Hatari zaidi katika mtandao

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Utafiti uliofanywa kwa mapana kuhusiana na matumizi salama ya mtandao unathibitisha kwamba visa vya ulaghai na uhalifu vimezidi katika mitandao ya kijamii, kama vile Facebook.

Utafiti uliofanywa na kampuni kubwa ya Microsoft, unaonyehsa uhalifu huo umeongezeka mara 12, ikiwa ni pamoja na hali inayojulikana kama mashambulio ya 'phishing', wakati ambapo wahalifu hutumia ujumbe unaoelekea kuwa ni halali, ili kuweza kuwahimiza watumiaji mtandao kutoa maelezo yao ya kibinafsi ambayo kwa kawaida huwa ni ya siri.

Waandishi wa BBC wanaelezea kwamba kutokana na umaarufu wa mitandao ya kijamii, sio ajabu kwamba sasa wahalifu wameanza kuangazia upande huo katika kuwalenga watumizi.
 
Back
Top Bottom