Hata CHADEMA mafisadi wapo... Unabisha?

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
4,971
6,520
MAWAZO YANGU:

Mimi nafikiri hakuna uhusiano wowote kati ya Ufisadi (Matumizi ya mali ya umma kwa manufaa binafsi) na Chama cha huyo anayefanya/aliyefanya Ufisadi, tuamini kwamba Ufisadi ni tabia ya mtu mwenyewe, kwa mantiki hiyo basi, fisadi anaweza kutoka CHADEMA, CCM, CUF, CWT (Chama cha Walimu Tanzania) au hata SACCOSS.

Siamini kwamba CCM yote imejaa mafisadi, wapo viongozi kutoka CCM wenye hofu na Mungu na wala si mafisadi, halikadhalika si kweli kwamba CHADEMA wote si mafisadi, miongoni mwao wapo mafisadi pia. Tofauti ninayoiona hapa ni idadi ya mafisadi, huenda CCM ikasemekana ina mafisadi wengi kuliko Vyama vingine.

Naamini pia kwamba ufisadi wa CCM unajidhihirisha zaidi kwasababu ni Chama Tawala, tofauti na ufisadi wa Vyama vingine ambavyo havihusiki na utendaji wa moja kwa moja Serikalini.

Nimemaliza...
 
Problem ni jinsi unavyoshughulikia mafisadi waliomo miongoni mwa jamii yako. hapa ndipo inapokuja tifauti ya CCM na Chadema.
 
6dZ0usAAAAAElFTkSuQmCC
Mpaka hapo utatofautisha maana ya ufisadi
 
Hukawii kumwita babaako pia 'fisadi' kisa anaongoza familia..ili upate sababu za kuutetea ufisadi wa ccm
 
Hapo umenena vyema ila umeshindwa kutambuwa kwa nini CCM kinatajwa chama cha mafisadi, ni pale chama kinashiriki kitika ufisadi huo au kiongozi anafanya ufisadi kisha chama kina mlinda hapo ndio tunasema ccm ni chama cha mafisadi.
 
MAWAZO YANGU:

Mimi nafikiri hakuna uhusiano wowote kati ya Ufisadi (Matumizi ya mali ya umma kwa manufaa binafsi) na Chama cha huyo anayefanya/aliyefanya Ufisadi, tuamini kwamba Ufisadi ni tabia ya mtu mwenyewe, kwa mantiki hiyo basi, fisadi anaweza kutoka CHADEMA, CCM, CUF, CWT (Chama cha Walimu Tanzania) au hata SACCOSS.

Siamini kwamba CCM yote imejaa mafisadi, wapo viongozi kutoka CCM wenye hofu na Mungu na wala si mafisadi, halikadhalika si kweli kwamba CHADEMA wote si mafisadi, miongoni mwao wapo mafisadi pia. Tofauti ninayoiona hapa ni idadi ya mafisadi, huenda CCM ikasemekana ina mafisadi wengi kuliko Vyama vingine.

Naamini pia kwamba ufisadi wa CCM unajidhihirisha zaidi kwasababu ni Chama Tawala, tofauti na ufisadi wa Vyama vingine ambavyo havihusiki na utendaji wa moja kwa moja Serikalini.

Nimemaliza...

hayo ndio maneno yenu ya kinapenape kwamba ccm ni nzuri lakini viongozi wake ndio wabaya au wanachama wake ndio wabaya na mnayasema hayo kwa hila ili watu waichague ccm, hayo maneno yenu ya hila lazima yale kwenu na yanaijenga chadema. hila zenu ni pembe la ngombe azifichiki tena,kila siku nawaambieni haya hamtaki kujirekebisha muache hila, kweli sikio la kufa alisikii dawa
 
Rejea kwanza nini maana ya ufisadi, halafu uje kujimwaga jamvini. Hicho ulichoeleza hakuna cha kuchangia na uzi hauna mvuto.
 
MAWAZO YANGU:

Mimi nafikiri hakuna uhusiano wowote kati ya Ufisadi (Matumizi ya mali ya umma kwa manufaa binafsi) na Chama cha huyo anayefanya/aliyefanya Ufisadi, tuamini kwamba Ufisadi ni tabia ya mtu mwenyewe, kwa mantiki hiyo basi, fisadi anaweza kutoka CHADEMA, CCM, CUF, CWT (Chama cha Walimu Tanzania) au hata SACCOSS.

Siamini kwamba CCM yote imejaa mafisadi, wapo viongozi kutoka CCM wenye hofu na Mungu na wala si mafisadi, halikadhalika si kweli kwamba CHADEMA wote si mafisadi, miongoni mwao wapo mafisadi pia. Tofauti ninayoiona hapa ni idadi ya mafisadi, huenda CCM ikasemekana ina mafisadi wengi kuliko Vyama vingine.

Naamini pia kwamba ufisadi wa CCM unajidhihirisha zaidi kwasababu ni Chama Tawala, tofauti na ufisadi wa Vyama vingine ambavyo havihusiki na utendaji wa moja kwa moja Serikalini.

Nimemaliza...

Yeah Kila MTU ni MLAFI lakini inategemea TABIA ya ULAFI... Unachota kila kitu haubakizi kwa wananchi; Au Unachota kidogo unawabakizia Wananchi angalau Chai ya Asubuhi...

Angalia Rais Nyerere Familia yake Jinsi inavyosota na Rais Kikwete Familia yake Jinsi inavyopepetua... Wote Walitoka kwenye FAMILIA za MACHIFU... Nani hapo anachota zaidi ya MWINGINE??
?
 
Bila shaka nawe ni mmojawapo mlopata msamaha wa matokeo, aya kazana lakin jua unatoa taulo na watu tnakuona
 
Back
Top Bottom