Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,803
- 71,229
Kodi inalipwa kwa ajili ya maendeleo ya taifa lolote husika na kuhudumia raia wake. Kanuni hii ya kulipa kodi ilikuwepo ulimwenguni miaka mingi hata kabla ya Yesu.
Kwa Tanzania katika miaka mingi ya karibuni CAG na vyombo mbalimbali wamefichua ukwapuaji endelevu mkubwa wa fedha za umma na watu wakiwa ni wale wale kila mwaka na hakuna hatua za wazi zinachukuliwa.
Sasa kubwa kuliko yote ni kuwa katika ripoti ya 2021/22 iliyoko bungeni inayoonyesha takribani robo ya fedha tukusanyazo zinaenda katika ubadhilifu, Spika wa Bunge (kwa maelekezo toka juu) anawazuia wawakilishi wa wananchi (hata kama ni wamchongo) kuijadili tena eti hadi Novemba.
Katika hali hii ni nani kwa hiari yake kabisa anaweza kulipa kodi akijuwa inaenda kuliwa na majambazi wajiitao viongozi?