Hali mbaya SANA.... sikitiko

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
24,893
11,289
Kwa kweli there is no better way to explain shida za mafuta, umeme, nk.

Upande wa wafanyabiashara, wana hoja na zina mantiki... hasa kuhusu ulaghai!!
Upande wa serikali... tunasikia kujadili, kutoa notice etc.
upande wetu, hali mbaya sana... wapo wanaojifungulia njiani, wanakosa elimu, wanaokosa vipato nk

kinachoniudhi ni jinsi wahindi na waarabu ambavyo hadi sasa hawajaathirika... this just confirm kwamba wana mitandao na serikali zao ndani ya hii nhci na hawaathiriki kwa namna yoyote na janga hili.... THEY HAVE ESTABLISHED THEIR OWN FUEL SUPPLY SYSTEMS

SAD!!
 
Inanisikitisha sana, watanzania ni mafundi wa kulalamika tu - leo mji mzima wanakimbia kimbia na vidumu hovyo hovyo - hakuna majibu ya maana toka serikali yao na wao wanaishia kulaumu tuuu hakuna action.

Ndiyo maana Wakenya wanatutania - Wa TZ maneno ni mingiiiii......

Angalieni sky news muone wenzetu wa Uingeleza (mnaopenda kuwafanyia reference kwa kila kitu) walivyousafisha mji wa Tonteham. yaani sasa hivi sisi wananchi tungekuwa tumeviteka vituo vyote tangu jana. Police wasingethubutu kutupiga mabomu ya machozi kwani wakifanya hivyo tu, tungetishia kulipua vituo vyote.

kwa maana hii naomba tukae kimya tukisubiri hatua za na Serikali yetu kupitia wizara ya NISHATI na Madini - tusiharibu amani na utulivu uliodumu miaka yote - TUZIDI TUVUMILIANA:

Na tunaelekea kubaya zaidi, hapa kazini inabidi tuombe ruhusa walau ya wiki kwani kuna hatari ya kulala barabarani sasa.
 
tz hatuna umoja, hakuna jambo litakalo tuweka barabarani kama umeme na mafuta vinatutesa na bado tunakenua meno.
 
Halafu king ndo hana habari kabisa.
Haya makampuni c yanamilikiwa na ccm na wao ndo wafadhili wakuu wa kampeni za ccm. Wewe unatarajia nini hapo?
 
JAMANI SHIMA TUUNGANENI TUWATOE HAWA MA JASUSI, ni kwa njia ya umma tu ndo wataelewa kuwa tumechokaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kuna dokezo kwamba endapo serikali itafuta lesseni za biashara kwa kampuni hizo kubwa za mafuta zilizogoma basi tunaweza kuwa gizani kwa zaidi ya miezi miwili kwani meli ya mafuta ambazo hizi kampuni zimefanya order ambazo zipo on transit zitarudi, it takes weeks ku order mafuta hadi yafike dar. Unless Jeshi liingilie kati kuuza mafuta kwenye depo's.

Hali ni mbaya sana ndugu zangu na Bado - napenda hi kitu ili watanzania tujifunze matatizo - tupo soft sana ili Next time tukiambiwa tuchague watu makini nafikiri tutasikiliza.
 
jana nimesikitika sana sana .... mfanyabiashara mmoja wa samaki kutoka mwanza generator yake iliisha mafuta .... akapata hofu kubwa sana ya kuogopa samaki wake kuharibika kiasi cha kutaka kuwauza hata kwa bei ya chini .... akaanza kulalamika na mjadala ukaanza ...swali la mjadala likawa je ni nani wa kulaumiwa kwa hiki kilichompata huyu mfanyabiashara ..... je ni tatizo la umeme au ni tatizo la uhaba wa mafuta ...?
 
Hii inaaibisha serikali sana..ila wananchi kuna somo tunapata kuhusu mamlaka ya seikali halali iliyowekwa na wananchi na iliyowekwa kwa nguvu ya fedha..
 
It can't go any worse than it is now!!! This place is called rock bottom,you can't go any further down! The only way left to go is UP!
dy/dx=0
d[SUP]2[/SUP]y/dx[SUP]2[/SUP] = +ve
"Wajasiriamali" wanazidi tu kutafuta ulipo ukomo wa uvumilivu wa watanzania. Let's see.....
 
Watz cjui nani katuroga, tunalalamika tu, there is no any actions.
c.c.m nchi imeshawashinda hii, haitaji elimu ya chuo kikuu kufahamu hili, badala ya kutatua kero za wananchi wao wanadhunguka nchi kupiga kelele za kuvuana magamba, wawo c ndio serikali? wawakamate hao wanaowaita mafisadi weka ndani, kazi ya polisi sio kuzuia maandamano ya amani, kamateni mafisadi.
kutumia nguvu ya umma ndio sasa, tunangoja nin watz?
 
Kwa kweli there is no better way to explain shida za mafuta, umeme, nk.

Upande wa wafanyabiashara, wana hoja na zina mantiki... hasa kuhusu ulaghai!!
Upande wa serikali... tunasikia kujadili, kutoa notice etc.
upande wetu, hali mbaya sana... wapo wanaojifungulia njiani, wanakosa elimu, wanaokosa vipato nk

kinachoniudhi ni jinsi wahindi na waarabu ambavyo hadi sasa hawajaathirika... this just confirm kwamba wana mitandao na serikali zao ndani ya hii nhci na hawaathiriki kwa namna yoyote na janga hili.... THEY HAVE ESTABLISHED THEIR OWN FUEL SUPPLY SYSTEMS

SAD!!

Usihofu sana ndugu yangu. Wakati mwingine inabidi mtu apitie hali mbaya ili apate akili ya kuweka sawa mfumo wake wa maisha na kuuboresha. Naamini huu ni wakati muafaka wa watanzania kutafakari njia bora zaidi ya kuifikia ile ahadi tamu ya Mheshimiwa Rais ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA. Mpaka sasa sio watanzania wengi tunaojua kuwa tunaye "common enemy" anayesababisha haya matatizo yote na kuwa haya matatizo yana uhusiano wa moja kwa moja. Yaani kupanda gharama za maisha, kukosekana kwa umeme wa uhakika, mgomo wa wauza mafuta, ufisadi, umaskini, ujinga na maradhi. Siku tukimjua huyu adui hatutakumbuka huu upuuzi wa udini, ukabila, ukanda, uchama na mambo yanayofanana na hayo. Tutachukua hatua stahiki muda muafaka ukifika.
 
jamani kweli hali mbaya, jana j4 ndugu yangu amelazimika kusukuma gari yake datsun kutoka Makongo mpaka Mwenge kijiweni kwake na hiyo ni licha ya kununua mafuta lita 5 kwa tshs. 17,000 na mbaya zaidi hakuna ambalo serikali inalifanya. sasa ndio naona nguvu ya wafanyabiashara wanaoichangia ccm na viongozi wafanyabiashara. kunahitajika mapinduzi hata ikibidi watu walambwe shaba labda kutakuwa na mabadiliko.
 
jana nimesikitika sana sana .... mfanyabiashara mmoja wa samaki kutoka mwanza generator yake iliisha mafuta .... akapata hofu kubwa sana ya kuogopa samaki wake kuharibika kiasi cha kutaka kuwauza hata kwa bei ya chini .... akaanza kulalamika na mjadala ukaanza ...swali la mjadala likawa je ni nani wa kulaumiwa kwa hiki kilichompata huyu mfanyabiashara ..... je ni tatizo la umeme au ni tatizo la uhaba wa mafuta ...?
Uzuri ni kuwa vyote viwili waziri ni Ngeleja............ tatizo si la umeme na wala si la uhaba wa mafuta ... NI LA NGELEJA NA JK WAKE........... Si tuja shida ya mafuta yeye kaenda kufuturisha wakristu ambao hata hawajafunga....
 
Back
Top Bottom