Hatimaye afande Kova ajibu shutuma juu yake

muhimili huu wa mahakama ambao haujawahi kukanusha uhusika wake ktk kupokea Rushwa kwa kiwango cha kutisha sasa umeingiliwa na ccm kama kimbilio muhimu ktk harakati zake za kijinga na za kitoto kuokoa jahazi linalozama kwa kasi ya ajabu, Lakini juhudi hizi za ccm zimepoteza matumaini kabisa,
 
UKITAKA KUJUA ATHARI ZA SINEMA ZA KIHINDI KURATIBIWA NA UONGOZI WA KI-CHINA BASI KAMUULIZE ALHAJI AFANDE SELE PALE 'MAMBO YA NDANI' NA JINSI GANI ALIVYOLITIA KOVU LA KUDUMU JESHI LA POLISI

Kwa akili tu ya kawaida, busara zinatuamrisha ya kwamba pindi tunapoinuia kutengeneza sinema ama yaa Kihindi, Kimang'ati au hata ya Kichina, ni vema tukawapa nafasi watu wenye ufahamu mzuri na tamaduni za mahali husika wakatusaidia kuratibu mambo.

Ajabu na kweli ni kwamba katika jaribio la kumchukua uhai Dk Ulimboka, majina ambayo yatokea kutajwatajwa yametokea kuwa ni wa upande fulani tu. Madai ya Uhalifu huo ni wao, Uchunguzi ni wao, Usemaji ni wao, na hata Uratibu mzima bado ni wao tu.

Hakika hili kidogo linatatiza kwa kuwa jeshi letu la polisi sote tunajua halina dini lakini kwa mwenendo huu wa mara Abeid wa Ikulu, Ahmed Msangi wa Kanda Maalum, Selemani Kova kubwa lao, Saed Mwema ambaye ndiye Back-stopper hapo -- mmmmmmhhhh!!!

Japo ni jambo ambalo halisemwi wazi wazi na wengi LAKINI mmmhhhhh!!! Kwa nini na kwani kuna nini??? Siku zote Matokeo ya mambo kama haya, pengine ni ajali tu imetokea hadi hapo, mwisho wa siku huleta taswira kama vile ya Picha ya KIHINDI kuratibiwa vile na WACHINA.

Mtu akiangalia ki-undani,
pale kwenye ONYESHO LA PILI, jinsi gani ka-Gwajima (Mkristo) na Joshua (nalo jina la kikristo ila mbebaji wa jina hilo HATUNA UHAKIKA na dini yake mpaka atakapotuthibitishia kwa kinywa chake mwenyewe) wanavyovutwa kwa nguvu zote kuwa sehemu ya mchezo katika filamu hii - yote yanayojitokeza ni VITUKO VYA KARNE katika historia ya mambo ya kipolisi duniani kote.

Kwa watazamaji wapya wa picha hii ya '
KOVA KATIKA MABAWA YA MABADILIKO YA NGUVU YA UMMA NCHINI TANZANIA', kwa kukumbushia tu, ONYESHO LA KWANZA ilianzia pale Leaders' Club na kuishia Mabwepande Tegeta na walioonekana mwishoni mwa picha ile ni Mama Kijo Bishimba, Mzee Mwanakijiji, Mjeruhiwa Dk Ulimboka pamoja na wanakijiji katika yale mandhari asili ya MabwePande.

Sababu ya kusema hivyo ni kwamba Alhaji Afande Sele (Kanda Maalum Jijini Dar), kwa kosa moja tu la kutokufahamu desturi na taratibu za madhehebu ya ki-Kristo ki-ajali kabisa kajikuta AMEUNGUZA PICHA ZIMA kwa kudai kwamba mgeni wake Joshua Muyungi alienda na AKATUBU katika kanisa la Nabii Mkuu na Askofu Gwajima juu ya uhusika wake kwenye jaribio la kumua Dr Ulimboka. Hii ndio maana kila wanapojaribu kuunganisha picha hizo mbili hali inaendelea tu kuwa kama mafuta ya taa na maji kwenye maabara zetu za kibongo hizi.

Ukweli wa mambo ni kwamba mbali na Kanisa Katoliki ambako watu hujichagulia kwenda kwa Padre na kutubu dhambi zao, madhehebu mengine yote ya ki-Kristo hayana utaratibu huo. Lakini kwa kuwa Alhaji alikua anatafuta MNOGO WA PICHA YENYEWE ndio hapo maini yakaingia nyongo.

Kama bado tu mtu hajashtuka kitu hdi hapo, hivi watu bado tu hamjiulizi kwa nini
ONYESHO LA TATU (linalotegemewa kuwa ndefu sana mpaka hadhira kujikuta wachapa tu usingizi badala ya kuendelea kufwatilia picha) la filamu ilivyoanza kwaa usiri mkubwa katika mahakama ya Kisutu na kwamba wahusika wote huko wakawa ni WATU WA KUFIKIRIKA tu huku wengine wakidaiwa kuwasili tu kutoka katika taifa la KUSADIKIKA ('nimewasili na bado ninaendelea kuwazoea').

Mpaka hapa wala mtu hahitaji kutngaziwa kwamba kwele Alhaj Afande Kova kalitia kovu chombo hiki, tulichopata kukiamini na kukithamini sana miaka hiyo, kwa namna ambayo itachukua miaka kuturudisha imani sisi Umma wa Tanzania.

Sasa kilichobaki pengine ni wahusika wkuu wa filamu hii warudi tena mezani ili waje na ubunifu mwingine maana huu wa sasa ndio kama hivo umekwishagonga mwamba.


Dooh! Mkuu uandisgi huu umenikumbusha mbali sana. Enzi ya akina Ben R Mtobwa, marehemu.
 
wel said.mchungaji kaumbua.Na makanisa kova aliyoyawekea uongo kachemsha hata kama watamshinikiza mchungaji picha imeharibika.Haya makanisa huwa yanalaani sana toba kupitia binadamu.Kova sijui anatafuta nini katika TV hku akijua kwa fikra, kwa matendo na hata kwa SURA yake hayupo presentable.Anongea kama taahira.

Wanatangazia taifa ujinga kuhusu silaha za kivita kushikwa dar zimepitaje mipaka yote bila inteligensia yao kuwa aware?HAwa jamaa wamekuwa na tabia ya kudhalilisha sana ukristu huku wakiwa waislam, wameanza na madawa ya kulevya, wamekuja hii scandle ay dr. Uli wameanza mamabo ya sadaka kama alivyojiingiza kwa nguvu rostam.Huku wakishangilia uamsho.

CCM imekufa vibaya.

Watamshika mchungaji kivipi? wakati kova anatoa taarifa yake si walikuwa tayari wameshampeleka mahakamani kimyakimya?
 
Kama katiba inaturuhusu hakuna, narudia hakuna, anayeweza kutuzuia tukitaka hizo taarifa. Kama kuna sheria inayozuia sisi kupewa taarifa na kutoa fikra zetu basi sheria hiyo inakinzana na sheria na hivyo nisheria batili.

Gerald, kuuuita huu udikteta movie, ni kubilittle, umuhimu wa suala zima, tulipe hili sualka mtazamo wa kisheria na kikatiba zaidi. Tusichukulie kama movie no, no please this is a serious issue.

ngambo

Mkuu inabidi hii ya wafungwa waliokusudiwa then ikastukiwa ikaja hii ya kova, mkenya na mchungaji ngwajima tuiite movie cause aiingii akilini kama professsional agency like kova from intelectual security kutoa report kama hii public.

Sasa kwenye seriously issue ni hii, Tunaomba upelelezi ufanyika na watu wengine cause serikali ndio mtuhumiwa number 1 (Msangi).

Ulimboka apewe airtime ya nini kilichomtokea kwenye TV kama mchungaji ngwajima alivyojisafisha jana na kwa ulimboka iwe hivyo hivyo.

Na hii mada irudi bungeni ijadiliwe ni nini kilichomtokea ulimboka pia serikali na madoctor kwa ujumla serikali bado aijatueleza kuhusu afya zetu cause sisi wananchi atuna mkataba na madoctor ila tunamkataba na serikali so inabidi itueleze mstakabali mzima wa afya zetu inaelekea wapi.

Bila hivyo inanibidi hivyo vya kina kova niziite movie tu.
 
Last edited by a moderator:
.........................




Mie nadhani huu ushauri unatoka kwa Kikwete mwenyewe..

Polisi hawawezi kuwa wajinga kiasi!!!


Lazima kuna mtu asiekuwa na taaluma hiyo anawasukuma nyuma ku act juu ya jambo hili...

Aibu gani hii!! mie naogopa hata kutembea tembea siku hizi!

Nchi kakabidhiwa c.h.i.z.i.!! anaweza kuamua kutumaliza wote!!


.
kama wametumwa na wale IGP Mwema alipowahi kusema hawagusiki tusitegemee lolote.Bottomline mwananchi hana mlinzi na hili ndo la kutizama kabla ya kuendeleza nguvu ya umma kwasababu wao wana silaha.
 
Hivi jamani hii tabia ya jeshi la polisi kupenda kutumia umbea kujitetea imetoka wapi? Haiwezekani muhusika kapayuka tu coz hana akili nao waseme ndo mwenyewe. Kwanza huyu mtu wangetakiwa wamuache akili irudi vizuri, afu watumie tumu huru na wana psycholojia kumhoji, na kutumia vifaa kufanya uchunguzi ...kwani mtu aliyeua NDA fingerprint huwa si zinaonesha? what about other forensic investigations? naona siku hizi umbea ndo evidence. Kwanini walivyoambia Msangi ndo muhusika wasingemkamata na kufanya uchunguzi na kwake? coz hatujasikia hata maneno ya msangi kutoka mdomoni mwake kama alivyotamka huyo anayesemekana kuwa mwehu aliyetumwa au kupakaziwa? Nadhani serikali kwa kweli kwa sasa hivi inatafuta mbinu zozote za kujisafisha, maana ni serikali dhalimu ambayo haina kibali wala utukufu mbele za Mungu...maovu yenu yamemfikia Mungu kwenye kiti chake cha enzi na Ole umefika. Coz hamna tofauti namfalme Pharao alivyowatesa wana wa Israel.. NOW ITS YOUR DEAD END!
 
Mi ninachoamini Kamanda Kova hakusema Gwajima alimkamata na kumpeleka polisi. pili Mch. Gwajima alisema walizi wake ndiyo walimkamata huyo jamaa je walimpeleka wapi? je walimkamata kwasababu zipi? Nani waliwataarifu polisi? Sawa tuseme katengenezwa je huyu jamaa ilikuwaje aseme aliyemtuma ni mtu wa serikalini? kwanini Kova asilifiche hilo akaliweka wazi? Mch. Gwajima anasema kwake watu hawaungami lakini akumbuke kuwa Kova alisema huyo mtu ndiye aliye sema hayo na si Gwajima. Nadhani Gwajima anajaribu kutafuta umaarufu baada ya umaarufu huo kupotea aweke wazi aache kubwabwaja, kwanini nasema hivi? kwasababu Gwajima alitamka kuwa huyu mtu atakuwa hana akili timamu au ametumwa mimi siyo wa kudanganywa na vipesa sasa aseme alipewa pesa na nani? Naamini huyu bwana Gwajima ana siri nzito anapaswa kuhojiwa maana kanena mwenyewe. Huyo Msangi anayemsema inajulikana wazi kuwa ilikua propaganda ili iundwe tume huru. Mchungaji na Nabii Gwajima namkumbuka sana alivyosema anaweza kumfufua Amina Chifupa na sakata lake na Mchungaji na Nabii Geor Davie. Bwana tunachezewa akili na hao jamaa wote siwaelewi kabisa. Nadhani nahitaji kuanza kazi ya uandishi wa uchunguzi zadi
wacha kumshambulia gwajima hajasema kwake hawaungami, bali alisema kuungama kwao hakuhusishi kuonana ana kwa ana baina ya muungamaji na kiongozi wa dini utaratibu huu unafanyika na kanisa katoliki. Jeshi la polisi na usalama wa taifa wanajichanganya sana siku hizi na haya ni matokeo ya kupeana nafasi hizo kindugu matokeo yake wameakyumuleti mapoyoyo matupu yenye uwezo mdogo wa kupanga na kutekeleza mikakati yao.
 
Eti serikali nayo inalia sawa na sie walalahoi,

Hivi sasa na wao wameibuka na uzushi wa kutafuta kusawazisha kwa mashaibu ya Dr Ulimboka kwa kudai eti afisa wake 'kutekwa, kupigwa na kutupwa katika msitu usiokua na jina na wala mdhurika wao huyo Mwanasheria wa NEMC wala hatibiwi popote pale'.

My foot kwa uzushi kama huu; naona sasa mambo yote yameshakua 'Geresha ya Kova' kila mahala.
 
Back
Top Bottom