiliko, Makamanda muwe macho saana. Nasema hivi kwa sababu ninawajua vizuri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom