Hatimae Polepole awaangukia Maaskofu

Yaani iwe siri sirini tu?
Mbona sielewi miye?
Kwani mahubiri huwaje?
Huwa chumbani jamani?
Sielewi kitu jamani miye
Mahubiri kuwa siri?
Hii ndio Tanzania?
Kila mtu anaililia?
Raiss anatubania?
Vyuma kutukazia?
Chatle kupendelea?
 
Tatizo wamezoea siri na watu wasiojulikana ndo maana wanataka iwe siri kumshauri bwana mkubwa
 
Polepole anazidi kuwagombanisha watu badala ya kuwafanye wawe kitukimoja kupitia itikadi za dini,kwani anasema kwamba kiongozi wa dini akiwa na mwelekeo wa chama Fulani mtu wa chama kingine hawezi kwenda kwake kwa maana ya kwamba wana ccm wawe na maaskofu wao na wana chadema wawe na maaskofu wao kwa maana tu,wote ni wanachama wa chama husika,ameshindwa kuelewa kwamba askofu anaweza kuwa na itikadi ya chama Fulani lakini kwa upande wa dini akawa anawaudumia watu wa vyama vyote,hilo yeye Polepole halioni na kama ameshindwa kuliona hilo vipi ataona ualali wa mwana ccm kumuudumia mwana chadema katika hali ya kawaida? watu wenye mawazo kama ya Polepole hawatufai kabisa katika nchi hii ndio maana sasa hivi inaanza kujitokeza kwamba mwana chadema akipata tatizo kama alivyopata Lisu mwana ccm anashindwa kwenda kumuona na akienda anafikiriwa vibaya, hivyo polepole lazima aonywe mapema kwa huo mtazamo wake

Fikra za kipumbavu walizo nazo baadhi ya watu kipindi hiki ni kuhusisha hoja na vyama.
Viongozi wa dini wajibiwe hoja walizozitoa au marekebisho yafanyike tusonge mbele.
Tunahitaji watu wenye mtazamo mpana, wanaowaza kuanzia ndani mpaka nje ya chama (taifa hadi kimataifa).
Hoja nyingi ni za jumla tu kwa wananchi wote, wenye vyama na wasio navyo.
 
Naona vinyamkera vimeanza kusukuma makabati na kuparamia masufuria huko magogoni.Vinginevyo lile joka lingesimama tena na kuanza kufokea watumishi wa Mungu.Kheri ya mwaka mpya.
 
Kupambana na askofu kakobe au kiongozi yeyote yule wa dini inamaanisha unataka kupambana na wananchi maanba wako wengi wanaoamini katika wao. Hivyo inapofika wakati unatakiwa tu uchomwe sindano ili upone jabo inauma inapoingia mwilini
Jakaya anawajua vizuri viongozi wa dini kwa kuwa wana ushawishi mkubwa kwa wana kondoo wao sasa huyu shetani anataka kupambana nao bila kujua mwisho wa siku ataumia
 
Mbona wanaomba kuombewa na kutaka kusifiwa hadharani?? Wakubali pia kukosolewa hadharani....

Mkuu hivi sasa kweli tuwaombee tu maana kama wanatishwa mpaka na Cartoons ujue pashakuwa parefu.
Dhambi zikishakuwa nyingi unaweza kuiogopa hata picha uliyochora kwa mkono wako, tuwaombee tu na kuwabembeleza wakatubu.
 
Ndugu zetu maaskofu wa DRC wao wameandamana kabisa kumpinga kabila kuhusu suala la uchaguzi, laiti maaskofu wote kabisa wangekuwa na uthubuti serikali lazima ingebadili mwenendo wake kwani hali za wananchi sio nzuri kabisa lakini tunaaminishwa hali ni nzuri.
 
Tatizo wamezoea siri na watu wasiojulikana ndo maana wanataka iwe siri kumshauri bwana mkubwa
Ushauri wa siri Pogba alishaukataa ndiyo maana hata watoa habari za ndani hapo magogoni wanalalamika chini2 jamaa hataki ushauri sasa inabidi Maaskofu wammegee dozi ya ugonjwa anaoumwa hadharani
 
Sindano zimeanza kuwaingia sasa.
IMG-20150712-WA0051.jpg
 
Kila muumi ni anaamini kuwa ,Serikali iliyopo au iliyo chaguliwa imewekwa na Mungu nashangaa kuona eti askofu anashindwa kuhesimu kazi ya Mungu na muumini wa kawaida ataamini nini? Au Biblia ilikosewa ilipo andikwa kuhusu kutii mamlaka? Au vya Kaisari mpe kaisari na vya Mungu mpe Mungu? binafsi naona wanamkosea Mungu kwa sababu madhabahu inatumika kama jukwaa la ki siasa.
 
Sindano za maaskofu kumbe kidogo zinawaingia kumbe,
Maaskofu ongezeni Cc tafadhali
Mbaya zaidi hata kuwakamata hawawezi.
Unamkamata askofu Leo jumamosi. Kesho jumapili unataka uende kanisani kwake akakuongoze katika sala.
Pagumu hapo.
 
Haijawai kutokea Toka tumepata uhuru wa nchi hii,kubwana Kwa wananchi kutoa maoni kama Sasa hivi
 
Watu wanataka kuhalalisha maendeleo Kwa kukanyaga migogongo ya watu hii haikubaliki
 
Back
Top Bottom