Hatima ya ubunge wa Opulukwa leo

fikrapevu sungura

Senior Member
Oct 26, 2011
110
11
Hatima ya ubunge wa Opulukwa leo

By Habari Leo

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tabora leo inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Meatu katika mkoa mpya wa Simiyu yaliyompatia ushindi mgombea wa Chadema, Meshack Opulukwa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na mpigakura Renatus Masanja ilianza kusikilizwa Machi 12, mwaka huu mjini hapa.

Katika kesi hiyo, Masanja anadai kuwa, katika uchaguzi huo, kulikuwa na ukiukwaji wa kanuni, taratibu na maadili ya uchaguzi kutokana na dosari zilizojitokeza katika uchaguzi huo.

Katika hati ya mashitaka, Masanja anadai kiuwa Opulukwa alitumia lugha za kibaguzi dhidi ya mgombea wa CCM, Salum Khamis “Mbuzi”.

Pia anadai kwamba baadhi ya wasimamizi wasaidizi katika vituo vinane, walimpigia kampeni mbunge huyo na kwamba Msimamizi wa Uchaguzi alitangaza matokeo mara mbili kinyume cha taratibu za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Katika kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa na Jaji Fredrick Wambali, upande wa mlalamikaji ulileta mahakamani hapo mashahidi 15 ili kuthibitisha madai yao huku upande wa utetezi ulileta mashahidi tisa.

Kesi hiyo ilivuta hisia za wananchi wananchi wengi waliokuwa wakiisikiliza kutoka katika maeneo mbalimbali ya wilaya za Meatu, Bariadi, Maswa na Shinyanga na leo inatararajiwa kuwa na wasikilizaji wengi zaidi.

Katika kesi hiyo, walalamikiwa ni watatu ambao ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Opulukwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Meatu.

Mlalamikaji alikuwa akiwakilishwa wa Wakili Kamaliza Kayaga huku Mbunge wa Meatu akiwakilishwa na Wakili Godwin Mganyizi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Msimamizi wa Uchaguzi wakiwakilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kanda ya Tabora, Jackson Brashi, Mwanasheria Mwandamizi wa Serikali, Jackline Mrema na Mwanasheria wa Serikali, Abraham Mohamed.
 
Wana JF nipo maswa katika viunga vya mahakama makamanda na wananchi wengi wametoka meatu kuja kumuunga mkono mpiganaji Dr Opulukwa,ila napata mashaka maana mnamo saa 1 na dk 40 ziliingia gari 3 zikiwa zimejaza maaskari chini ya usimamizi wa RCO wa mkoa wa shinyanga - Mr.Kashinje so sielewi hapa maswa tunao askari wa kutosha ya nini tena tuletewe wengine kutoka shy KIFUPI NAANZA KUPATA MASHAKA NA HUKUMU HAKI INAWEZA KUTOTENDEKA,

kumbukeni walalamikaji ambao ni wapambe wa jamaa alomwagwa ni kwamba Mhe. aliwaambia wananchi wasimchague kwani ni mwarabu,hiyo ndo kesi ilivyo na kweli mgombea alikuwa mwarabu ni mambo kama ya Arusha wanaoshikia bango ni wengine tofauti na aliye galagazwa!

Nawasilisha!


SOURCE: Mimi mwenyewe toka eneo la tukio.
 
Lete taarifa!
Kama mambo ni hayo basi ni masikitiko mengine kwa wana cdm!
Watatumia precedence ya kesi ya Lema!
 
Hukumu inatarajiwa kusomwa saa ngapi?
Kama upo eneo la tukio, endelea kutupa updates!
 
Back
Top Bottom