Hakuna umuhimu wa machine za kubeti mitaani

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
Kuna viongozi wananufaika na hizi machine za ku bet ambazo zimesambaa kila mahali.

Kama sio hivyo basi tuambiwe faida ya hizi machine kwa taifa. Kila mahali kuna machine za wachina wanapita kukusanya pesa kila siku pesa badala ya kusaidia kamii inaenda kusaidia hawa wawekezaji fake na viongozi wala rushwa.

Mwaka jana nilikuta mlinzi wangu wa shamba ameweka rehani Pikipiki yangu ili apate pesa ya kubeti kule kidomole Bagamoyo.

Huko vijijini watu wanaishia kwenye kubeti badala ya kufanya kazi.
 
Ww una kaz gan???.....ujue wanalipa mapato!!.... Ukisema mchna asiwepo means mtoe na SPORT PESA ...and the likes
 
Naamini asilia mia wachina export price zote tunazotuma kwao wanatumia haya madubwi kutulipa, huku sisi import zote tunazoagiza kutoka kwao tunawalipa tena kwa mfumo wa dollar jasho kubwa la nchi na wananchi tunachopata kisa viongozi wachache wanaonufaika na michezo hii

Ukiwaza sana haya machine ya mchina Yana faida Gani kwa mwananchi wetu, ingekua sisi ndo tumeyapeleka kwao isingepita muda wangetunyogea mbali
 
Kuna viongozi wana nufaika na hizi machine za ku bet ambazo zimesambaa kila mahali. Kama sio hivyo basi tuambiwe faida ya hizi machine kwa taifa. Kila mahali kuna machine za wachina wanapita kukusanya pesa kila siku...
kama hailipi wasingebet. Hakuna binadamu anayependa matatizo hasa ya kifedha.

Mashine zile we zichukulie kama sanduku la kijumbe wa kikoba yaani leo unaweka kesho utachukua
 
Back
Top Bottom