Hata kama ni ndugu zangu wa damu,sipendi tabia hii.

Mawasiliano ni pande mbili,siyo tutafutane wakati wa shida tu.Kuna watu kweli wana tabia hiyo,anakutafuta wakati wa shida tu.
 
Khaa! Kumbe ni lazima kusalimiana!
Mimi nahisi kipato kinakuzuzua na uchoyo uliokujaa ndio hivyo tena unataka kuwatenga nduguzo!
...
Kwani ukiwasalimia wewe kunaubaya gani?
Wewe jifyetue afu yakukute ndio utajua umuhimu wa ndugu!
Hata aibu huna! Hiyo ndio ishu ya kutengana na ndugu zako?
...
Aisee nakuonea huruma sana!

excellent
 
Saidia ndugu wewe acha kulia lia!!!!!

Rizqi nyingine zinapitia tu mikononi mwetu ziende kwa wenyewe au unaona wewe kufanikiwa ni jitihada binafsi????!!!!!

Au we hujawahi kusaidiwa???!!Au huyo demu ndio anakushauri hii maneno????!!!!!!Ukimuoa si atakuambia utumie jina la baba yake,if so!!!!

Maisha kisu cha kukunja ujue hakikati mpaka kikunjuliwe sasa wewe makali ya kisu unataka uyafiche wenzio watakatia nini??????!!!!!!!
 
bora kujinga daraja, kuliko ukuta, we naona ume reverse bora kujenga ukuta kuliko daraja, kama vipi chimba handaki kabisa ili mzinga ya mwesho wa mwezi isikupata
 
Damu ni nzito kuliko maji............USITHUBUTU KUFANYA HUO UPUMBAVU....anza wewe kujenga mahusiano mazuri na wao watafuata....
 
Washkaji wanakua ndugu,ndugu wanabaki watu baki,sio ndugu ukiwa na tatizo ni ndugu wakiwa na dhiki. Usiponiona wakati wa raha na kwenye shida tusionane,kama mwana uwe mwana na si siku nyingne tukimbiane _mwanafa

No matter what happens, ndugu watabakia ndugu na washikaji watabaki hivyo.
Halafu eti sababu ya kutengana na ndg ni kumtegemea wanapokuwa na shida na kukosekana mawasiliano wasipokuwa na shida. Huo ni ubinafsi uliopitiliza. yeye huwa anawatafuta? ndg zetu wengi wana simu lakini hawana hela ya chakula na mahitaji mengine ya lazima. Hivi atanunua vocha ili akupigie kukusalimia tu kweli? Hili pia kwa mbinafsi itaonekana wanajikombakomba kwake b'se ana hela.
Jambo la msingi ni kuambizana ukweli badala ya kuwasusa na kubadili line. Hao washikaji wapo naye kwa sababu ana mkwanja. Ngoja la kumkuta limkute aone hao washikaji watakavyokuwa"washikaji"
Nikionacho mimi…Masikiniakipata…..!
 
Ndugu yako ni ndugu acha hizo. Uncle wangu alkijitenga na ndugu akawafungia vioo mia, akawa yeye na mke wake na watoto wake na ndugu wa mkewe tuu.
Mungu si mwajuma akapata tatizo la figo, kazunguka kila sehemu na pesa anayo. Kila hosp anashauriwa figo ya ndugu, atawaanzia wapi naye aliwatupa. Mkewe na ndugu zake figo hazimfai. Mbona kajifia huku analia ndugu hawajamsaidia figo? Na alikuwa anauwezo wa kununua hata ya mil 100
 
Asalaaam wana jf.kuna kitu kimoja huwa kinanishangaza sana,mimi naishi dar city,nimeajiriwa serikalini,na huku dar,ninaishi mimi kama mimi,sina ndugu jijini hapa zaidi ya jamaa na marafiki,na mpenzi wangu.Back to the topic ni kwamba ndugu zangu hawana kitu kinaitwa kujaliana na kujuliana hali.Yaani wao kunijulia hali ni pale mtu anapokuwa na shida hasa ya mshiko ndio ananipigia simu kama hana shida ya pesa anajeuri yakukaa hata miezi mitatu hajakupigia wala kukutumia ujumbe wowote zaidi yakuomba pesa.Mimi hii tabia yao huwa inanifanya hata nisipokee simu zao coz nimeshajua tabia yao,yaani mtu anakupigia simu mwisho wa mwezi na ukishatatua tatizo lake baasi!itakuwa big deal kuipata simu yake labda mpaka awe na shida,XO Ninafanya maamuzi magumu yakubadiri line wawe pia na wao wananipata kwa msimu.I DNT CARE WETHER I'M RIGHT OR WRONG,I GONNA TRYING LIVING MY LIFE ON MY OWN.

Hao ndg unaowasengenya JF ndiyo waliokulea kwa namna moja au nyingine na ukute ndiyo waliokusomesha na kukufikisha hapo ulipo. Endelea kukumbatia wapenzi na marafiki wa Dar uone kama utakuwa nao siku ya shida. Ndugu ni ndugu hata kama ni masikini kiasi gani. Heshimu utu wao. Imagine leo uvunjike mguu kiasi cha kushindwa kwenda chooni unadhani hao marafiki zako watakubali kukuogesha na kukupeleka uani? Lakini ndg yako anaweza kufanya haya! Usifikiri maisha ni shangwe kila siku, kuna kilio pia. Kwenye shangwe marafiki kibao, kwenye kilio hubaki ndg tu, marafiki wanasepa. Nakupa hii kutokana na uzoefu wa maisha ya mjini!

Afteral wewe ni mfanyakazi wa serikali na mshahara wenyewe wa serikali unajulikana, hii pesa unayotoaga kila mwisho wa mwezi unaipata wapi? Au umeamua kujipigia filimbi kwamba una hela?! I wish ungefuta hii thread JF kwa sababu unawadhalilisha ndg zako na unajidhalilisha mwenyewe.
 
Asalaaam wana jf.kuna kitu kimoja huwa kinanishangaza sana,mimi naishi dar city,nimeajiriwa serikalini,na huku dar,ninaishi mimi kama mimi,sina ndugu jijini hapa zaidi ya jamaa na marafiki,na mpenzi wangu.Back to the topic ni kwamba ndugu zangu hawana kitu kinaitwa kujaliana na kujuliana hali.Yaani wao kunijulia hali ni pale mtu anapokuwa na shida hasa ya mshiko ndio ananipigia simu kama hana shida ya pesa anajeuri yakukaa hata miezi mitatu hajakupigia wala kukutumia ujumbe wowote zaidi yakuomba pesa.Mimi hii tabia yao huwa inanifanya hata nisipokee simu zao coz nimeshajua tabia yao,yaani mtu anakupigia simu mwisho wa mwezi na ukishatatua tatizo lake baasi!itakuwa big deal kuipata simu yake labda mpaka awe na shida,XO Ninafanya maamuzi magumu yakubadiri line wawe pia na wao wananipata kwa msimu.I DNT CARE WETHER I'M RIGHT OR WRONG,I GONNA TRYING LIVING MY LIFE ON MY OWN.

mmmmhhhh kwei kweli ww ni cruel...halafu ukifa utazikwa na nani?
 
si hivyo mkuu..usiwatenge ndgzo unatakiwa nawe ujiangalie km huwa unawatafutaga au?usije kuwa unalalama tu hapa ooh hawanitafuti hadi wapate shida kumbe nawe ndo wale wale...TAFAKARI !
 
Dawa yake ndogo mkuu. Ndugu wengi watakutafuta kwa sababu wana shida. Kwa sababu shida nyingi zinahusiana na hela, fanya hivi:

"waambie tufungue account ya kuweka na kukopa, ili mtu akipata tatizo asikimbilie kukuomba au kujifanya anakukopa hali hatarudisha, badala yake akopeshwe kutoka hiyo account na atarudisha with very little interest ili account iendelee kukua, yeyote atakayekataa kujiunga, basi asikutafute kwa mambo ya hela". Mie nimefanya hivyo and it works, watu kibao baada ya kuwaelezea wameniiga.
Saccos mpaka family level duh, bila shaka tungekuwa tunayasimamia hayo mambo kisayansi inawezekana tungekuwa mbali sana sisi km jamii na hata mmojammoja
 
U don't care!!!! Wewe unamatatizo, subiri siku ukalie kuti kavu utawatafuta hao. Maisha ni kupanda na kushuka
 
Extended family is killing this dude..
Ninachokushauri wala usibadili namba za simu kila kukicha..jaribu kutafuta lugha ya kuwasiliana na nduguzo ili wakuelewe na wasikuone unajisikia...Ni kweli inauma kila wakati kuwa mrija wa kulisha wenzako..ila usikate mrija mara moja..waeleweshe vizuri kuwa kusalimiana na kujuliana hali ni jambo jema pia ..sio lazima kwenye shida ndo tuwasiliane!.. Charity begins at home!..Onyesha kwa vitendo unachotaka utendewe..Ogopa kulaumu wakati na wewe ni sehemu ya Tatizo!..Ni hayo tu bro!
 
Back
Top Bottom