Halotel waache uhuni wa kuwaibia wateja

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
12,917
15,348
Wasalam wadau wote.

Nachukua fursa hii kuitahadharisha kampuni ya simu za mikononi ya Halotel kuacha kabisa hii tabia ya hovyo wanayofanya ya kuwaibia wateja wake.

Kampuni hii ina tabia moja ya hovyo sana kwamba wakiona una GB nyingi kwenye simu yako na unataka kuongeza tena salio kwa kuongeza GB zingine ili ufanye Top Up kabla muda haujaisha basi hawakubali.

Wanachofanya hapo ni kukuruhusu uingize salio jipya lakini pale unapojaribu kujiunga ili ufanye hiyo Top Up ndio mtandao utagoma kabisa lengo lao kuu ikiwa ni kutaka muda wa salio uishe ili wazichukue ndio uanze upya.

Na kingine kibaya ukipiga ile simu namba 100 ya huduma kwa wateja ni kupoteza muda tu hakuna msaada wowote utakaopata.

Uhuni mwingine wanaofanya ukiweka salio kwa mfano shilingi 2,000 basi ghafla wanakata shilingi 200 bila sababu yoyote ili ibaki shilingi 1,800 lengo lao likiwa kwamba ununue tena vocha ya shilingi 500 au zaidi ya hapo ili upate shilingi 2,000 ambapo kwa hali hiyo wanabaki na salio lako ambalo pia watalikomba tu usipoitumia kwa kujiunga.

Hii kampuni mara ya kwanza ilionekana nzuri na wakati huo akina Voda na Airtel ndio walikuwa na huu mchezo lakini sasa na wenyewe Halotel sasa wanaufanya huku Tcra wakiwatizama tu. Pia hawa Holotel hawataki kabisa kuwambia wateja wao kwamba salio lako kinakaribia kwisha ili ukiweza uongeze salio, hamna.

Naona niende nao tu hivi ili GB zangu ziishe niachane nao, hawafai kabisa.

Halotel has really become a very hopeless telephone service provider and I can't recommend it to anyone. Bure kabisa.
 
Kabla ya upumbavu wao huo nilikuwa natumia halotel kwa kila kitu japo kuwa nilikuwa na line nyingine kwa simu, kwa sasa halotel kwangu wanajuta ninachowafanyia!

100 ukipiga, utapokelewa baada ya lisaa lizima! Upuuzi kabisa huu
 
Back
Top Bottom