Hali ya Fedha mfukoni ni mbaya kwelikweli, Kwenu vipi waungwana?

Ndugu yangu we acha Tu, tena kwa hapa Arusha watu wanavyopenda pombe, bar zimekauka, Yan kila mtu analia, elfu kumi best haitoshi
Hivi kina masamaki wana husiano wowote na hii hali kweli,Au ni baba mkubwa kaingia nyumba mpya na gundu
 
Mkuu, sikubaliani na wewe; jk wakati anatoka madarakani, dola kwa shilingi ilikua inakimbilia 2300 but sasa hivi ni Tsh 2186 kwa dola 1; sema ufisadi umepungua na vikao visivyokua na maana navyo vimepungua na watu wanalipa kodi stahiki this is why mzunguko wa pesa umeshuka; habari njema ni hi, wale tuliozoea kuishi maisha ya vipato vya halali hatuna cha kupoteza, kama Magu akiendelea kubana namna hi nina hakika sasa kodi za nyumba zitashuka, viwanja pia vitashuka bei na sasa ndio wakati wetu na sisi wa kujenga vibanda vya kupumzikia uzeeni!
Sasa mkuu tuliokuwa tumezoea halali si tulikuwa tukiuzia wale wezi na pesa tunapata?
Sasa wezi na wakwepa kodi pesa zao wamezitoa kwa mzunguko,sisi si ndio tutasaga meno au?
 
Bar zimepungua wateja kwa kasi ya kutisha

Katavi ngoja nikuchekeshe, kuna watu zamani ilikuwa nikiwapa ofa ya kiroba bar wanakataa, wanataka bia

sasa hivi kiroba ndo kinywaji chao kikuu, sasa cha ajabu nikifika wakinipa kiroba nakataa nawaambia sinywi nakunywa biere. hapo sasa
 
Jamani siasa ni maisha, Ebu tuelezane wajasiria mali wenzangu.

Hii hali ya mfukoni mnaionaje? Mbona mifuko ya watu nahisi imetoboka sana. Namaanisha mfukoni hela wengi hawana. Nina ka biashara kangu sehemu flani ki ukweli pato limeshuka mpaka naingia uoga.

Tatizo nini haswa? Kila ninayemuuliza analia kama mimi. Baadhi wanasema nisubiri Bunge la bajeti lipitishe 2016/2017 najiuliza upo uhusiano kweli?

Hali ikiendelea hivi, Pango linaweza kuwa mtihani achia mbali watoto shule na mahitaji yao muhimu.

Naomba Mungu na kule Zanzibar patokee maridhiano maana wafadhili nao wakifunga koki ndio balaa zaidi.

Mungu atusaidie wakuu hali ni ngumu kweli kweli sijuwi tu kwenu.


Hakuna safari za nje bila sababu, na washa za kila siku zisizo na tija.
 
Hiii hali mimi naiita tuheshimiane.

Kwa mwendo huu naona wengi wetu tutageuka kuwa wakulima iwapo serekali hii itaweka mazingira mazuri kwa mkulima kama kushusha pembejeo na kuonda kodi za manyanyaso.

Wale watu waliozoe kwenda mjini kufanya deal za katika yaani madalali kazi wanayo. Mimi miaka michache iliyopita nilinunua shamba kabuku nikawa naliendeleza kidogokidogo. Sasa wangalau vijana wa shambani kila wiki wananitumia hela ya mauzo ya mbogamboga na mauzo ya mayai. Ila kama ni mtu ulikuwa unangoja kutengeza risiti fake ofisini imekula kwako.

Na huu ni mwanzo tu, mpaka mwisho wa mwaka huu wale wanaoishi kwa ujanja ujanja ndio mwisho wao ni lazima sasa wakatafute kazi za halali na hakuna zaidi ya kilimo kwani ajira hakuna.
Nimeipenda!
 
wakuu nyinyi wote hamnishindi mm....niko sehemu ya makontena...pesa yangu nusu na robo ya mshahara nilikopea...nikitegemea dili kazin..rais kabana sasa....yaan bank inaingia laki na kumi kwa mwez...kila siku naona kama siku zirud nyuma
 
Walioathirika wengi ni wale waliozoea ujanja ujanja Ila kwa sie tunaofata straight line ndio kwanza tunaona mambo yanazidi kuwa mazuri.
 
Juzi kati nilienda coco katikati ya week mida ya saa tano unusu ivi nkakuta parking lot kavu kabisaa... na ile karioke imedoda mbaya.. yaani hali ni tete.
Coco ilikuwa ikifika saa sita usiku deileee ilikuwa inachanganya mpaka kuchee ila sasa duuuuhh...
 
Ninawaonea huruma sana wanafunzibwa kike, walishazoea kuishi maisha ya 'ma TX' wakati wangali wanafunzi, walikua na maisha ghali kuliko hata senior employees.
Sasa hivi ili kuweza angalau ku maintain ka status wanalazimika kuzibua na kuongeza vyanzo vingi vya mapato...(Mabwana zaidi).
Matokeo yake shule inapoteza maana na uzito kwao.
 
mpaka kuna muda inabidi unywe chai katikati ya asubuh na mchana apo unakuja itafuta jioni.unakua umesave
Daah umenikumbusha those days i used to be a college boy,kipindi hicho boom limekata unapiga chai saa sita then lunch sa kumi na mbili jion hiyo ndo imetoka usiku unapiga kavu kavu.
 
mimi nimeanzisha maradi njooni tujioganize tujichange kila mmoja lakilaki kisha tushuke kijijini tukalime sio mnalalamika tuu! mnafikili pesa itajileta yenyewe!
 
Katavi ngoja nikuchekeshe, kuna watu zamani ilikuwa nikiwapa ofa ya kiroba bar wanakataa, wanataka bia

sasa hivi kiroba ndo kinywaji chao kikuu, sasa cha ajabu nikifika wakinipa kiroba nakataa nawaambia sinywi nakunywa biere. hapo sasa
Hahahaah viroba vimepata soko na pombe zile chakavu
 
Sasa mkuu tuliokuwa tumezoea halali si tulikuwa tukiuzia wale wezi na pesa tunapata?
Sasa wezi na wakwepa kodi pesa zao wamezitoa kwa mzunguko,sisi si ndio tutasaga meno au?
Nyie mliyekua mnauza kwa bei mbaya (cause wateja wenu walikua mafisadi) sasa hivi ni zamu yenu kushusha bei and hence na sisi tutanunua sasa, bei ya viwanja nchi hi kwamfano ni kubwa sana kuliko hali halisi. Kuna wakati Fulani kule Uingereza katika jiji la London Mtanzania 1 alinunua nyumba kwa Pound 450,000/= na ikawa breaking news kwamba how comes mtu kutoka nchi masikini kama Tanzania aweze kununua nyumba ya bei mbaya katika moja kati ya majiji makubwa duniani? Wakati huo Exchange rate ya Pound kwa Tsh ilikua 2300, pesa ile ukii convert kwa Tsh ni kama sh 1,035,000,000, hiyo ni hesabu ya wakati ule but juzi tu hapo kuna mtu aliwahi kutwambia Tsh 10M ni hela yake ya mboga na jamaa yake (kaka yake wa kufikia) alimtoa kama 1.6 B. Ufisadi ukibanywa namna hi wenye vipato halali tutapumua kidogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom