Hali ya nchi yawatisha maaskofu

Ndugu yangu naomba nikusaidie kidogo kufikiri, hawa tunaowaita wanasiasa pia ni wa madhehebu ya kikristo, kiisilamu na hata wasio na dini pia, mathalani ww ni mkristo, kukicha wanakuandika kwa ufisadi (kweli/uongo), mchungaji akikemea utasema anafanya ama anataka kuwa mwanasiasa hapo, hivyo tuache wanasiasa wafanye watakavyo? wachungaji na/ama mashehe nao wanahaki kikatiba kwa sababu ni watanzania kuchagua/kuchaguliwa ktk nafasi za uongozi wa nchi hii, na kujadili pia. MNAPOAMINISHWA NA WENYE DHAMANA KWAMBA VIONGOZI WA DINI WASIONGELEE SIASA MJIONGEZE KUFIKIRI, OTHERWISE KICHWA CHA NINI SASA KAMA HUWEZI KUKITUMIA KUFIKIRI SI HERI UBAKI NA SHINGO PEKEE
watu wanakwenda makanisani/misikitini kufata ibada na sio siasa, kama tunataka kusikia siasa basi tutahudhuria mikutano isio isha ya CDM na CCM. Sehemu za ibada zizungumzie ibada na bungeni wazungumzie siasa.
 
Maneno ya maaskofu ni mazuri sana, ni maneno mazito kwa ajili ya taifa letu na kwa kweli yanawalenga viongozi wote lakini kichwa cha habari ni kichokonozi hakiko kwa ajili ya habari yenyewe ya maaskofu hao bali kwa lengo lingine
we mbona hueleweki? mara uponde mara usifie. Agghhhh!!!!!
 
Tatizo la watu wenye majibu ya chapchap kama hilo ni kwamba hamtafakari mambo na kutumia elimu mliy nayo kuangalia mambo. Yaani unataka kuwadanganya watu kwamba Wakristo wana MOU na serikali? Kama unayo, iweke hapa jukwaani, kwa vile watu wanajua kusoma
unabisha hata vitu vilivyowazi? MOU ya 1992.
Kweli duniani kuna watu na viatu. Na bila shaka wewe ni hichi cha pili.
 
Lowassa alikuwepo napata kigugumizi inawezekana sio kauli za maaskofu bali za Lowassa kwani katika siki za karibuni Lowassa naye amekuwa analalama kuwa serikali haifanyi maamuzi magumu na mara ajira kwa vijana wakati yuko ndani ya vyombo vyenye haki ya kutoa maamuzi kama NEC -CCM, bungeni angeweza kutoa hoja binafsi ya ajira kwa vijana, yeye na kikwete hawakukutana barabarani angeweza kwenda Ikulu kumshauri mwenzie na rafiki yake wa muda mrefu..... anazunguka nje ya system kummaliza mwenzie.....vuguvugu la Urais 2015
unajua hawa watu wanatufanya sisi watoto wadogo. Lowasa anachofanya ni kupiga ndogondogo kwa ajili ya urais 2015 na anafamya kwa baraka za Kikwete. Lowasa na Kikwete hawajakutana barabarani kwanini asiende kumwambia hukohuko ikulu kuwa vijana wanahitaji ajira? mbinu alizotumia JK ndo hizohizo anazotumia Lowasa. Misaada makanisani nk. Na wala usifikirie anaongea kummaliza mwenzake. Hiyo ni mipango yao wote (JK & EL)
 
Back
Top Bottom