Ni sawa mzazi wa kiume kumtupia lawama mzazi mwenzake wa kike pale mtoto wao anapokuwa na tabia mbaya?

lwambof07

JF-Expert Member
Jul 12, 2016
4,593
5,203
Hellow JF

Nianze kwa kusema kuwa kuna msemo usemao kuzaa huwa sio kazi bali kazi hasa huwa ni kumlea huyo aliyezaliwa kukua katika misingi iliyo bora na awe na tabia njema/nzuri zinazomfurahisha kila mtu anayekutana naye na wahenga husema samaki mkunje angali mbichi.

Mara kadhaa pale mtoto anapokuwa na tabia mbaya lawama hutupiwa mwanamke kuwa ameshindwa kumlea mtoto na je kwa nini wababa huwatupia lawama wamama zaidi?

Kwa upande mwengine unaweza kusema kuwa wazazi wa kiume wako sawa kwa sababu tu ni ule ukweli usiopingika asilimia kubwa ya wababa hutumia muda mchache sana kuwa na watoto wao tofauti na mama nianze kwa kutoa mifano miwili ambayo mimi mwenyewe nimeshuhudia kwa macho yangu.

1.)Nilipata bahati ya kumtembelea ndugu yangu na kukaa pale kwake siku kadhaa pale kuna dada wa kazi lakin pia kuna binti ndugu yake mwanamke ambaye mtoto wake anamuita shangazi sasa nyumba ile mama mwenye nyumba hafanyi kazi kabisa yeye ni kutuma tena humtumia mwanaye mwenye umri wa miaka 9 yupo darasa la nne.

Yule mtoto akirud kutoka shule anafanya homework zake chap kwenye T.V hapo ni mwendo wa katuni hadi saa sita usiku ndipo analala na remote anaficha wale wadada wakibadilisha tu kuweka michezo yao dogo mbio kwa mama wamebadilisha wameweka michezo yao utasikia nyie muwekeeni mtoto katuni basi wale wadada wana sepa zao nje wakiondoka dogo mbio kwa mama utasikia mama wakina dada wamekasirika wameniacha peke yangu utasikia mama mtu nyie msimuache mtoto peke yake sebuleni.

Yule dogo akimaliza kula sahani anaacha hapo hapo watatoa wadada kuna siku walikuja wageni wadada wakaandaa msosi mezani vizuri wadada wanataka kuwakaribisha wageni dogo kawahi mezani funua funua kachukua paja sasa shangazi yake akawa anamkonyeza si usubir kwanza wageni waanze kupakua dogo akalipuka sasa shangazi mimi si nina njaa jamani shangazi mtu ikabidi awe mpole.

Shangazi alinambia yaani huyu mtoto we acha tu usiku tumelala si akaniamsha anataka maji nikaenda mchukulia akanywa yale yaliyobaki akamwagia kitandani ule upande ninaolala sasa mm sikusema kitu nikashuka zangu chini nikalala dogo choropo kwa mama yake mama shangazi amelala chini ameniacha peke yangu kitandani mama mtu huyo lala kitandani na mtoto hakuna cha kuuliza sababu wala nn basi nikalala kibishi hvyo hvyo.

Siku nyingine ametoka zake shule wadada wapo nje wanapika akasalimia zake halafu akasema naona dada wa kazi mdogo na mkubwa wanapika akesepa zake ndani.Yule dogo chochote anachotaka anapewa na mama yake sasa maagizo anampa mwanaye then mtoto anakuja kuwapa wadada mama kasema leo mpike hivi na hivi,mama kasema pale mlangoni kuna nguo zangu na zake mfue na amesema zitakate,mama amesema muamke kumeshakucha mkafanye kazi na mfagie mavi ya mbwa yote.

Akirudi shule kama hamna anachokipenda mezani na mama yake hayupo huyo kwenye simu ya mezani mama leo wapika nisivyopenda anamwambia haya muite dada aje dada akienda haya dada mpikie mtoto vitu anavyotaka.

Ikiwa siku ya kufanya fumigation nyumba nzima anatoa tu maelekezo basi wadada watatoa vitu vyote nje nyumba inakuwa tupu wanapiga dawa wanarudishia vitu mama na mtoto wanarudi usikuu utamsikia mama mtu mimi nina allergy na hizi dawa mtoto sasa leo nyumba imependeza.

Baba mtu hanaga hayo mambo sema shida anatoka asubuhi kurud usiku hana muda wa kutosha pale nyumbani na akiwepo nyumbani yule dogo huwa anakosa amani flan hivi kwa sababu baba yake hataki ujinga na hata akiwepo hamwambii kitu chochote baba yake kwa mama .

2.)Jirani mtaa tunaoishi kuna mdada mmoja amepewa na jamaa mmoja hivi sema alimkuta na mtoto tayari alikuwa na umri wa miaka 3 wakati anamuoa ila sasa mama mtu ametengeneza mazingira dogo amuone jamaa kama baba yake na sasa hivi dogo ana miaka 7 lakini anamuita baba yule jamaa baada ya kuliona hili nikasema kumbe mwanamke ana mchango mkubwa sana kwenye malezi na tabia kwa ujumla maana mama amefanikiwa mtoto wake kumuona jamaa kama baba yake na dogo anamjua baba yake mzazi na anampenda vibaya sema siku hizi hawaonani maana alimtelekeza mtoto so mama mtu amechukia.

Kwa mantiki hiyo mtoto ni mama mama akiwa hayupo vizuri kwenye malezi mtoto ni rahisi sana kupotea.
giphy.gif
giphy.gif
 
Wanaume tujitahidi sana kujua wanetu wanalelewa vipi tukiwa hatupo nyumbani, hata kama uko busy vipi tumia njia zozote kujua maana itakuja kukucost huko mbeleni.

Kingine kikubwa tusiwanyime watoto fimbo, kwenye malezi kuna rewards & punishments, mtoto akifanya kitu kizuri ama akiwa mtekelezaji mzuri wa maelekezo unayompa you have to reward him/her. Akikosea ama kushindwa kufuata yale uliyomuelekeza you have to punish him/her.

Na hakuna kitu kibaya kama kumlea mtoto akiwa na mentality ya akitaka chochote anapata, anakula kile anachotaka yeye, anavaa anachotaka yeye. Hii ni sumu mbaya sana kwa watoto. Mtoto anapaswa ajue ya kwamba kile kilichopo ndicho kinamfaa kwa wakati huo.

Anyway, kwa kifupi jamaa hana mke hapo, maana mke jukumu lake la kwanza ni malezi. Kama hajui malezi hamna kitu hapo, kama mwanamke hapiki, hafui, hajui kulea watoto, huyo ni mke ama kituko? Ina maana hapo ni kama ameajiri hao wadada ndiyo walezi, mke anamtimizia haja za ki-hormone tuu ambazo huenda na zenyewe hawezi
 
wala hujakosea kuna wazazi hawawagusi watoto wao aisee wanaogopa watalia na ukifuatilia zaid asilimia kubwa ni hizi familia zenye dada wa kazi mama anasema yan mm namlipa mshahara halafu mwanangu afanye kazi hapana kwani yeye yupo kwa ajili gani hapa

Jamaa amekosa vyote aisee mke hana pale kabisa yan
 
Yani huyo mtoto wa kisa cha kwanza aje aishi na mimi wiki moja tu ntamfurahisha!
Haha humuwezi yule dogo atakupa stress tu
anamkera shangazi yake sasa shangazi yake naye binadamu basi anamnunia akiwa anampakulia chakula sasa utamsikia shangazi mbona unanipakulia chakula huku umenuna naenda kumwambia mama huyo kwa mama yake mama mtu sasa utamsikia shangazi usimnunie mtoto.

Yaan pale mama mtu kila kitu anamtuma mwanaye aje awaambie boss mtoto hatar sana kuna siku kaamka saa kumi na mbili akaenda chumban kwa wadada nyie amken wakina dada mumeambiwa muamke wakamchunia akaenda kwa chumban kwa mama yake mama nawaamsha wanajifanya hawasikii wamelala basi mama mtu huyo haya haya amkeni kumeshakucha amka.

Yaani ukimfanyia kitu chochote hata kama ni saa nane au saa tisa usiku mbio chumbani kwa mama yake kwenda kusema
 
Yani nakuambia hivi.. hivyo vitabia angeacha tu.. labda sio mimi..!
 
mkuu tutafute pesa, nikijua mwanamke anamlea mwanangu hivi namzingua...mtoto kama wa kiume anamtengeneza awe chokooooooooo. Mwanangu wa kiume(6) alinifuata kulalamika kapigwa na mwenzie nkamwambia Manup na wewe mvizie mtembezee kichapo hata kupiga tena, alienda kumtembezea makonde mpaka akaelewa show..nkamwambia we wa kiume usikubali kuonewa. Home akileta disrespect kwa mtu yeyote anachezea kipigo na hakuna kulalamika kama mwanamke sasa ninyi huyo mtoto mbona mlalamish hivyo ?
 
wazazi sasa hasa mama mtu mwenzako keki yake halafu sasa ni kike
 
mkuu tutafute pesa, nikijua mwanamke anamlea mwanangu hivi namzingua...mtoto kama wa kiume anamtengeneza awe chokooooooooo. Mwanangu wa kiume(6) alinifuata kulalamika kapigwa na mwenzie nkamwambia Manup na wewe mvizie mtembezee kichapo hata kupiga tena, alienda kumtembezea makonde mpaka akaelewa show..nkamwambia we wa kiume usikubali kuonewa. Home akileta disrespect kwa mtu yeyote anachezea kipigo na hakuna kulalamika kama mwanamke sasa ninyi huyo mtoto mbona mlalamish hivyo ?
kweli kabisa pesa ndo kila kitu
 
Back
Top Bottom