Halmashauri yaamrisha mgambo kukatakata bidhaa za machinga Mwanza kwa kukataa kuhama

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,963
Shehena ya matunda ya wafanyabishara wa soko la Kirumba jijini Mwanza imeharibiwa kwa kukatwakatwa na watu wanaoshukiwa kuwa watendaji wa halmashauri ya Ilemela na kusababisha hasara ya mamilioni kwa wakazi wa jiji hilo

Mgambo ndio waliotumwa kutekeleza kitendo hichomusiku wa kuamkia Ijumaa kushinikiza wafanyabiashara kuhama kwenye soko hilo

Wafanyabiashara hao wameongea kwa masikitiko wakisema biashara yao wameifanya kwa fedha za mikopo na hawajui watazilipaje na Rais Magufuli alishawaruhusu wafanye biashara yao kwenye maeneo yasiyo rasmi hadi watakapotafutiwa sehemu nyingine,

mkuu wa wilaya ya Ilemela alitembelea sehemu hiyo na kukataa kuongea na waandishi wa habari na mkurugenzi wa jiji hilo alipotafutwa hakupatikana
biashara katika soko hilo zilisimama kwa siku nzima huku kukiwa na ulinzi mkali wa polisi
 
Hii serkal kila kiongozi akiamka anafanya mambo anayoamua hata kama kisheria sio sawa.

Ni hii tabia wanaiga toka kwa superior wao.

Hapo ndyo mjue Tanzania bado haijabata kiongozi.
 
Kwani mkuu wa kaya si alisema waachwe mpaka halmashauri itakapowapatia sehemu nzuri.....au wanamjaribu?
 
TBC ni chombo cha propaganda cha CCM.....wamemtafuta katibu wa ccm ili iweje? Kwann hawakumtafuta na wa CUF au Chadema!!!? Poor Tanzania
 
Hawa ndio wanaofanya watu waichukie serikali kwa maamuzi ya kijinga jinga bila kufikiri athari zake
 
Back
Top Bottom