"Hakuna ukabila wala ubadhirifu CHADEMA"-Chacha Wangwe

MMJJ,
Usituchekeshe hapa. Ulikuwa na nafasi ya kumuuliza Bw. Wangwe hayo maswali na hukuyauliza, sasa unayaleta JF ili iweje wakati hayupo?

Nimesikiliza mahojiano yako yote na Lissu pamoja na ya Wangwe. Ukweli ni kuwa Wangwe ndiye aliyetoka mshindi kidedea tena kwa sana na Lissu ameonekana kama vile ametumwa kuendelea kumchomea Wangwe.

Kama unataka kufanya mahojiano ya haki, mlete Mbowe sasa tusikie na yeye anasemaje kuhusu hizo shutuma. Au kama ikiwezekana waweke wote kwa pamoja, Mbowe vs Wangwe ili baada ya hapo tuweze kujua nani ni mkweli.

Changia angalau dola 10 for half an hour of interview.. zinagharimu!
 
....huyu ndio unamkabidhi nchi kweli? mbona EPA na Meremeta itakuwa cha mtoto!
 
Baadae mmuulize na Ben alisemaje kuhusu RUSHWA wakati anafanya kampeni na mara alipoingia madarakani.
 
Wangwe yuko sahihi.
chadema kuna ukabila na pia hakuna ukabila.
Kama ilivyo sehemu nyingine yoyote.
Inategemea tu uko upande gani wakati unaongea.
Kama haujakugusa vibaya, hauna nguvu/haupo, ila ukikugusa vibaya ndio mbaya.
Wanasiasa wanaamini kutambikia mizimu yao, itakuwaje wasiwe na ukabila?
tutakuwaje na makabila bila ukabila?
Wangwe alikuwa sahihi wakati ule (kwa hisia na muono wake) na yuko sahihi sasa ( kwa hisia na muono kwake)
Ndio siasa hiyo.
 
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-

Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.

Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?

Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.

Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?

Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?

Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?

Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.

Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.

Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.

Katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliopita, CHACHA WANGWE hakuwa chaguo la Mwenyekiti MBOWE, lakini aliweza kushinda. Kutokana na kitendo cha CHACHA WANGWE kutangaza kwa mara ingine kugombea Uenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi wa Disemba 2008 amezidi kujenga maadui kutoka Makao Makuu ya chama hicho. Hofu ya MBOWE inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa WANGWE anaungwa mkono na matawi mengi ya CHADEMA nchini kutokana na msiamamo wake wa kutenda haki na kusimamia ukweli daima.

Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha. Kwa sababu hiyo, WANGWE anadai kwamba hakuelezwa siri alizovujisha hatua ambayo inakidhi matakwa ya kisheria kwamba MBOWE amemhukumu WANGWE bila hatia. Hatua hii ina lengo la kukwaza ustawi wa demokrasia na utawala bora katika vyama vya siasa.

Katika hili la kuvujisha siri WANGWE anajitetea kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa basi mtu aliyetakiwa kuwajibika ni DR SLAA ambaye mke wake ni diwani wa kuchaguliwa wa CCM wakati mkewe CHACHA WANGWE ni mwanachama mwaminifu wa CHADEMA. Kitendo cha DR SLAA kuwa na mke mkereketwa wa CCM yamkini Nyaraka za siri za CHADEMA zinaweza kuangukia kirahisi kwa mkewe na hatimae CCM na pia wageni wa CHADEMA wanaofika nyumbani kwa DR SLAA ambako kuna tawi la CCM kwa maana ya mkewe DR SLAA ambaye anawajibika kuwakirimu wageni na hivyo kusikia mazungumzo yao. WANGWE anataka kujua ni nani kati yake na DR SLAA anaeweza kuvujisha siri za CHADEMA?

Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani. Urafiki huu unaweza kuwa wa binafsi/kawaida kuliko mambo ya siasa kwa sababu ya uzalendo, hivyo tofauti ya itikadi siyo uadui bali ni suala la kusimamia ukweli kama ambavyo ZITTO KABWE alivyojumuika na wabunge wa CCM katika kamati ya madini ya Bomani.

Pia WANGWE anadai, kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa mbona MBOWE amewahi kuonekana akiwa katika mazungumzo na Rais JAKAYA KIKWETE hata kufikia kumkumbatia mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Halikadhalika MBOWE ameonekana katika mazungumzo na viongozi wengine wa CCM, vivyo hivyo wana CHADEMA wengine?

Kwa ujumla kashfa hizi zinakuja wakati bado baadhi ya Watanzania wanahoji uadilifu wa FREEMAN MBOWE. Kashfa ya kukopa na kushindwa kulipa deni la NSSF kwa muda stahiki ilitia mashaka ya uadilifu wa MBOWE kwa taifa lake. Hakika bila kujibu hoja nzito za WANGWE, Mwenyekiti MBOWE asitarajie kupata kura za Watanzania wenye fikra mbadala katika uchaguzi ujao ndani ya chama chake na asijisumbue kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.

Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???
 
mi napendekeza tuwe na Hansad ya JF tuwe tunaweka habari muhimu za hawa wanasiasa wetu uchwara zitatusaidia huko mbeleni kuwabana wakae pembeni.
 
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???

Naona hatimaye Waraka huu umeletwa JF. Huu ndio Waraka alioandika Balillle na kumpa Mzee Yusuph Halimoja, ndio waraka ambao Chacha Amekuwa akipita katika vyombo vya habari kutoa hoja zake akiusoma.

Katika waraka huu mtaona ule mkakati niliowadokeza wa kumweka Mbowe mwenyewe kikaangaoni, hii ilikuwa ni baada ya mkakati wa mwanzo wa kumng'oa kwanza Dr Slaa kushindwa.

Katika waraka huu Kamati ya Mziray imetajwa, mtakumbuka niliwaeleza siku za nyuma kuhusu hili. Hii ndio njia mpya ya Wagawe, Uwatawale inayoendelea.

Na katika taarifa hii Balille anafanya spinning sasa kuwa ripoti hii iliminywa toka mwezi Disiemba kumbe ukweli ni kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati Bwana Mziray ndiye ambaye katika vikao vyote vya kamati kuu vilivyofuata hakutaka kuleta ripoti yake mpaka Mkakati na Rostam wa kumtoa Dr Slaa Dodoma Juni 28 akaipeleka ripoti hiyo Dodoma siku moja kabla ya kikao ili ripoti hiyo isipitie kwenye sekretariati kama zilivyo nyaraka nyingine za kamati kuu.

Kabla ya kuipeleka ripoti hiyo Dodoma alishatoa ripoti hiyo kwa Rostam, Kaborou, Ballile na Halimoja. Ndipo Kaborou akamsaidia Chacha kuandika waraka wa kumpinga katibu mkuu ambao mwanzoni ulikuwa utoke kwa jina lake lakini baadaye akaamua utoke kwa jina la Yusuph Halimoja kwa wajumbe wote wa kamati kuu. Ballile naye akajiandaa kuchapa ripoti hiyo Mtanzania ndio maana habari ya Mtanzania ya Juni 29 kama nilivyowadokoza siku chache zilizopita ilikuwa na taarifa za ripoti hii kuwa ilimkandamiza Dr Slaa(hiki ndicho Ballile alitaraji kitokee lakini hakikutokea). Badala yake taarifa ya wazee ndio ikachukua uzito na hatimaye ikapelekea Chacha kusimamishwa.

Sasa kuhusu taarifa ya Mziray, pamoja na kuwa ilifika dodoma bila kupitia sekretariati mwenyekiti Mbowe akiamini katika demokrasia alikubali ijadiliwe(kwa mujibu wa wachambuzi hili lilikuwa kosa la kisiasa la mbowe).

Taarifa hiyo ilijikita katika kusema CHADEMA kuna ubaguzi wa ukabila, elimu na dini. Kwamba CHADEMA inapendelea zaidi wasomi katika kugawa nafasi za utumishi makao makuu na hata viti maalumu. Pia taarifa ili eleza kuhusu ukabila kwa kutumia takwimu zilizotajwa hapo juu.

Mjadala ulipoanza ikabainika kwamba Kamati ya Mziray iliandika taarifa za uwongo kabisa na majungu kwa kutoa takwimu na hoja za uwongo. Kura zikapigwa na wajumbe 29 wa Kamati Kuu wakaikataa hiyo taarifa kama si nyaraka ya chama(total dismissal). Wajumbe wawili tu wakapiga kura za ndio, Mwenyekiti wa kamati Mziray na mjumbe wa Kamati Mzee Shilembi wa Shinyanga. Hata wajumbe wengine wawili wa kamati hiyo waliikataa ripoti hiyo, Katibu wa Kamati mama Sophia Khatau alipiga kura ya hapana na Wakili Mbogoro Mjumbe wa kamati naye alikataa kwa kuwa hakushiriki kwenye vikao vya Kamati. Mjumbe mmoja toka Pemba wa Kamati hiyo alifariki kabla ya Kamati kuwasilisha kazi yake.

Sasa kwa kuwa Mkakati wa Rostam kuichafua CHADEMA hususani Dr Slaa ulijikita katika ripoti hiyo na walitarajia kuwa ndio njia ya kumuondoa Dr Slaa, wakafanya kikao tarehe 29 Dodoma na kukubaliana kati ya Ballile na Rostam kwamba waitoe ripoti hiyo bado pamoja na kuwa imekataliwa na ili isionekane ni Rostam Rai na Mtanzania zijikite katika kumnukuu Chacha Wangwe akizungumzia ripoti hiyo kuwa ni maoni ya wanachama, na gazeti la Majira liichape ripoti yote kama ilivyo.

Ripoti hiyo iliandaliwa na Mziray katika kile kinachoitwa Kamati imewahoji viongozi na wanachama 42 wa CHADEMA. Alipotakiwa kuwasilisha majina ya waliohojiwa na Kamati kuu akasema wamewahoji viongozi 31 tu na alipotakiwa kutoa majina yao hakuwa nayo, ila Bwana Mziray alikiri mbele ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho kuwa kati ya aliowahoji ni pamoja na Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi bwana Kaborou.

Kikao cha jana pamoja na mambo mengine kilikubaliana kwamba Rostam atoe fedha za ziada kwa ajili ya ripoti hiyo kusambazwa nchi nzima kwa ajili ya kumchafua Dr Slaa na CHADEMA.

Kama nilivyowaahidi, nitawaletea taarifa kuhusu kikao cha kesho kadiri nitakavyozipata

PM
 
RUZUKU, UKABILA WAIGAWA CHADEMA

CHADEMA ndicho chama pekee nchini kilichokuwa kinaonekana kutokuwa na migogoro, lakini hili la ruzuku na mengine yanaelekea kukigawa katika makundi mawili ya CHADEMA – MBOWE na CHADEMA – WANGWE.

Hali hii imejitokeza baada ya kutokea malalamiko ya wanachama wa CHADEMA kususu masuala kadhaa ya msingi. Masuala hayo yameibua mgawanyo uliozaa makundi hayo mawili na baadaye Mwenyekiti wa chama hicho FREEMAN MBOWE akatangaza kumsimamisha Makamu Mwenyekiti (CHACHA WANGWE).

Kwa tafakuri pana kila Mtanzania alitarajia kwamba kabla ya kumsimamisha Makamu Mwenyekiti, CHACHA WANGWE, Mwenyekiti wa chama hicho alitakiwa kujibu tuhuma moja baada ya ingine ili kujisafisha yeye mwenyewe pamoja na viongozi wengine wa juu wa CHADEMA.

Kimsingi,CHACHA WANGWE anamtuhumu MBOWE katika masuala yafuatavyo:-

Mosi, Kuna matumizi mabaya ya ruzuku (ufisadi wa ruzuku) ndani ya CHADEMA Makao Makuu. Hivyo, CHACHA WANGWE anamtaka Mwenyekiti FREEMON MBOWE atoe maelezo ya matumizi ya Ruzuku, ambayo ni fedha ya walipa kodi inayotolewa na serikali kwa vyama vyenye wabunge. Aidha WANGWE anamtaka MBOWE aonyeshe mapato na matumizi ya Ruzuku hiyo katika vikao vya chama au aunde kamati ya kuchunguza tuhuma hizo. Pia, WANGWE ana mashaka na hesabu zinazoonyesha mgawanyo wa matumizi ya ruzuku yanayopelekwa kwa msajili wa vyama vya siasa kutoka chama cha CHADEMA.

Pili, CHACHA WANGWE hakubaliani na kitendo cha Mwenyekiti na Katibu Mkuu (DR WILBROAD SLAA) kuzuia ruzuku isifike mikoani. Anasema hali hii ina maana matawi ya chama yasifunguliwe na chama kisiwe na ofisi hali ambayo inadhoofisha chama. Vivyo hivyo, WANGWE hakubaliani na kitendo cha MBOWE kufuja fedha za chama kwa ziara za helkopta huku akiwaacha wagombea ubunge na udiwani wa chama chake hawana msaada wowote wa kifedha kutoka katika chama. Katika mazingira haya WANGWE anauliza nani anakihujumu chama kati ya MBOWE na WANGWE? Nani anadhoofisha CHADEMA?

Tatu, CHACHA WANGWE ana hoja kwamba MBOWE, anawajibika kuwaeleza watanzania, ni kwa vipi wabunge watano kati ya sita wa kuteuliwa (viti maalum) wote watoke mkoa wa Kilimanjaro ( MBOWE ni Mchaga wa Kilimanjaro). Ikumbukwe kwamba Tanzania bara ina mikoa 21 na Zanzibar mikoa 5. Kwa kawaida, idadi ya viti maalum inategemea idadi ya wabunge ambao chama kinapata katika uchaguzi mkuu, ambapo asilimia 90 ya viti vya ubunge zilizoleta viti maalum vya CHADEMA zilitoka kanda ya Ziwa. Hivyo, MBOWE kasahau kanda zilizosaidia CHADEMA ikipata viti maalum na kuvipeleka KILIMANJARO.

Nne, CHACHA WANGWE anamtaka MBOWE, aeleleze inakuwaje kati ya wakurugenzi nane wa Idara mbalimbali za CHADEMA wanne ni Wachaga wa Kilimanjaro?

Tano, WANGWE anamtaka MBOWE, aeleze umma wa watanzania inakuwaje Madereva wote wa Makao Makuu ya CHADEMA ni Wachaga kutoka Kilimanjaro?

Sita, WANGWE anataka MBOWE, ajibu tuhuma kwamba yeye mwenyewe, DR WILBROAD SLAA na PHILIMON NDESAMBULO wanajilipa fedha kwa ajili ya kurudisha gharama walizotumia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. WANGWE anauliza mbona wanachama wengine hawarudishiwi gharama hizo akiwemo yeye WANGWE? Je, huu siyo ufisadi? Je huku ni kutenda haki?

Saba, WANGWE anataka kujua ni kwa nini miaka minne iliyopita MBOWE alivunja tawi la CHADEMA mkoa wa DAR ES SALAAM na kubaki na CHADEMA Makao Makuu. Hatua hii imekifanya chama hicho kukosa viongozi na wawakilishi wa chama mkoa wa Dar ES salaam.

Nane, WANGWE anataka kujua kwa nini Wakurugenzi wote wa CHADEMA wameteuliwa na MBOWE badala ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya chama kwa mujibu wa katiba ya CHADEMA. Aidha, Kwa Mujibu wa katiba ya CHADEMA kifungu 7.7.3 (vii), Katibu mkuu anatakiwa kuwajibika kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekti. Hata hivyo, DR SLAA ambaye ni Katibu Mkuu wa CHADEMA hakuwa akitoa ushirikiano kwa WANGWE hadi kufikia kumnyima ofisi alipoteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.

Tisa, Katika moja ya hatua za kumfukuza WANGWE katika Uongozi, Katibu Mkuu aliitisha kikao cha Kamati ya wazee wanne wa CHADEMA lakini kati yao wawili wakiwa wa kabila la Mwenyekiti . Wazee hao wa Kichaga ni EDWIN MTEI ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Wazee wa CHADEMA na PHILIMON NDESAMBULO. Hapo kulikuwa na mgongano wa kimaslahi (conflict of interest). Ikumbukwe kwamba, Mwenyekiti mstaafu wa CHADEMA Bw. EDWIN MTEI ni baba mzazi wa mke wa FREEMON MBOWE kwa maana kwamba MTEI ni mkwe wa MBOWE. Mke wa MBOWE anaitwa DR LILIAN EDWIN MTEI ( Hivi sasa anajulikana kwa jina la DR LILIAN FREEMON MBOWE) ni binti wa EDWIN MTEI.

Kumi, CHACHA WANGWE analalamika kwamba suala la kumfukuza liliibuka ghafla katika kikao cha Kamati Kuu ya CHADEMA wakati halikuwemo katika agenda. Inadaiwa kwamba MBOWE ndiye aliibua agenda hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za CHADEMA, kama suala hilo lilitakiwa kuwa agenda ilitakiwa lijulishwe kwa wajumbe siku 21 kabla ya kikao ili wapate mawazo ya wanachama. Hata hivyo, liliibuka katika kikao bila mtuhumiwa CHACHA WANGWE kujiandaa. Aidha, katika kuhakikisha kuwa WANGWE anavuliwa madaraka yake kwenye kikao, baadhi ya viongozi waliotakiwa kuhudhuria kikao hicho kwa mujibu wa katibu hawakupata mwaliko kwa sababu ilihofiwa kuwa wangekuwa upande wa WANGWE.

Kwa ufupi WANGWE anadai kwamba kuna ufisadi Makao Makuu ya CHADEMA. Kwamba MBOWE hajatoa maelezo kuhusiana na tuhuma hizo na badala yake anamtuhumu WANGWE kwamba anakigawa chama na kuamua kumsimamisha uongozi.

Katika uchaguzi wa Makamu Mwenyekiti uliopita, CHACHA WANGWE hakuwa chaguo la Mwenyekiti MBOWE, lakini aliweza kushinda. Kutokana na kitendo cha CHACHA WANGWE kutangaza kwa mara ingine kugombea Uenyekiti wa CHADEMA katika uchaguzi wa Disemba 2008 amezidi kujenga maadui kutoka Makao Makuu ya chama hicho. Hofu ya MBOWE inatokana na ukweli kwamba, hivi sasa WANGWE anaungwa mkono na matawi mengi ya CHADEMA nchini kutokana na msiamamo wake wa kutenda haki na kusimamia ukweli daima.

Hivyo, MBOWE akamjengea zengwe kwamba, WANGWE anavujisha siri za chama lakini katika kikao cha Kamati Kuu hawakuweza kueleza siri ambazo WANGWE anadaiwa kuvujisha. Kwa sababu hiyo, WANGWE anadai kwamba hakuelezwa siri alizovujisha hatua ambayo inakidhi matakwa ya kisheria kwamba MBOWE amemhukumu WANGWE bila hatia. Hatua hii ina lengo la kukwaza ustawi wa demokrasia na utawala bora katika vyama vya siasa.

Katika hili la kuvujisha siri WANGWE anajitetea kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa basi mtu aliyetakiwa kuwajibika ni DR SLAA ambaye mke wake ni diwani wa kuchaguliwa wa CCM wakati mkewe CHACHA WANGWE ni mwanachama mwaminifu wa CHADEMA. Kitendo cha DR SLAA kuwa na mke mkereketwa wa CCM yamkini Nyaraka za siri za CHADEMA zinaweza kuangukia kirahisi kwa mkewe na hatimae CCM na pia wageni wa CHADEMA wanaofika nyumbani kwa DR SLAA ambako kuna tawi la CCM kwa maana ya mkewe DR SLAA ambaye anawajibika kuwakirimu wageni na hivyo kusikia mazungumzo yao. WANGWE anataka kujua ni nani kati yake na DR SLAA anaeweza kuvujisha siri za CHADEMA?

Aidha, imeonekana kwamba, kutokana na nafasi yake ya Ubunge WANGWE na wabunge wengine wa upinzani wanaweza kujipatia marafiki kutoka chama tawala CCM kama ambavyo Wabunge wa CCM wanaweza kuwa na marafiki kutoka vyama vya upinzani. Urafiki huu unaweza kuwa wa binafsi/kawaida kuliko mambo ya siasa kwa sababu ya uzalendo, hivyo tofauti ya itikadi siyo uadui bali ni suala la kusimamia ukweli kama ambavyo ZITTO KABWE alivyojumuika na wabunge wa CCM katika kamati ya madini ya Bomani.

Pia WANGWE anadai, kwamba kama kuzungumza na wana CCM ni kosa mbona MBOWE amewahi kuonekana akiwa katika mazungumzo na Rais JAKAYA KIKWETE hata kufikia kumkumbatia mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005. Halikadhalika MBOWE ameonekana katika mazungumzo na viongozi wengine wa CCM, vivyo hivyo wana CHADEMA wengine?

Kwa ujumla kashfa hizi zinakuja wakati bado baadhi ya Watanzania wanahoji uadilifu wa FREEMAN MBOWE. Kashfa ya kukopa na kushindwa kulipa deni la NSSF kwa muda stahiki ilitia mashaka ya uadilifu wa MBOWE kwa taifa lake. Hakika bila kujibu hoja nzito za WANGWE, Mwenyekiti MBOWE asitarajie kupata kura za Watanzania wenye fikra mbadala katika uchaguzi ujao ndani ya chama chake na asijisumbue kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Natoa mwito kwa MBOWE kuitisha mkutano wa waandishi wa Habari kujibu tuhuma moja baada ya nyingine. Vinginevyo MBOWE atakuwa ameingia katika kundi la Wenyeviti wa vyama vya siasa wanaoua demokrasia nchini.

Kwa upande mwingine, DR SLAA na KABWE ZITTO wamekuwa watu muhimu kwetu watanzania katika kutoa hoja zinazohusiana na ufisadi bungeni lakini inashangaza wameshindwa kudhibiti ufisadi wa MBOWE ndani ya CHADEMA na badala yake wamemwachia WANGWE pekee. Hakika watu hawa walitusaidia sana katika kuunda tume za kuchunguza Richmond na EPA inakuwaje kwa muda mrefu tangu Desemba 16, 2007 wanakalia ripoti ya Kamati ya Mziray iliyoundwa kuchunguza mambo yanayoweza kusababisha migogoro ndani ya CHADEMA? Kamati hiyo ilibaini ubaguzi wa kikabila na kidini katika CHADEMA lakini haikuwekwa wazi kwa Watanzania na wala haijafanyiwa kazi. Je tuwaelewe vipi viongozi hao wa CHADEMA? Ufisadi ni ule unaofanywa na viongozi wa serikali ya CCM tu? Je sio kweli kwamba Hisani siku zote inapasa kuanzia nyumbani???

Kama nilivyowaeleza, uamuzi wangu wa kuanika ili mikakati umefanya Ballile aingie kazini kwa nguvu kubwa zaidi. Sasa ni vyema fikra mbadala akaingia kwanza hapa na kujibu hoja:

https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=15327

Rostam ana kazi mwaka huu

PM
 
Leo nawakumbusha maneno ya Chacha Wangwe mara baada ya kuchaguliwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA. Alifanya mkutano na waandishi wa habari pale makao makuu ya CHADEMA ambapo pamoja na mambo mengine alisema- hakuna ukabila CHADEMA, wala hakuna matumizi mabaya ya ruzuku. Alisema pia anakubaliana na maamuzi ya kutumia helikopta. Alisema yanayosemwa kuwa amesema ni uchonganishi wa magazeti. Wakati huo tamko lake liliandikwa na magazeti ya Mtanzania, Habari leo na mengineyo. Kuna mtu anaweza kutuletea vile vipande vyake?

Sehemu ya maneno yake ilinukuliwa na Tanzania Affairs hapa:

Meanwhile CHADEMA itself was not without its problems. According to the Swahili press the leadership had to deny that there were differences within the party. Tarime MP and deputy chairperson Chacha Wangwe, told the press that there was no row within the party, and he had never accused the leadership of misuse of funds or of ethnic bias. Party Leader Freeman Mbowe said “We are as united as ever, but the pro-CCM media has been trying to smear us.” Wangwe was elected party deputy chairperson by 56 votes to 38 after a heated debate. He will hold the office for one year, and, according to the media, might then try to replace Mbowe. Some CHADEMA members were reported to consider Wangwe an ‘unguided missile’ and others baptised him ‘the Jacob Zuma of CHADEMA’ – Mtanzania

Chanzo: http://www.tzaffairs.org/?p=264

Swali la kujiuliza: Je, Chacha ameamua kuyakana maneno yake mwenyewe?

Usicheze na ndege tunduni wewe, chochote kile utasema ili mradi watoto wapishane TT
 
nilijua hili la ukabila litakifuna chadema na linaendelea kulitafuna msipojirekebisha chadema mtakwisha na kukiua chama mtabaki historia tu.nakumbuka mbowe alikuja na sera yake ya majimbo kipindi kile cha uchaguzi wa 2005 na jk alitumia hiyo kama siraha kwa kumgeuzia mwenyewe na ikawa ni mwiba kwa mbowe.mambo haya ya ukabilia baba wa taifa alijitahidi sana kuyakemea kwani alijua madhara yake.chonde chonde chadema jisafisheni kwa hili.aisaidii sana kukanusha tu na kukana wakati tunaona wabunge wa viti maalum wengi ni kutoka kule kuleeee......! anyway najua kuna watu wanakereka na hili na mimi nataka wakereke ili mwisho wa siku wajirekebishe ili tuwe na upinzani makini bungeni.tunataka mwaka 2010 ikiwezekana tuwe na zaidi ya 50% ya upinzani bungeni...upinzani wowote ule iwe ccm ndio wapinzani au vyama vingine ndo viwe vya upinzani maaadamu ni upinzani uwe zaidi ya 50% zidi ya chama chochote kitakachochukua sirikali..
 
Kuna kitu kisichokuwepo kinacholazimishwa kuwa kipo, nacho ni ukabila wa CHADEMA. Ukabila manake ni ubaguzi, maamuzi kufanyika au kutofanyika kwa misingi ya kabila. Unaweza kutueleza ukabila wa CHADEMA? Au na wewe unaingia mkenge wa propaganda za Chama Cha Mafisadi?

Halafu kuna ambalo lipo linalolazimishwa kuwa halipo- ni kama Rostam wa Chama Cha Mafisadi anavyokwenda KKKT na kulazimisha kusema kwamba yeye HANA UFISADI!

Tofauti ni kwamba la kweli litakuwa la kweli na la uwongo, litakuwa laungo. Tuendelee kusubiri tu!

Asha
 
tehehehhhhhehhheheee....
nilijua wenyewe litawakera tu....
anyway nakubaliana na wewe kuwa ni la kweli litakuwa la kweli na la uwongo litabaki la uongo...tuendelee kusubiri tu!
 
Kuna kitu kisichokuwepo kinacholazimishwa kuwa kipo, nacho ni ukabila wa CHADEMA. Ukabila manake ni ubaguzi, maamuzi kufanyika au kutofanyika kwa misingi ya kabila. Unaweza kutueleza ukabila wa CHADEMA? Au na wewe unaingia mkenge wa propaganda za Chama Cha Mafisadi?

Halafu kuna ambalo lipo linalolazimishwa kuwa halipo- ni kama Rostam wa Chama Cha Mafisadi anavyokwenda KKKT na kulazimisha kusema kwamba yeye HANA UFISADI!

Tofauti ni kwamba la kweli litakuwa la kweli na la uwongo, litakuwa laungo. Tuendelee kusubiri tu!

Asha

Kuhani Mkuu

Una maoni gani juu ya kauli ya Chacha kuwa hakuna ukabila wala ubadhirifu wa ruzuku CHADEMA?

Mara ya mwisho nimemsikia Chacha KLH News anasema wamejaa Wachaga CHADEMA.

Na akasema kuna financial improprieties.

Kama baada ya hapo kageuka naomba nipe update.

Lakini kama ni lolote alilowahi kusema siku za nyuma hiyo hainishangazi. Wote Chacha, Tundu, Mbowe na kina Slaa na CHADEMA nzima wote walikuwa wanawaka moto wa mapenzi dhidi ya Chacha.

Tundu kasema juzi yeye ni mmoja wa walio m-promote na kumpigia Chacha tarumbeta siku za nyuma. Wote walikuwa katika honey moon!

Na mimi nina swali kwenu: Kama huyu Chacha ni kichaa mmoja anaetaka kukwida watu kwenye mikutano, mwongo mmoja anaezusha shutuma za ukabila, mamluki aliyepandikizwa na CCM, mwenye matusi yasiyoweza kutajwa JF wala kwenye radio, basi ilikuwaje mumpe Uongozi wa juu kabisa wa Chama pembeni ya Mwenyekiti?

Nyinyi kina Tundu Lissu na Bob Makani na Dr. Slaa, ma prominent attorneys na madaktari wa falsafa na wajenga hoja kina Asha Abdallah, ilikuwaje kuwaje mmkampa loose canon Uwenyekiti? Ilikuwaje?

Na kama hakuna ushahidi wa neutral parties kwamba alitaka kuwapiga basi munge invest kwenye video camera chumba cha mkutano. Naamini mnaweza ku afford manake mnatembea na helikopta manjiani!
 
Mbona hauulizi ilikuwaje mkamsimamisha?

Mbona haulizi kwanini Zitto Kabwe na wengine hawakuwa wakiumuunga mkono?

Lakini kwani wakati huo alikuwa amepiga mtu kikaoni basi na kuvujisha siri za chama kwa kiwango alichofanya akiwa makamu mwenyekiti basi?

Kwa hiyo umekubali kwamba the guy is a flip flopper eeeh. Kama hakuona ukabila januari 2008 ameuonaje mara baada ya kusimamishwa?

Nakwambia akihojiwa tena leo atakuwa na maneno tofauti kabisa na jana!

Haya honey moon imekwisha, Chacha halisi amewekwa hadharani kama nitatumia maneno yako.

Bado unamuunga mkono?

Asha
 
Back
Top Bottom