Harakati za jumuia ya uamsho ,mapokezi kwa wananchi na mbio za kuuvunja muungano

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Nimebahatika kuhudhuria mikutano ya Jumuia ya kiislam ya Uamsho inayofanyika kwa kasi visiwani Zanzibar
1)Mkutano uliofanyika Makunduchi kusini Unguja. Mwitikio ulikuwa mkubwa . umati wa watu walifurika.Magari kutoka Mjini yalikuwa mengi sana
2)Mkutano wa Uwanja wa Lumumba hivi Karibuni. Huu naufananisha na mkutano wa vyamavya siasa. yaani Umati ulikuwa mubwa. mwitikio ulikuwa mkubwa sana. uwanja huu unaweza kuufananisha na uwanja wa Jangwani Dar.Uwanja huo ulijaa mpaka wengine kukosa nafasi
3)Viwanja vya sebleni jumamosi iliopita. mwitikio ulikuwa Mkubwa sana
WANACHOAMBIA WAZANZIBAR
1)Zanzibar inanyonywa na wazanzibar wajitoe kwa hali na mali kuilinda nchi yao.
2)Zanzibar ijitoe katika Muungano
3)Wanamlaumu Mwalimu Nyerere kwa kuimeza Zanzibar

img_3129.jpg

baadhi ya Umati wa wasikilizji
 
sawa jitoeni nimechoka na haya malalamiko kila kukicha mie binafsi na taka TANGANYIKA nchi yangu MUUNGANO hauna faida yeyote .. kwangu ....
MIMI BINAFSI NI RAIA WA KWANZA KUPINGA MUUNGANO.. IKIPITISHWA KURA YA KUUVUNJA SIKU HIYO NTAFANYA SHEREHE maana kila siku ooh wazanzibari wanaonewa mara hoo wabara wanapendeleana bana hata ndoa takatifu zinavunjwa
UVUNJWE MUUNGANO TUJIPANGEEE
 
Kuvunja muungano ni Rahisi kuliko hizi harakati za Mombassa republican Council za hapa Kenya.
Zanzibar ni Nchi kama Tanganyika waacheni waende jamani kama wanashawishiwa na ndugu zao OMAN/MUSCAT let them Go.
 
Bara inaonekana kama ni mkoloni wa wazanzibari, kwanini wasipewe uhuru ili waweze kuendelea? Misuguano hii inarudiasha nyuma maendeleo
 
Pliz bara wachieni wazanzibar wajitawale nasi tubaki kwetu haya malumbano hadi lini??
 
Hongera sana WaZnz kwa kuona mbaaaaaali sana kwa mustakabali wa nchi yenu.
 
Bara inaonekana kama ni mkoloni wa wazanzibari, kwanini wasipewe uhuru ili waweze kuendelea? Misuguano hii inarudiasha nyuma maendeleo
yea! hata mimi nimekuwa na hisia hizo! Tanganyika inaikoloni Zenj na wa wazenj wameshtukia hiyo. ndiomaana waTanganyika wengi wanalazimisha muungano wa nchi moja.
 
Hayo ni mawazo yao au wanatumiwa ....
Mkuu amini usiamini hayo ndiyo mawazo ya wazanzibar na watanganyika wengi kama siyo wote. Kuendelea kuzibia masikio suala la muungano kutatufikisha pabaya.
 
Kweli bwana, ukiangalai bunge akisimama mzenji tu unajiuliza atakuwa analalamikia nini sasa. you can predict nini mzenji atalalamikia kuhusu hoja iliyopo. nasi pia tumeuchoka muungano kwa kweli. tuuvunje tukate umeme wetu maana wanatupunguzia megawati tu.
Pliz bara wachieni wazanzibar wajitawale nasi tubaki kwetu haya malumbano hadi lini??
 
kaka sio watanganyika wenye kulazimisha muungano ni CCM na serikali yake.kuna watu bado wana fikra za kumrudisha sultan aje atawale Zanzibar wakiamini watapata maendeleo kama Oman.Wachiwe waende zao jamani kwa amani.
 
Sisi tuna akili na tunafikiria kabla ya kutenda

Mkuu tafuta hoja nyengine, sio ya kuwa sisi tuna akili. Kwani Wazanzibari hawana hizo akili? Acheni woga Wadanganyika. Daini Tanganyika yenu.
 
Sisi tuna akili na tunafikiria kabla ya kutenda

Mkuu tafuta hoja nyengine, sio ya kuwa sisi tuna akili. Kwani Wazanzibari hawana hizo akili? Acheni woga Wadanganyika. Daini Tanganyika yenu, siyo kukaa kimya tu.
 
Leo munamulaumu Mwl na si Karume aliyemwanbia Mwl tuungane kama nchi moja yaani hapo ni kumezana kabisa ila Mwl akapooza na kuacha Zanzibar katika ramani na Tanganyika kufutika kwenye ramani na matokeo yake tunajua jinsi watanaganyika wanavyolalamika hadi leo. kama shukurani ni hizo na kwa kuwa Afrika ya mashariki sasa ipo bora ufe kila mtu ababe mzigo wake. Tunahitaji Tanganyika yetu ama serikali tatu.
 
Wewe ambaye ni graduate wa chuo kikuu una nn cha maana? Au una mchango gani kwa jamii yetu? Afadhali yao wanathubutu japo kusema kuliko wewe unayesemea mtungini. Shame on you!

kwikwiw kwiwkwiii wanafiki wakubwa wale wanapiga kelele hakuna anayewasikiliza, mshukuruni sana Kikwete anawachekea si mnakumbuka enzi za Mkapa mlivyokua mnachezea virungu?
 
Back
Top Bottom