Happy birthday my "birthday buddy/twin" Tanganyika

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
Pamoja na kila jina baya ninaloweza kutupiwa - mkimbizi, msaliti... you name it - kamwe sijawahi kujiona mmoja wa watu wasio na bahati ku-shea siku ya kuzaliwa na taifa langu la Tanganyika. Unfortunately hakuna neno sahihi kumaanisha "watu wawili waliozaliwa tarehe moja." Maneno ya karibu ni "birthday twins" japo si rasmi na "Irish twins" ambayo hasa ni kwa watu waliozaliwa tarehe moja lakini mwaka mmoja apart. Pia katika urban dictionary kuna "birthday buddy."

That aside, ku-shea birthday na Tanganyika hunifanya nilazimike kufanya tafakuri kwa sababu kama mwana wa Tanganyika ni wajibu kuitumia siku hii kuangalia tulikotoka, tulipo na tuendako.

Ni rahisi sana kuiongelea vibaya Tanganyika, na pengine hata kutamani mkoloni arudi. Ni rahisi kwa sababu Watanganyika wengi hawajawahi kuishi kwenye ukoloni. Ni rahisi pia kwa sababu Watanganyika wengi hawajawahi kutoka nje ya mipaka ya nchi yao na kupata fleva ya huwa chini ya himaya ya mtu asiyetoka nchi moja na wewe.

Lakini ni rahisi pia kwa sababu watawala wetu wanawapa wananchi kila sababu ya kuichukia Tanganyika yao.

Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa hawa watawala majahili wanatokana na sisi wenyewe. Sie ni mahiri sana wa kuwanyooshea wenzetu vidole. Ni wazuri sana katika kulaumu. Na baadhi ya wenzetu ni mabingwa wa matusi. Ongea lolote lile kinyume na imani zao, basi ni halali kwao kukutukana.

Hawa ni madikteka kama Magufuli. Tofauti pekee yeye ni Rais na wao ni wababaishaji mitandaoni/mtaani. Lakini wote ni wakandamizaji wa haki za kikatiba za wenzao kutoa maoni yao.

Ni muhimu katika maadhimisho haya ya miaka 57 ya uhuru wa Tanganyika yetu tukajaribu kuangalia nafasi yetu sisi kama Watanganyika, katika (a) kuchangia matatizo yanayoigubika Tanganyika hivi sasa (b) kujadiliana kuhusu way forward.

Japo pengine hili si la muhimu, lakini naamini kwamba kuna breakdown ya communication katika ngazi mbalimbali. Na hili linaanzia katika ngazi ya familia. Mengi ya tunayoyaona mtaani muda huu ni matokeo ya socialisation. Na moja ya vinavyoathiri socialisation ni poor - or no - communication.

Mtoto anayekua akiona baba anamdhulumu mtu haki yake, hata kama dhuluma hiyo inafanyika tu ili familia husika ipate mlo - anaweza kuamini kuwa dhuluma is acceptable in order to make ends meet.

Kuna huge crisis of morality kwenye familia zetu. Haya ya Magufuli kwa Watanganyika yanatokea kila kukicha kwa waume kwa wake zao, viranja mashuleni kwa wanafunzi wa kawaida, viongozi wa dini kwa waumini wao.... na kwa vile "haba na haba hujaza kibaba" hatimaye tunajikuta tuna tatizo kubwa katika ngazi ya taifa.

Chanzo kikuu cha matatizo yetu kama taifa kipo katika ngazi ya familia. Tunaposherehesha maovu katika ngazi hiyo tusitarajie uadilifu katika ngazi ya taifa.

Angalia suala la uzinzi katika level ya familia. Tunachukulia ni suala la kawaida tu. Na ndio maana hata tukisikia kiongozi flani anasaliti ndoa yake, haitusumbui. Tunachozembea hapa ni ukweli kwamba mtu asiye na maadili kwenye ndoa yake hawezi kuwa na maadili kwa taifa. Kwamba mtu anayediriki kum-cheat mkewe hashindwi kuwa-cheat wananchi anaowaongoza.

Lakini ukosefu wa maadili in the form of kuchepuka sio tatizo linalowahusu watawala wetu pekee bali linaanzia huko mtaani kwetu kutoka ngazi ya familia.

Tukipanua uwanja, hata hilo genge kubwa la wanasiasa matapeli ni matokeo ya sie wenyewe. Hawa watu sio kama walishuka kutoka mbinguni wakaingia madarakani. Hapana. Tuliishi nao mtaani. Tulipuuzia mapungufu yao walipokuwa "hawana kitu" lakini sasa twatarajia wawe waadilifu baada ya kuwakabidhi dhamana ya kutuongoza.

Wanaomjua Magufuli watakwambia hakuna geni katika urais wake ambalo hakufanya alipokuwa Waziri. Je Magufuli amewezaje kuwa Rais licha ya hizo kasoro ambazo huenda zilipaswa kuwafanya waliomuunga mkono kubaini mapema kuwa "huyu akiwa Rais basi tumekwisha."

Ni mara ngapi JK aliwashiana moto na Magufuli lakini yakaisha kimyakimya? Leo hii, JK ambaye laiti angechukua hatua stahili dhidi ya "wazri wake mtukutu" isingepelekea mtukutu huyo kuwa Rais, naye ni shujaa pia. JK huyu huyu aliyedhihakiwa kwa kila namna.

Lakini JK huyo nae alikuwa product ya Mkapa. Kama ambavyo Mkapa alikuwa product ya Mwinyi/Nyerere, na Mwinyi product ya Nyerere. By "product" namaanisha mtu aliyelelewa katika mfumo/awamu husika.

To make matters even worse, tatizo la communication katika ngazi ya familia sasa limehamia kwenye ngazi ya kitaifa. Na kwa kiasi kikubwa linachangiwa na udikteta. Intaneti haina ubaguzi, inatoa fursa sawa kwa watu wenye akili na vichwa panzi. Na kwa bahati mbaya, Intaneti pia hukutanisha makundi haya mawili takriban kila sehemu.

Tumefika mahala kwamba aidha uwe CCM au uwe mpinzani. Na hata ukiwa upande mmoja kati ya hizo haimaanishi upo salama. Wapinzani wanachukia Wana-CCM pengine justifiably, kama ambavyo wana CCM wanavyowachukia wapinzani wakiongozwa na "mkuu wa Kamati ya roho mbaya."

It's becoming virtually impossible kutoelemea upande wowote. Mwaka 2010 nilikuwa mmoja wa watu waliofanya jitihada kubwa kumkampenia mgombea urais kwa tiketi ya Chadema Dokta Slaa (wengi wenu hamkuwepo mtandaoni zama hizo). Watu wa CCM wakataka kunimeza nikiwa hai. Nikaitwa kila jina. Nikatukanwa kila tusi.

Mwaka 2015 nikaamua kumuunga mkono mgombea wa CCM kwa sababu sikuafiki uamuzi wa Chadema kumpokea Lowassa. Kama walivyonitenda makada wa CCM 2010 ndivyo walivyonitenda wanamabadiriko mwaka 2015. Nikaitwa kila jina. Nikatukanwa kila tusi.

Na kuamua kujiweka kando na kelele za siasa kumepelekea ndoa ya matusi kutoka kila upande. Nikikosoa Chadema, mvua ya matusi. Nikikosoa CCM, mvua ya matusi. However, kuna funzo la muhimu hapa. Kwamba tofauti kati ya wafuasi wa CCM na wa Chadema/Upinzani ni ndogo sana. Waunge mkono hata kama hawako sahihi, basi wewe mzalendo haswa. Wakosoe, halali yao kukutukana. Wa CCM nao hivyohivyo.

Unfortunately, matusi na lugha mbovu sio tu zinakwamisha mijadala ya muhimu kuhusu mustakabali wa Tanganyika yetu bali pia yanatuondoa kwenye reli ya kuangalia mambo mengine muhimu kama kinachojiri nje ya Tanganyika yetu na ambacho kwa hakika kitakuwa na athari kwetu huko mbeleni.

Dunia inabadilika kwa kasi. Vuguvugu la utaifa linazidi kushika kasi, huku baadhi wakihisi ndio Trump Effect, japo kimsingi Trump ni matokeo tu ya failure ya elite class ku-deliver the goods kwa watawaliwa. Kuibuka kwa likes of Trump ni matokeo ya wananchi wa kaiwada "kuipa middle finger salute" elite class (pardon my French).

Miaka si mingi ijayo, nchi zenye huruma kwetu zinakuwa chini ya tawala zisizotaka kusikia lolote kuhusu sie. Ukiangalia kuibuka kwa far-right politics katika nchi rafiki kama Sweden basi unaweza kwa yamkini kuhisi huko mbele kutakuwaje.

Leo hii ni vigumu kwa Trump kumkemea Magufuli kwa sababu US sasa hivi haina moral authority kuwa "polisi wa dunia." Not after Trump kuendelea kumkingia kifua gaidi MbS, kwa sababu za kibiashara zaidi kuliko common sense.

Unapoona Rais wa Marekani anaitangaza media kuwa adui wa watu na kusherehesha siasa za kibaguzi sambamba na kuwa muumini wa fake news (ilimsaidia kuingia madarakani anyway) basi mustakabali ni tete.

Kuna eneo jingine ambalo pengine kwetu si la muhimu sana lakini kwa hakika litatufanya tuwe kwenye "kisiwa cha mbumbumbu." Ni maendeleo ya sayansi na teknolojia. Vitu kama Artificial intelligence, Machine Learning, Blockchain, nk vinaonekana kama anasa tu kwetu ilhali huko tuendako ndio vitakavyokuwa among basic needs. Je tuna wasaa wa kujihangaisha kuhusu masuala kama haya?

Nihitimishe gazeti hili kwa kusihi sana tuboreshe mawasiliano yetu, tupingane hoja bila kupigana, na kubwa zaidi tuunganishe nguvu zetu ili tuweze kuikwamua Tanganyika yetu.

Nirudie tena kusema happy birthday Tanganyika, my birthday buddy/twin.
 
Nimeiona busara ikimea katika andiko lako hili. Tunalo tatizo kubwa katika jamii yetu ;wengi wetu ni madikteta haswa ;tunakosa tu madaraka ya kuonesha udikteta wetu ; hata we we mwandishi una tatizo hili pia.
 
Tazama sasa watu walivyo kususa yaani uzi una zaidi ya saa mzima lkn wachangiaji 6? Jirekebishe mshikaji wangu
 
Happy Birthday. Good food for thought, and I quote, "

Chanzo kikuu cha matatizo yetu kama taifa kipo katika ngazi ya familia. Tunaposherehesha maovu katika ngazi hiyo tusitarajie uadilifu katika ngazi ya taifa.
Angalia suala la uzinzi katika level ya familia. Tunachukulia ni suala la kawaida tu. Na ndio maana hata tukisikia kiongozi flani anasaliti ndoa yake, haitusumbui. Tunachozembea hapa ni ukweli kwamba mtu asiye na maadili kwenye ndoa yake hawezi kuwa na maadili kwa taifa. Kwamba mtu anayediriki kum-cheat mkewe hashindwi kuwa-cheat wananchi anaowaongoza.
Lakini ukosefu wa maadili in the form of kuchepuka sio tatizo linalowahusu watawala wetu pekee bali linaanzia huko mtaani kwetu kutoka ngazi ya familia."

Relevant!
 
Watumishi fanyeni hujuma indirect dhidi ya serikali hii onevu kwenu ni miaka 3 hakuna ongezeko la mishahara na maslahi yenu yanazidi kukandamizwa.
 
Back
Top Bottom