Hata ije katiba ipi Bado CCM itaendelea kuwepo madarakani kutokana na Sera na Ajenda zake zinazogusa Maisha ya Watanzania

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,342
9,767
Ndugu zangu huo ndio ukweli na uhalisia wenyewe maana Kuna watu wanasema kuwa uchaguzi wa Tanzania kwa upande wa Urais unatabirika mshindi wake kutokana na katiba iliyopo.

Mimi nasema hawapo sahihi na Kama wapo sahihi Basi hawaelezi sababu ya kutabirika mshindi wa kiti Cha Urais, Ndugu zangu kinachoifanya CCM iendelee kuwepo madarakani Ni kutokana na kuwa na Sera pamoja na ajenda zenye kumgusa mwananchi moja kwa moja.

CCM inabeba na kuweka katika ilani yake mambo na vitu vinavyokuwa vinamlenga mwananchi mnyonge katika maisha yake ya kila siku, utakuta CCM muda wote inazungumzia habari za kuboresha Elimu, Huduma za Afya, usambazaji wa huduma za maji Safi na salama pamoja na umeme Hadi vijijini.

Utaikuta CCM ikizungumzia habari za ajira kwa vijana akina mama na watu wenye ulemavu na namna ya kuwa saidia kujikwamua kiuchumi, utaikuta CCM inazungumzia habari za kuvutia wawekezaji ili kuongeza wigo wa ajira kwa vijana pamoja na Kodi, utaikuta CCM inazungumzia habari za wamama wajawazito kujifungua bure pamoja na wazee kupata huduma za matibabu bure lakini pia utaikuta CCM inazungumzia habari za kufuta Ada za mitihani kwa wanafunzi wa msingi Hadi sekondari ambapo wanufaika Ni watoto wa wanyonge.

Hayo yote na mengine mengi inayokuwa inayazungumzia utaikuta CCM ipo bize kuyatekeleza na kufuatilia utekelezaji wake, Hayo Ni Mambo yanayofanya wananchi waendelee kuiamini na kuipenda CCM, Ni mambo yanayofanya wananchi waende kila uchaguzi kuipa kura CCM, Ni mambo yanayofanya wananachi wailinde, waipiganie,waishangilie na kuitabilia CCM ushindi wa kishindo kila uchaguzi unapokuwa unakaribia.

Nani asiyependa kuona mtoto wake anapata Elimu hata Kama Ni maskini? Nani asiyetaka kuona huduma za Afya Elimu maji umeme na hata Miundombinu ikiboreshwa na kusogezwa karibu yake? Sasa CCM ikiyatekeleza kwanini isipewe nafasi ya kupata ushindi wa kishindo?

Ukweli Ni kuwa Upinzani wa Tanzania hauwezi kuitikisa ccm kwa kuwa hauna Sera Wala ajenda zenye kugusa maisha ya watanzania wanyonge, Hauna mambo yanayoweza mfanya mwananchi hata akatamani kuwapigania, Ni upinzani unaopigania maslahi yao binafsi kupitia ubunge na udiwani au uenyekiti wa mitaa, Ni upinzani njaa, ni upinzani maslahi, Ni upinzani wa tonge kinywani, Ndio maana unaona hauna unachokisimamia Wala kukitetea kinachogusa ugali wa mtanzania mezani.

Upinzani hauna kitu ambacho unachokifanya kinachoweza mfanya hata Bibi au babu kule kijijini akasema Hawa Ni watetezi wao, upinzani Hauna kitu Cha kugusa moyo wa mtanzania, ndio sababu Hakuna anayewasikiliza kwa lolote hata wakilalama vipi, Bado hakuna mbadala wa CCm nchi hii, wanachi Wana Imani na CCM na ndio maana wameendelea kuipa ushindi wa kishindo kila uchaguzi Kama sehemu ya kuhitaji huduma yake.

Kazi ya tume Ni kumtamgaza mshindi, hivyo hata ije tume toka marekani bado upinzani hauwezi kupita, kwa kuwa wapiga kura Wana Imani na CCM na kuwapuuza wapinzani, Ni upinzani ambao hata ukiangalia safu zao za uongozi hauna hata matumaini ya kuonesha kuwa kweli Hawa wanaweza kuwa mbada wa CCm, Ni mkusanyiko tu wa watu wanaojiita viongozi wasio na sifa.

Ikumbukwe pia kuwa mtu hawezi kukuunga mkono au kukupigania katika jua na mvua na katika shida zote wakati hajuwi Wala haoni muelekeo wa kunufaika na chochote kutoka katika Vita hiyo, watanzania hawajaona kinachoweza wafanya wauunge mkono upinzani wa nchi hii, Hawaoni Ni kwanini waiche CCM wakati inatimiza majukumu yake vyema halafu waupe upinzani usio na muelekeo Wala ajenda na Sera zinazogusa maisha yao.

Kazi iendeleee, CCM Ndio Tumaini la wanyonge wa nchi hii katika kuwaletea maendeleo, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka.

Asante
 
IMG_20220914_180443_804.jpg
 
Kumbe ndiyo maana wakati wa uchaguzi hutumia,jeshi Polisi na vyombo vya usalama kuuwa watu, kutia vilema watu na kunajisi dada na mama wa watu?
Kazi ya vyombo vya dola ni kuhakikisha kuwa uchaguzi unatawaliwa na amani bila mamluki kuleta machafuko hapa nchini
 
Back
Top Bottom