Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 35 leo Mei 29, 2023.
Ufungaji wa kamera za Ulinzi
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Hamad Masauni amesema Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi limekamilisha mradi wa ujenzi wa mji salama utakaotumia kamera zenye mfumo wa utambuzi wa Sura.
Katika awamu ya kwanza, kamera hizo zitafungwa Katika mkoa wa Arusha, Dar es salaam na Dodoma. Hii ni sehemu ya kuongeza nguvu katika kubaini na kuzuia vitendo vya kihalifu nchini.
Hali ya Magereza Nchini
Akizungumzia hali ya magereza nchini, Waziri Masauni amesema hadi Mei 2023, jumla ya wahalifu 30,901 walikuwepo kwenye magereza yote nchini ambapo wafungwa wapo 18,887 na mahabusu 12,014.
Pia, Utekelezaji wa adhabu Mbadala umekuwa unafanyika ambapo wafungwa wenye kifungo cha nje wapo 780 na waliohukumiwa kutumika vifungo vyao kwa kutoa huduma kwa jamii wakiwa 3,719.
Matukio 14,184 ya ukatili wa kijinsia yameripotiwa Polisi
Kutoka Julai 2022 hadi Mei 2023, jumla ya mashauri 14,184 ya matukio ya ukatili wa kijinsia na Watoto yalitolewa taarifa katika vituo va Polisi ikilinganishwa na matukio 12,642 yaliyotokea kipindi kama hicho mwaka uliopita.
Matukio ya Ajali za Barabani ni 1,283
Hali ya usalama barabarani imeimarika kutokana na Jeshi la Polisi kusimamia Sheria za Usalama Barabarani.
Amesema “Katika kipindi cha Julai 22, 2022 hadi Mei 23, 2023 matukio ya ajali yalikuwa 1,283 tofauti na mwaka mmoja uliopita ambapo yalikuwa 1,731, hivyo yamepungua kwa 25.9% sababu ikiwa ni kuimarika kwa usimamizi wa Sheria, kufanyika kwa oparesheni maalum Nchi nzima na elimu kutolewa kwa makundi yote.”
Waziri Masauni: Magereza yote nchini yana wahalifu 30,901
Akizungumzia hali ya magereza Nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema hadi Mei 2023, jumla ya Wahalifu 30,901 walikuwepo kwenye magereza yote, kati yao wafungwa ni 18,887 na mahabusu ni 12,044.
Amesema utekelezaji wa adhabu mbadala umekuwa unafanyika ambapo wafungwa wenye kifungo cha nje wapo 780 na waliohukumiwa kutoa huduma kwa jamii ni 3,719, ameeleza kipindi kama hiki kwa Mwaka 2021/22 kulikuwa na Wahalifu 32,671 gerezani