Harusi: Tarumbeta, honi na upambe wa magari umekuwa kero mijini

Exaud J. Makyao

JF-Expert Member
Nov 30, 2008
1,518
22
Siku hizi imekuwa fashion maharusi kuzunguka mabarabarani ili kujionyisha kwa umma baada ya harusi kufungwa.
Mizunguko hii inamaana gani lakini?
Mara nyingi husababisha msongamano wa magari barabarani.
 
hata kama wakikukera mi nahisi pamoja na kujionyesha huwa kuna neno kwenye sheria ya ndoa kuwa *marriage need to be public* labda wanajifunika ili watu wajue ameolewa au ameoa tena mbaya zaidi ni ile wanapokaa juu ya magari noma kabisa.
 
jamani hizi harusi zinakera mno, hasa wenyeji wa arusha mtakubaliana na mimi, siku ya jumamosi kuna kua na foleni za hatari kisa harusi.. wanachukua barabara nzima, barabara zetu zenyewe finyu.. wengi wao ni kujionyesha tu, maana sio harusi tu mpaka ubarikio na vipaimara lazima wapite na matarumbeta mji mzima..
 
Ingependeza pia wanapotalikiana basi wafananye hivyo hivyo kujionyesha kuwa sasa tuameachana mitaani, na kwenye mabara bara!! Matarumbeta, na kila shamra shamra maana divorces need to be public as well

Masa
 
Mbona mmechelewa sana hii ni tangu enzi za mababu zetu tatizo si harusi bali mfumuko wa ulwetaji wa magari mabovu toka nje mbona huko nyuma zilikuwepo hakukuwa na msongamano waulizeni bandari!!!!wala msiwaguse wanandoa kama kuachana wakipenda wanaweza fnya hivyo
 
jamani hizi harusi zinakera mno, hasa wenyeji wa arusha mtakubaliana na mimi, siku ya jumamosi kuna kua na foleni za hatari kisa harusi.. wanachukua barabara nzima, barabara zetu zenyewe finyu.. wengi wao ni kujionyesha tu, maana sio harusi tu mpaka ubarikio na vipaimara lazima wapite na matarumbeta mji mzima..

NYASHI
Ni kweli.
 
Ingependeza pia wanapotalikiana basi wafananye hivyo hivyo kujionyesha kuwa sasa tuameachana mitaani, na kwenye mabara bara!! Matarumbeta, na kila shamra shamra maana divorces need to be public as well

Masa

MASA,
Haya ya kutalikiana, ni mawazo mapya na changamoto muhimu.
 
Siku hizi imekuwa fashion maharusi kuzunguka mabarabarani ili kujionyisha kwa umma baada ya harusi kufungwa.
Mizunguko hii inamaana gani lakini?
Mara nyingi husababisha msongamano wa magari barabarani.

Naona umeuliza swali na kujijibu mwenyewe. Shukrani kwa kutushirikisha mawazo yako!
 
Mimi sioni tatizo. Kwa wale wenye imani (dini) kama mimi, hii ni sikukuu ya kubwa katika maisha ya binadamu. Ni siku ambayo unakuwa umeweka agano mbele za Mungu kuwa na mwenzi wako mpaka kifo kitakapowatengenisha. Kwa kifupi ni siku kuu! Hapa kila mtu anapaswa kusheherekea kwa kila style. Ukiamua kupita jiji zima na matarumbeta, au ukiamua kwenda beach (kipindi kabla hazijafungwa) ni katika shamrashamra za kusheherekea. The public has to know bwana. Kama hukubahatika kufanya hivyo pole sana.
 
Noise pollution. Huu ni ushamba mkubwa na unatakiwa kupigwa vita mpaka ukomeshwe. Wanasumbuliwa watu wanaotakiwa kupumzika mchana baada ya kufanya kazi shift za usiku, wagonjwa mahospitalini wamelala mchana kwa vile hawakuweza kulala usiku kwa sababu ya maumivu n.k. Kwa nini matarumbeta na honi zisipigwe nyumbani kwa bwana na bibi harusi? Mambo haya yapo hapa kwetu tu, nchi nyingi zimepiga marufuku kelele kama hizi.
 
Ni kweli zamani kijijini ilikuwa ni kitu cha kawaida na haikuwa kero kwani everybody was invited! Lakini in urban settings hii imepitwa na wakati! But these are the growing pains of developing countries!
 
Hivi, kinachokukera hasa nini? Si uendelee tu na shughuli zako. Hata kama wakiacha ndio barabara zitapanuka?
 
Waacheni wajitanue. Inawakera "in moral terms" lakini hamna hoja ya msingi kupinga hizo sherehe.
 
Ingependeza pia wanapotalikiana basi wafananye hivyo hivyo kujionyesha kuwa sasa tuameachana mitaani, na kwenye mabara bara!! Matarumbeta, na kila shamra shamra maana divorces need to be public as well

Masa

hahahahahahahahahahaahahahah jamani msinivunje mbavu mie sasa talaka nayo wafanye maonyesho wakati ni kitendo cha huzuni kwikwi kwi kwi
 
acheni watu wale maisha bwana, hata kufurahia mnataka kuwawekea mipaka? watu wapo wa aina nyingi, wengine bila kujionyesha, basi siku haijawa nzuri, wengine hawapendi kujionyesha. Inapotokea kujionyesha kwa wengine, au kujisifu inakuwa kero, tufanyeje, ndio tofauti tulizo nazo hizo, ndio kinachofanya dunia ipendeze, tungekuwa wote wa aina moja, hobby hizohizo, kila kitu, dunia ingeboa sana. kuna wengine wanapenda kuishi bila kufa, wakidhani watafaidi sana, hasa mafisadi, sisi wengine hakaaa, tujiondokee tu Mungu akipenda, tutaboreka bureee!!
 
Siku hizi imekuwa fashion maharusi kuzunguka mabarabarani ili kujionyisha kwa umma baada ya harusi kufungwa.
Mizunguko hii inamaana gani lakini?
Mara nyingi husababisha msongamano wa magari barabarani.

Barabara ndio finyu nadhani, na wala si harusi, mfano Dar asubuhi kingia mjini ama jioni kutoka mjini barabara husongamana. Jee hii misongamano husababishwa na harusi?. Nadhani mjadala hapa ni vipi Serikali itajipanga kujaribu kuondoa misongamano katika miji yetu, na wawe na mipango endelevu sio ile ya zimamoto.
 
hata kama wakikukera mi nahisi pamoja na kujionyesha huwa kuna neno kwenye sheria ya ndoa kuwa *marriage need to be public* labda wanajifunika ili watu wajue ameolewa au ameoa tena mbaya zaidi ni ile wanapokaa juu ya magari noma kabisa.

Ehe juu ya magari tena! Kama umewaalika watu kwenye harusi yako inamaanisha hao ndiyo uliotaka uwatangazie au wawe ndiyo shuhuda mbele ya mungu! sasa ukipita mitaani ukijidani ndiyo tujueje? Siku ya harusi unatakiwa uwe ndiyo malikia/mfalme ukae uhudumiwe watu wakupongeze pale ulipoandaliwa sio kupita ukizunguka huku na huku (unatafuta nini tena jamani?) Huu ni utumiaji mbaya wa pesa mlizochangiwa kwa mafuta na usumbufu wa wale waliowafuata kusherehekea - Mnawachosha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kay
 
Hii ni changamoto.
 
...na michango ya lazima waache,yaani mtu akioa basi anaona kama haki yake achangiwe na anaweka mpaka kiwango anachotaka na anataka watu muende vikao vyote na usipoenda ni tabu tupu,hiyo miharusi tafadhari isiwe kero kwa wengine ....mambo ya ajabu kabisa!
 
Back
Top Bottom