HARMONIZE vs MARIOO

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,305
Kwa kawaida tushazoea kuwa kwa masilahi mapana na usalama wa Verse yako usijaribu kumtanguliza "Marioo" katika ngoma.

Pia wewe kama msanii usikubali kabisa "Harmonize" akikutanguliza katika ngoma ni lazima yawe mauajii humo ndani.

Mjadala ulianzia katika "Naogopa" maneno yalikuwa mengi sana na wengi wetu tulitamani tupate ngoma nyingine itakayotuonesha M-babe kati yao {Melodies plus uandishi}.

AWAY imekuja na majibu tosha kabisa na nilichopenda kila mtu kakaa katika nafasi yake kwa maana "Marioo-verse ya kwanza}, "Harmonize-verse ya pili}.

Binafsi niseme tuu angalau hata ndani ya "Naogopa" Marioo alijaribu kushambulia, ila humu ndio kakimbizwa mbaya.

Kama Marioo ataendeleza ubishi basi nitatamani wajipe muda na wakae mezani wajadili kuhusu ujio wa "EP ama Album kabisa}

Inafaida katika muziki wao maana Mashabiki macho na masikio yapo kwao kila wakisikia ujio wa kazi toka kwao.

Olo ini olo Mpaka sasa "Harmonize- 2.....Marioo-0}.....tunahitaji ngoma nyingine huenda Marioo akasawazisha

"Marioo & Harmonize~Away"🎶🔥

Credit - DullahTheking2
 
Back
Top Bottom