Hali ya Fedha mfukoni ni mbaya kwelikweli, Kwenu vipi waungwana?

kinachoniuma ni vitu kuzidi kupanda bei...yaani ukienda sokon ndo utaelewa na kila m2 anasingizia huo hvo kua tutaisoma namba..haya maigizo yamezidi bora vyakula uishuke alafu ndo mfanye mengne.
 
Hahaha kumbe sio mm mwenyewe,mm mpaka ni wasa wameniendea kwa washenzi mini,!?
 
Hivi majipu yana husiano wowote na hii inshu.
Yes coz hela za dili zimepungua sana au zimetoweka kabisa, so kila mtu anakuwa makini na hela yake maana hana uhakika kama kesho atapata nyingine
 
Duh!

Kumbe mitanzania ilikuwa inataka mabadiliko ya uongo! Mlidhani mabadiliko ni Kikwete na wanawe kuacha kuingia magogoni tu? Haya ndio mabadiliko ya kweli!

Kila aliyekuwa anaishi kiujanjaujanja haya ndio mabadiliko na sio kuzungusha mikono au kuwaimbia wenzako wataisoma namba!

Nidhamu ya pesa, juhudi na uwajibikaji kazini, udhibiti wa malipo hewa na hali nyingine za ujanjaujanja ndio sehemu ya kwanza ya mabadiliko tunayoanza nayo!

Mtusamehe wananchi ila tunaijengea nchi uwezo na tunaanza na nidhamu!

Tutaheshimiana tu!
 
Sisikii tena zile mbwembwe za vijana kushinda Samaki Samaki, Maisha club na kwingineko wanakouza sura

tumebadili gia angani na sasa tunapatikana sana tandika madafu, kwa mnyamani na mahakama ya mateso ambako kote huko ni uswazi na kunapatikana gongo za ndizi na zile za mvuke wa kinyesi ambazo ukizinywa tu lazima mdomo wako utabadili mwelekeo huku ukiwa umebabuka.
 
Ha ha ha ha nina kama week siijui chai, naamka nimechelewa nasonga ugali tu, sio kwamba sipendi chai ila mifukooooooo imetobokaaaa
sasa kama zaman iyo hali ndio ilikuwa ngumu najiuliza je sasa hivi itakuwaje?

Nakumbuka 2007-2009 mtu unaamkia kiporo cha kande baadaye unazuga kitaa unavamia kwa jirani lunch dona na arage haijaungwa mida ya jioni kahawa na kashata eti kuiga wazungu "snacks" kwa muktadha huo kwa nini IQ isidumae na CCM kuongoza miaka nenda rudI?
 
Jamani siasa ni maisha, Ebu tuelezane wajasiria mali wenzangu.

Hii hali ya mfukoni mnaionaje? Mbona mifuko ya watu nahisi imetoboka sana. Namaanisha mfukoni hela wengi hawana. Nina ka biashara kangu sehemu flani ki ukweli pato limeshuka mpaka naingia uoga.

Tatizo nini haswa? Kila ninayemuuliza analia kama mimi. Baadhi wanasema nisubiri Bunge la bajeti lipitishe 2016/2017 najiuliza upo uhusiano kweli?

Hali ikiendelea hivi, Pango linaweza kuwa mtihani achia mbali watoto shule na mahitaji yao muhimu.

Naomba Mungu na kule Zanzibar patokee maridhiano maana wafadhili nao wakifunga koki ndio balaa zaidi.

Mungu atusaidie wakuu hali ni ngumu kweli kweli sijuwi tu kwenu.

Allah akufungulie milango ya Rizik mimi kwa upande wangu Alhamdulillah sio tajiri kama haoo ila tajiri wa nafis na Rizk yangu halal jalali ananipatia sina shida kiviile.... Alhamdulillah
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom