Hatima ya tanzania

ODD

Member
Mar 25, 2010
31
2
ONENI HII. JK NYERERE ,1994.........
Nchi yetu bado changa. Tusione haya kuendeleza taratibu ambazo zinaonekana kuwa zinafaa, na wala kubadili zile ambazo japokuwa huko nyuma zimetufaa, lakini sasa "zimepitwa na wakati." Ndivyo tulivyofanya kuhusu mtumo wa chama kimoja; tusiogope kufanya hivyo kuhusu mageuzi ya kuleta demokrasia zaidi ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Inawezekana kwamba demokrasia peke yake ambayo kwa sasa itaendelea kuwa na maana kwa nchi hii wakati tunasubiri kupata mpinzani mzuri na makini nje ya CCM, ni demokrasia ndani ya CCM. Wanachama wa CCM wana wajibu wa kukitazama upya chama chao na kuona jinsi ya kuongeza demokrasia ndani yake. Wajibu huu si kwa chama chao tu, ni wajibu wa uzalendo kwa manufaa yaTanzania nzima.


Ole wake Tanzania
Tusipoisaidia!
Niwezalo nimefanya:
Kushauri na kuonya.
Nimeonya: Tahadhari!
Nimetoa ushauri:
Nimeshatoka kitini;
Zaidi nifanye nini
Namlilia Jalia
Atumulikie njia;
Tanzania ailinde,
Waovu wasiivunde.
Nasitumsaidie
Yote tusiyamwachie!
Amina, tena Amina!
Amina tena na tena!

 
Wana macho lakini hawaoni wana masikio lakini hawasikii ukikubali kipofu akuongoze wote mtatumbukia katika shimo, amesema niwezalo nimefanya kushauri na kuonya salama pekee ya nchi ni kubadilisha mfumo uliopo hii ndio hatma ya Tanzania kwa sababu tumeshindwa kujisahihisha. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom