kakuruvi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2009
- 770
- 256
Wadau kuna jambo limenipa matumaini, jana jioni nilipanda daladala pale posta hakukuwa na kugombania sana labda kwa wale waliozoea. Leo asubuhi hali ilikuwa pia sio mbaya, tumetumia dakika 30 tuka Ubungo-Posta kwani huwa tunatumia mara nyingi si chini ya saa 1.
Sasa wadau nime-note kwamba kumbe kuna idadi kubwa sana ya wanafunzi wanaosoma katikati ya mji wakitokea sehemu mbalimbali za mji, hii inamaanisha pia kuna walimu na wafanyakazi wa mashuleni wanaokuja na kurudi toka katikati ya mji ila kwa sasa wengi wamefunga shule. Kwa jinsi idadi yao ilivyo kubwa ndio inapelekea foleni kubwa hapa mjini japokuwa kuna sababu nyingine nyingi ila hii ni muhimu.
Wadau, wakifungua shule hali itarudia vile vile, nini kifanyike ili wanafunzi wasome karibu na wanakoishi bila kutumia magari (daladala)? kwa jinsi wengi wanavyopata tabu ya usafiri kinachowaleta shule za katikati ya mji nini haswa? Asanteni kwa hoja mtakazo changia.