Hakuna wa kuihujumu e-GA, Serikali haina Software engineers kama sekta binafsi

Madumbikaya

JF-Expert Member
Jun 6, 2018
638
1,902
Maamuzi ya wizara ya habari kutafuta Software developers au ushirikiano toka sekta ya kibenki ni wa kupongezwa,Serikalini bado wanajikongoja sana software engineers wake
,Wale vijana waliokuwa wabunifu pale BOT sasa walihamishwa na kupewa vyeo huko e-GA

Baada ya kusikia wizara ya habari wameingia makubaliano na NMB kwenye mambo ya kuendeleza Software ,Wafanyakazi wazembe na wasio wabunifu serikalini wameanza kulia lia kuwa wanahujumiwa

Kama vijana Serikali wana talent watengeneza software kama wenzao wa Mabenki au Makampuni ya simu

Vitambulisho vya NIDA tu vinawasumbua hapo serikalini

e-GA au mamlaka ya serikali mtandao ilianzishwa mwaka 2012 chini ya Dkt Jabir Bakari

Ni ukweli usiopingika moja ya mafanikio ya e-GA ni utengenezwaji wa mfumo wa kulipa bili na kodi kwa kutumia Control number

Je ni nani walihusika na utengenezaji wa GePG? na Walitoka sekta gani? na Je walikuwa waajiriwa wa e -GA?

Waliotengeneza mfumo wa GePG hawakuwa waajiriwa wa e-GA chini ya Dkt Jabiri na wala hawakuwa na mpango wa kufanya kazi e-GA

Waliohusika kutengeneza mfumo wa GEPG ni vijana wa kitanzania waliokuwa wanaishi marekani na wanafanya kazi sekta binafsi lakini wakashawishiwa na Bank kuu ya Tanzania kurudi kufanya kazi nyumbani yaani benki kuu ya Tanzania (BOT).Hawa vijana waliajiriwa na Benk kuu ya Tanzania kama Software engineers ili kuwasaidia kubuni mifumo mbalimbali

Wakati wa hayati JPM wengi wa vijana hawa waliokuwa wabunifu na baada ya kupata umaarufu na mafanikio makubwa waliondolewa BOT na kuhamishiwa wizara ya fedha na wengine kupewa vyeo kama Mr Saus na hivyo kupunguza kasi ya utendaji,Unapomuondoa mbunifu na kumpa cheo unarudisha ubunifu wake,Ndani ya sekta binafsi wabunifu wanaongezewa fedha au malipo na sio kuwapa vyeo

Hapa Tanzania kwenye mabenki na makampuni ya mawasiliano(simu) ndio utakutana na bright Software engineers walioajiriwa kwa ajili ya kubuni bidhaa za kimtandao ambazo tunazitumia kurahisisha maisha kwa sasa

Kitendo cha wizara ya habari kuingia makubaliano na Bank ya NMB ni cha kupongezwa sana,

Hakuna asiyeona mapinduzi makubwa yaliofanywa upande wa kidijitali ndani ya Bank ya NMB toka kuasisiwa kwake ,Na hii ni kazi ya software engineers

Mkurugenzi mpya wa CRDB bwana Nsekela akiwa anatoka NMB kwenda CRDB alishawishi baadhi ya software engineers toka NMB ndio anafanya nao kazi sasa CRDB kubuni bidhaa mbalimbali za kimtandao

Je?Unafahamu kwa sasa Tanzania malipo yote unayafanya kwa kutumia whatsapp iwe kulipa bill ,kutuma pesa au kununua luku

WhatsApp yako ndio Benk yako kwa sasa ,Benk ya I&M Tanzania ina huduma hiyo ya kisasa kutokana na skills za Software engineers wake waliopo kenya

Wafanyakazi wa serikali wengi wana hofu isioonekana hasa hawa wanaofanya kazi e-GA,Kinachotakiwa ni ubunifu basi na sio kuishi kwa porojo au kazi alinipa mjomba
 
Back
Top Bottom