Halotel: Itatoboa kwa vodacom, airtel, tigo,ttcl?

Wako vizur sana upande wa internet 3g hadi vijijini, ila wazidishe promotions na offers ili kuteka soko la mawasiliano, halo tz
 
Kumbe wao ni 2g...wenzao wapo na 4g. Nahitaji internet ya uhakika nikiwa kijijini kwangu,lkni sio 2g...
 
Kama ni 3G ngoja nitafute line yao fasta... itanifaa sana nikiwa shambani kwangu. The place I love to be, to cool, to relax
 
Halotel wamekuja kuwekeza kiasi cha takribani dola 736 million za Marekani (sawa na tsh bilioni 16.9). je pesa hizi zingekua zako ungeweza kuiona fursa hii na kuziwekeza hapa Tanzania? Ukiweka maanani kwamba kuna kampuni zipo tayari kwa miaka mingi hapa nchini zikitoa huduma ya mawasiliano lakini bado hazijaweza kushika soko ipasavyo.

Just a correction, hiyo conversion yako hapo juu umekosea, yaani umekosea mbali sana, Sio Bilioni, ni approximately Tillioni 1.6
 
Hawa jamaa watatoboa cz coverage yao ni 90% kimtandao kuanzia vijijini mpaka mjini..pia ukitumia internet yao iko poa sana kulinganisha na voda,tigo na airtel.sema upande wa marketing waongeze juhudi..
 
Na wamesha funga internet kwenye halmashauri karibu zote,shule karibu zote za serikali na taasisi nyingi zilizo chini ya serikali hapa Tz..uwekezaji wao hawa kukulupuka tu...
 
Hii kampuni inaubia na mstaafu na Ina mkataba wa kufunga net kwenye halmashauri zote nchini baada ya Muda mfupi tu pesa Yao itakuwa imerudi.
Hivi nani anaipigia debe kampuni hii, naona kuna baadhi ya watu wenye mamlaka nchini wanaichangamkia sana kumpuni hii kuliko TTCL,kazi/projects ambazo zilipaswa kutekelezwa na TTCL wanapewa wao! Kuna nini nyuma ya pazia kuhusu kampuni hii ya Wavietnam,kwa nini na wao wasije kama makumpuni megine yanayo wekeza nchi bila ya kutegemea kubebwa na Viongozi Serikalini kwa kujaribu kui-undermine TTCL kiaina.
 
Na wamesha funga internet kwenye halmashauri karibu zote,shule karibu zote za serikali na taasisi nyingi zilizo chini ya serikali hapa Tz..uwekezaji wao hawa kukulupuka tu...
Mkuu lakini kazi hiyo ilipaswa kufanywa na TTCL sio Halotel/VieTel.
 
Hii kampuni inaubia na mstaafu na Ina mkataba wa kufunga net kwenye halmashauri zote nchini baada ya Muda mfupi tu pesa Yao itakuwa imerudi.

Malizia kabisa na mtoto wake na wamefungua na kampuni ya law kama washauli wao wa mambo ya kisheria
 
Mkuu nikweli,mimi nimezungumza nao inaonekana wamewekewa gavana/spana na TCRA - walinishangaza waliposema hawawezi kwenda kinyume na charges za makampuni ya simu nchini!

Hii inamaanisha kampuni hizi za simu Nchini zinaendesha biashara zao kwa mtindo wa ki-cartel hivi ambao ni kinyume cha sheria!

Tunambiwa Tanzania inaruhusu Biashara huria lakini naona kitu hicho hakipo kwenye Makampuni ya simu yanaonekana kuiteka nyara TCRA, shinikizo la makampuni ya simu nchini ndio kumeifanya HALOTEL ifuate mkumbo bila hilo tarrifs zao zingekuwa chini/nafuu mno.

Naona Dk.Magufuli atapaswa kutupia macho makampuni haya ya Simu vile vile na utendaji kazi wa TCRA una walakini sana hawaweki maanani maslahi ya wateja/watumiaji6 wa simu.

nakuunga mkono kabisa haiwezekani kampuni ndio inatafuta wateja halafu wanakuja na insu ya mb 20 . lazima wamepigwa biti ili hawa voda , tigo , airtel waendelee kutunyonya
 
Huu mtandao ni safi sana ila swali langu, ukipiga kwa mtandao wa zantel, halotel inakwambia mtandao wa zantel umezimwa, hata simu ikiwa on, hapo sipaelewi
 
Hivi nani anaipigia debe kampuni hii, naona kuna baadhi ya watu wenye mamlaka nchini wanaichangamkia sana kumpuni hii kuliko TTCL,kazi/projects ambazo zilipaswa kutekelezwa na TTCL wanapewa wao! Kuna nini nyuma ya pazia kuhusu kampuni hii ya Wavietnam,kwa nini na wao wasije kama makumpuni megine yanayo wekeza nchi bila ya kutegemea kubebwa na Viongozi Serikalini kwa kujaribu kui-undermine TTCL kiaina.
Ilivyoanza Airtel mlisema hivyo hivyo,Viongozi na wao ni watumiaji wa sim kama wewe tu.
We mwenyewe ukiulizwa kama una TTCl mobile utakuta huna
 
Kikwazo sio voda wala tigo wala halotel na wenzao, tatizo la mawasiliano Tanzania ni ubadhilifu na ufisadi wa serikali ya CCM, watu wa TCRA na watendaji katika kampuni za mawasiliano wana hisa katika makampuni haya, hawatenganishi biashara zao na uongozi matokeo yake tunaumia sisi malofa wa UKAWA na misukule ya LUMUMBA.

Mimi nadhani suala ni kuombea tu mungu huyu Makufuli awe na uwezo wa kutenganisha Chama na Serikali na kuwa na serikali inayosimamia Sheria sio inayotafuta 10% na usishangae haya Halotel walipoomba kbali nchini wapo watu waliotoa SHARTI la wawe na hisa ndipo wa oparate. Hapo tutatoka?
 
Watatoboa.

Soko ni kubwa sana.

kwa hiyo hawajatupa hela

lakini wenzao wamefika mbali
hembu hikiri namna hata hawa waliopo wanavyomenyana halafu ww ndo unaanza yataka roho ya paka si utani
 
Mkuu nikweli,mimi nimezungumza nao inaonekana wamewekewa gavana/spana na TCRA - walinishangaza waliposema hawawezi kwenda kinyume na charges za makampuni ya simu nchini!

Hii inamaanisha kampuni hizi za simu Nchini zinaendesha biashara zao kwa mtindo wa ki-cartel hivi ambao ni kinyume cha sheria!

Tunambiwa Tanzania inaruhusu Biashara huria lakini naona kitu hicho hakipo kwenye Makampuni ya simu yanaonekana kuiteka nyara TCRA, shinikizo la makampuni ya simu nchini ndio kumeifanya HALOTEL ifuate mkumbo bila hilo tarrifs zao zingekuwa chini/nafuu mno.

Naona Dk.Magufuli atapaswa kutupia macho makampuni haya ya Simu vile vile na utendaji kazi wa TCRA una walakini sana hawaweki maanani maslahi ya wateja/watumiaji6 wa simu.
sasa km n hivi kampuni hizi za tz yasiwaze kutoka nje ya hapa sababu huko ni full huria

halafu yasifikiri yatakua kivile sababu innovation itakua hakuna sasa watashindanaje hapo km kila mtu anatoa mb8 kwa jero?

ni saa ngapi mtu ataona huduma hii hainifai nijiunge na mtandao mwingine?
 
Biashara kubwa ya mitandao ya simu siku hizi ni bando,

Bando zao zina gharama sana kufanya watu wasiwaunge mkono though internet yao ipo vizuri

basi km internet yao ipo visuri huenda wamelenga segment fulani ya watu ambayo hitaji lao kubwa ni intenet yenye ubora hata km wataipata kwa gharama kubwa.

ila je hao watu ni asilimia ngapi ya watanzania mpaka uwalenge wao tu uache kundi kubwa ambalo lina kipato cha kati?
 
Back
Top Bottom