akilimtindi
JF-Expert Member
- Jun 30, 2008
- 421
- 83
Mkulu Bubu ataka kusema, mimi nilitoa hoja siku moja na nadhani kama JF wataifutilia itakuwa ni hoja yenye nguvu sana. Niliomba sana wakulu wenye kujua hesabu kamili kuhusu kila pahala ccm wanapoiba pesa washushe dataz hapa JF, tutaenda na moja baada ya nyingine na kuzifanyia kazi inayotakiwa, tukifanikiwa hata kwa 50% nakupeni hakika ccm itakuwa matatani. Sasa hawana wasiwasi sana maana wanajua pesa ipo na wakitaka kufanya lolote wana imani linawezekana...pesa bwana. La msingi sisi tuchimbe sources zao za hela, tukizipata TUZIZIBE, KWISHA. Naomba hii iwe kipaumbele hapa JF kama akili zangu zitakuwa zimenielekeza vyema wakulu, tukilifanyia kazi nadhani yaweza kupunguza muda wetu. Faida zake kubwa ni mbili; 1. Kwanza tutawakosesha nguvu ccm na viongozi watashika adabu maana wasiwasi wao utaongezeka. 2. Automatically hizo fedha zitakwenda maeneo mengine muhimu kutoa huduma kama huko tunakoona panakosa huduma kila siku. Ama wapewe basi hata wale wazee wetu ambao walikuwa pale ikulu jana wakisubiri JK aseme kama ameamua kuwasanii jumla waelewe moja maana inaonekana kizazi cha wanaodai malipo ya EAC kitakwisha chote kabla hawajalipwa. Warithi hawana nguvu kama wahusika kwahiyo nguvu zinapungua siku hadi siku wanavyokufa wale wahusika kamili, hadi wafe wote.Wanatuibia mabilioni kwenye rasilimali zetu na makusanyo ya kodi. Kwa mwaka mmoja tu 2005/2006 pale BOT wamekwapua billioni 288 na hapa hatujaweka wizi wa rasilimali zetu dhahabu, Almasi, Tanzanet n.k. kutokana na mikataba isiyo na maslahi kwa Watanzania . Fikiria kama mapesa yote hayo yangeelekezwa katika kuboresha mahospitali yetu basi hata mafisadi wasingezikimbia hospitali zetu