Hatimae Polepole awaangukia Maaskofu

Ndio, vyote visivyo na muwakilishi wa kuchaguliwa eneo husika. Tuume maneno tupendavyo ili kuhalalisha utashi wa rais lakini hii kusema eti ufanye siasa mahali ulipochaguliwa tu na siyo nchi nzima hiyo ni sheria ya mfukoni ya rais. Huu ni utashi wake na hakuna sheria ya hivyo.

Kama hufanyi siasa nchi nzima, unapataje wanachama wapya? Sera na ajenda zako zitafahamikaje kwa wananchi ili uwavutie. Katika vitu vinanifanya nisimuunge mkono Magufuli hata kwa hayo machache mazuri ni hii tabia yake ya kutuongoza kama watoto wa chekechea. Ni bora angeweka utaratibu wa kwamba mikutano ya siasa iwe mara moja au mbili kila mwezi. Sio yeye afanye siku yoyote atakayo ba popote yeye na chama chake kisha apangie wengine anavyotaka yeye.
Kuna kifungu cha katiba kinamzuia yy kuzuia jambo flani kwa utashi wake?
 
cf6d90e809c136b95b24f1ee8af72026.jpg

Wanaosema katiba inavunjwa na kama madai yao ni ya mcng katiba imeweka wazi jinsi ya kutatua hilo ttz.Wanasheria hiki kipengele hawakioni?
 
Duuh wanataka kusifiwa tuu kukosolewa hawataki bhna ndugu zetu hawa mmmh Ila tutafika tuu hata kwa mtutu wa bunduki
 
cf6d90e809c136b95b24f1ee8af72026.jpg

Wanaosema katiba inavunjwa na kama madai yao ni ya mcng katiba imeweka wazi jinsi ya kutatua hilo ttz.Wanasheria hiki kipengele hawakioni?

Hivi inakaaje mtu unaapa kuilinda na kuiheshimu katiba kisha unaivunja waziwazi? Binafsi sioni haja ya wanasheria wala majaji kusumbuka eti kusikiliza juu ya kesi za kuvunja katiba kwani ni kupotezeana muda tu. Kwanini wao wanasheria na majaji wasiwaige wenzao wa Kenya ambao hawasubiri kupelekewa bali wanafungua kesi wenyewe! Hawa wa bongo ni waoga na wasioitendea haki taaluma yao na umma wenyewe kwani hawana tofauti na polisi anaywapita wahalifu eti anakwenda kumsubiria mlalamikaji kituoni!
Au wamesusa kuuelimisha umma juu ya umuhimu wa kuitii katiba na sheria za nchi na kuwaachia walimu wkiumiza vichwa jinsi ya kuchopeka somo la katiba na uzalendo kwenye mitaala ya elimu ya msingi na sekondari? Wahurumieni walimu.
 


Baada ya maaskofu kuliamsha dude kuanzia kipindi cha Salam za krismasi na salam za mwaka Mpya, hatimae katibu mwenezi CCM ndugu Humphrey polepole amejitokeza na kuwaomba maaskofu waishauri serikali sirini kwani kwa hali ilivyo sasa ni kama wanaidhalilisha, Rais yuko tayari kupokea ushauri na kuufanyia kazi.

My take
Kila shetani ana mbuyu wake ukimya wa maaskofu na mashehe umetuumiza sana kama taifa na sina shaka wameamuka usingizini baada ya Askofu niwemugizi kuelekezewa bomba la moshi, pia salam zangu za pole ziwafikie Clouds Media

Muda si mrefu hawa maaskofu wataandamana kama wale d.r.c congo
 
Polepole, faragha niijuayo mimi ni ya baba na mama! Hii ya kiungozi ni kutafuta upendeleo na hata rushwa! What if wale mitume Yesu na Mtume Mohammed S. A. W wangesemea faraghani dunia ingepona?
Askofu, padri na mchungaji paaza sauti iwe juu kuishinda ile ya Yohana Mbatizaji na ivuke nyika nyingi hadi Kigoma na kwingineko kuhusu mambo yasiyo na afya kwa nchi yenu na watu wenu! Atakayekwenda kushauri sirini si mshauri bali mnywa chai na msaliti!
 
Itabidi tubadili utaratibu. Kuonya tuonye sirini badala ya hadharani na kufanya mapenzi tufanye hadharani badala ya sirini. Bravo Polepole kwa falsafa hii mupya!
 
Kuna kifungu cha katiba kinamzuia yy kuzuia jambo flani kwa utashi wake?

Sidhani kama anajali vifungu kwani yuko juu ya sheria, hivyo anafanya aonavyo kwani hata akifanya kosa hashitakiwi na wala hatoshitakiwa akitoka madarakani.
 


Baada ya maaskofu kuliamsha dude kuanzia kipindi cha Salam za krismasi na salam za mwaka Mpya, hatimae katibu mwenezi CCM ndugu Humphrey polepole amejitokeza na kuwaomba maaskofu waishauri serikali sirini kwani kwa hali ilivyo sasa ni kama wanaidhalilisha, Rais yuko tayari kupokea ushauri na kuufanyia kazi.

My take
Kila shetani ana mbuyu wake ukimya wa maaskofu na mashehe umetuumiza sana kama taifa na sina shaka wameamuka usingizini baada ya Askofu niwemugizi kuelekezewa bomba la moshi, pia salam zangu za pole ziwafikie Clouds Media

Huyu jamaa ana nafasi gani serikalini?kama kiongozi wa ccm ndo kapata kibali cha kusemea serikali?maaan alie semwa ni dola kwa jinsi wanavyovurunda.
Wadau nisaidieni ni kwa namna gani huyu jamaa kama kiongozi wa chama anaweza isemea serikali pale inapokosolewa
 
Bado waraka wa Katoliki utatoka very soon. Lazima Magufuli anyooshwe kwanza hadharani ili ajijue kuwa yeye sii Mungu wa miungu!
Rais wetu makini. Nyaraka zinatolewa kwa manufaa ya nchi na wala hazijaanza leo. Tangu enzi ya mwalimu
 
Mimi binafsi nilitegemea akili hii ndiyo itawale fikra za wanaccm daima, hakika taifa letu lingekuwa limepiga hatua kubwa kimaendeleo

Lakini nasikitika sana kuona huyu anakuja kusema hili sasa hivi wakati walifahamu vema hawawezi kushindana na viongozi wa kidini.
 
Hivi hyu jamaa kawaje jaman au ndio akili ya binadamu inavotakiwa iwe ukiwa ccm! Maaskofu wamekosoa serikali badala kujibu anaongea pumba kabsa chama ni imani hv hutaacha kumfata askofu eti kisa yupo chadema/ccm!? Zingatia nn anasema. Nimkumbushe akasome kijitabu cha Mwl Nyerere kiitwacho TUJISAHIHISHE
Ova.
 
...Kawangukia Maaskofu. Hii imenikumbusha Kangh'wimbo kasemako:
Akiambiwa aangukie anatoa pesa nyiingiii... Jamani eehe eehee, KUSIKILIZANA ndani ya nyumba ndio KUZURI eeeh... hasira za nini eehee ehee..
 
Back
Top Bottom