Hatimaye aliyemchinja yule kada wa CHADEMA Arumeru akamatwa!

Status
Not open for further replies.
Mh,hii ni laana!!!!!!!
Yaani ujira wa mil 2 unamshawishi mtu kutoa uhai wa mwenzake?Suala wala sio umaskini bali ushetani ulio pitiliza!!!!!
Unaishi dunia nyingine wewe. Sasa hivi tumefikia mahali ambapo sh elfu ishirini (20,000/=) inatoa roho ya mtu. Jeshi la watu wanaoweza kuua wenzao kwa malipo ya 20,000/= ndiyo silaha pekee waliyobaki nayo CCM.
 
jamaa atakuwa alikwisha tumiwa sana kwenye mision za namna hiyo na magamba,nafikiri wale polisi ccm hawatatueleza ukweli wote iwapo huyo killer akiwataja vigogo wa nyinyiem,ilifaa ahojiwe na G,Lema.kamanda
 
Du! huyu jamaa ni mkatili sana ,hata kama ni chuki hiyo imepitiliza

Nadhani chuki ilikuwa kwa aliyemtuma ila aliyemuu ni tamaa ya hela japo naamini zilikuwa zimekwisha kwani hela kama hizi hazidumu hata siku moja!
 
Pongezi kwa Jeshi la Polisi. Sasa ingieni kwa undani kujua driving force ilitokana na nini, fukua fukua ili kila mtu apate haki yake kulingana na matendo yake. Kila la heri polisi wetu.

Wakiamua wanaweza...ila sasa wasiingize siasa ndani ya uhalifu
 
ehuu natamani hi habari iwe ni ya kweli bandugu coz no source naona watu wanathrd kama hawana akili nzuri in fact umenikumbusha moja msiba ulioitesa nafsi yangu 2012.
 
Polisi wamefanya kazi nzuri katika hili wanastahili pongezi. Kitu kimoja ambacho nimeshindwa kukipata kwenye huu ujumbe ni juu ya nani aliyemtuma huyu muuaji, maana taarifa inasema alifanya mauaji haya kwa ujira wa milioni mbili. Je ni nani aliyelipa hizo fedha?! naomba kama kuna mwenye kufahamu juu ya hilo atujuze!
 
Hapana shegaboy! Usihukumu haraka hivyo kwamba ccm ni wauaji kwa maana sidhani kama kulikuwa na kikao cha ccm kilichokaa na kupanga mauaji.Kinachotokea Arumeru Mashariki ni kama kilichotokea Nduli Iringa. Ya Iringa tuyaache maana yapo mahakamani. Lipo tatizo za ukereketwa mkali. Wapo wanachama wa ccm ambao wanajiona wao ndo ccm yenyewe. Chama chake kikishindwa anaona ni yeye ameshindwa na anaumia sana kuliko mwenyekiti wake wa taifa. Ndo hao wanafanya vitendo vya ajabu si chama.

Kwa hiyo tofautisha matendo ya mtu binafsi na misimamo ya chama.
wale waumini wa Vitabu Vitakatifu wanasema, kuamini na kutenda ni vitu viwili lakini haviwezi kutenganishwa (inseparable).
Kwa hiyo tuseme walioua waandamanaji wa Arusha wakati wa Mkutano wa cdm (intelijensia) tutashindwaje kuamini kuwa walikuwa na 'ukereketwa' uliopitiliza!?

 
Nafikiri hawa magamba sasa muda wao umefikia mwisho, La maana jamaa abinywe mahali mpaka awataje hawa big potatoes waliomtuma kwenda kufanya kazi hiyo katika ujira huo, na hizo silaa za maangamizi aseme vizuri namna alivyozimilik
 
Inasikitisha sana sasa tunaanza kuamini kuwa watakaoleta machafuko Tanzania ni CCM hapa akuna ubishi kabisa kwani tumeona wenyewe na tunaendelea kuona kama mwenyekiti alishiriki hii ni kwamba CCM imeshiriki kwa namna moja katika mauaji haya jamani tunaipeleka wapi nchi yetu.

Tunataka kupata na list ya waliochanga hizo milion 2 kwani tunajua mwenyekiti wa Kijiji hana uwezo wa hizo hela na hata kama anazo hawezi kufanya kazi ambayo haina faida kwake lazima kuna wakubwa wametoa hela.
 
Mkwara aliomwaga kamanda Lema na Nassari imesukuma polisi wa Magamba kufanya kazi kwa speed! inaelekea CDM ikichukua nchi hapo 2015 jeshi la polisi litasafishwa na kufanya kazi kwa speed and standards!!maana kama muuaji asingepatikana ontime sheshe lingezuka siku sii nyingi!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom