Hakuna Mtanganyika (mtanzania bara) Anayemiliki Ardhi/Nyumba Zanzibar

Wakuu,
Naomba kufahamishwa endapo kanisa katoliki, sabato/SDA wanapo milikishwa ardhi wanaiwakilisha Tanzania Bara?
maana nimeshindwa kuelewa jibu hili.

Kanisa linawakilisha Mungu na sio nchi kaka.

Unataka kutwambia kuwa lile pale Kivukoni linawakilisha Vatican?

Utawala wa Kanisa Katoliki lina Jimbo Zanzibar chini ya uongozi wa Bishop na paroko zake kama Kanisa hilo hilo lilivyo na majimbo yake huko unakokwita Tanzania Bara.

Hakuna Kanisa la "Tanzania Bara" Mkuu
 
Huu ni uongo uliokithiri na kushtadi.

Mfano mzuri ni maeneo ya Chake-Chake, Kusini, Pemba ambako Kanisa la Roman Catholic wanamiliki kiwanja na wamejenga kindergarten

Hapa hapa Chake-Chake, Kanisa la SDA wanamiliki kiwanja na wamejenga hospitali.

Unguja, maeneo ya Cheju, Kanisa la Roman Catholic wanajenga high school.

Lakini kubwa ni kwamba karibu mtaondoka, viwanja vya nini?

Nyie huku mje mlime tu mpaka "muungano" utakapo kata roho.

Kweli bana Makaimati, huu ni uongo mkubwa, kuna watanganyika kibao nawafahamu wanamiliki viwanja na nyumba hapa Bububu, hebu acheni uzandiki wa uongo, in fact hakuna mtanganyika anayezuiwa kufanya chochote (legally and halal) in Zanzibar, tatizo linakuja ni pale mnapotaka kununua kiwanja ili kujenga bar, aaaaagh no,no,no,no because the spirit of the peoples of Zanzibar is increasing economic generation with halal activities-period!
 
...kuna watanganyika kibao nawafahamu wanamiliki viwanja na nyumba hapa Bububu, hebu acheni uzandiki wa uongo, in fact hakuna mtanganyika anayezuiwa kufanya chochote (legally and halal) in Zanziba
Mtanzania Bara haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar!

THE LAND TENURE ACT, 12 - 1992
ENACTED by the House of Representatives of Zanzibar.

Right of a Grant of land.

24.(1) The right of occupancy shall only be granted to
Zanzibaris who are above the age of eighteen.

"Zanzibari" means:

(a) any person who is a citizen of Tanzania in
accordance with the laws relating to citizenship
and that he was born or has been residing in
Zanzibar before and up to the 12th of January
1964;

(b) any person who, as from the 26th day of April,
1964 is a citizen of Tanzania and was born in
Zanzibar with both of his parents being
Zanzibaris or either his father or mother being
Zanzibari in accordance with the Zanzibari Act,
1985;

(c) any person who is a citizen of Tanzania and was
born or has been residing in Zanzibar before the
26th day of April, 1964; and

(d) any person who is a citizen of Tanzania with
both of his parents being Zanzibaris or either his
father or mother being Zanzibari in accordance
with paragraph (a), (b) or (c) above.

57: Zanzibari requirement.

If it is determined that:

(a) any grantee is, at any time, proved to be a non-
Zanzibari; or

(b) an interest holder-makes, or attempts to make, a
transfer of his right of occupancy to a non-Zanzibari;

an order of termination shall be issued by the Minister which
shall provide that the right of occupancy is terminated and
the land shall be vacated forthwith.

Ibara ya 57 ya sheria hiyo inasema ukigundulika wewe sio Mzanzibar na unamiliki ardhi utafutwa haki hiyo na kutakiwa kuondoka mara moja!

Ibara ya 57 inasema ukigundulika wewe sio Mzanzibar na unamiliki ardhi utafutwa haki hiyo na kutakiwa kuondoka mara moja!

Kwahiyo this means hawa wakuu waliosema wananyumba Zanzibar na wanapangisha huenda Asset zao zikawa hatarini, duh kama hii ni kweli basi ninawashauri waanze kutafuta wateja
 
a HAWANA NYUMBA WALA VIWANJA ZENJI HAO. WAMEAMUA TU KUONGEZA IDADI YA THREADS TU. AU VP WATAKUWA NI MAGAMBA.
 
Your real self - the ''I am I'' - is master of this land, the ruler of this empire. You rightfully have power and dominion over it, all its inhabitants, and all contained in its realm.

That tells us all that the Union was not intended to Occupy Zanzibar, there must be another reason very cheap no Meaning right now...
 
Huu ni uongo uliokithiri na kushtadi.

Mfano mzuri ni maeneo ya Chake-Chake, Kusini, Pemba ambako Kanisa la Roman Catholic wanamiliki kiwanja na wamejenga kindergarten

Hapa hapa Chake-Chake, Kanisa la SDA wanamiliki kiwanja na wamejenga hospitali.

Unguja, maeneo ya Cheju, Kanisa la Roman Catholic wanajenga high school.

Lakini kubwa ni kwamba karibu mtaondoka, viwanja vya nini?

Nyie huku mje mlime tu mpaka "muungano" utakapo kata roho.

Wazanzibar twawakaribisha sana bara ili mjenge majumba yenu ikitokea mungano unakufa nyie mtakuwa mmesha tujengea haijarishi mtauza kwa bei rahisi au kwa kuwazawadia watu au kwa kuyatelekeza majengo yeno. Pia wabara wazuieni kujenga huko kweno ili waendelee kuwekeza Tanganyikani kwao
HABARI NDIO HIYO!
 
Jambo hili ni mojawapo ya matatizo ya Muungano. Lakini pia kuna jambo jingine: Wanasiasa kutoka Zanzibar wanaweza kushika madaraka ya juu nchini Tanganyika, lakini Mtanganyika hawezi kufanya hivyo huko Zanzibar. Hata Rais Mtanganyika (ambaye ndiye Rais wa Muungano) haitawali Zanzibar na wala sidhani hana ofisi yake huko. Baadhi yetu tuliopendelea serikali 3 i.e. ya Zanzibar, Tanganyika na ya Muungano, tulitaka kulikwepa tatizo hili; lakini pia kumzuia Mzanzibari anayetawala Tanganyika na timu yake wasitumie nafasi zao kujiboresha kupindukia kiuchumi; jambo ambalo labda hawakuthubutu kulifanya walipokuwa madarakani huko Zanzibar. Hoja kama hizi zinaashiria kuwepo Muungano usio na usawa. Yapo mambo mengi yenye utata na Muungano huu, lakini kwa kifupi inaelekea ni Watanganyika wanaobeba gharama kubwa za kuwabembeleza Wazanzibari wabaki kwenye Muungano. Hivi majuzi Waziri Sitta alikuwa akizungumzia deni kubwa TANESCO inayoidai Zanzibar na kuongeza kwamba kama siyo Muungano Wazanzibari wasingelimudu deni hilo. Swali ni mpaka lini? Kwa upande mwingine, Wazanzibari hawawezi kulaumiwa katika hili maana wao wanaombwa kuja huku Tanganyika kutawala katika kile kinachoweza kutafsiriwa kuwa ni 'kuimarisha Muungano'. 'Uimarishwaji' huo, unaweza kuzaa asimia fulani ya Wazanzibari wanao milki uchumi wa Tanganyika lakini bila kuwa na Mtanganyika visiwani humo anaye milki hata kiamba.
Mtanzania Bara haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar!

THE LAND TENURE ACT, 12 - 1992
ENACTED by the House of Representatives of Zanzibar.

Right of a Grant of land.

24.(1) The right of occupancy shall only be granted to
Zanzibaris who are above the age of eighteen.

"Zanzibari" means:

(a) any person who is a citizen of Tanzania in
accordance with the laws relating to citizenship
and that he was born or has been residing in
Zanzibar before and up to the 12th of January
1964;

(b) any person who, as from the 26th day of April,
1964 is a citizen of Tanzania and was born in
Zanzibar with both of his parents being
Zanzibaris or either his father or mother being
Zanzibari in accordance with the Zanzibari Act,
1985;

(c) any person who is a citizen of Tanzania and was
born or has been residing in Zanzibar before the
26th day of April, 1964; and

(d) any person who is a citizen of Tanzania with
both of his parents being Zanzibaris or either his
father or mother being Zanzibari in accordance
with paragraph (a), (b) or (c) above.

57: Zanzibari requirement.

If it is determined that:

(a) any grantee is, at any time, proved to be a non-
Zanzibari; or

(b) an interest holder-makes, or attempts to make, a
transfer of his right of occupancy to a non-Zanzibari;

an order of termination shall be issued by the Minister which
shall provide that the right of occupancy is terminated and
the land shall be vacated forthwith.

Ibara ya 57 ya sheria hiyo inasema ukigundulika wewe sio Mzanzibar na unamiliki ardhi utafutwa haki hiyo na kutakiwa kuondoka mara moja!

Nd.wana jf. Nasikia ati ni marufuku kwa mtu kutoka bara (tanganyika) kumiliki aridhi,nyumba au jengo huko Zanzibar. Je ni kweli?
Kama jibu ni NDIYO. Kwa nini huku Tanganyika hatujawa na sera kama hiyo kwa wazanzibar?

Wazanzibar hawapaswi kumiliki ardhi huku Tanganyika. Kwani katiba inasemaje? Si kwamba mtanzania ana uhuru wa kuishi popote ndani ya Jamhuri ya Muungano. Kwa nini watanganyika hawamiliki aridhi kule?

Hii ni kweli wala sio uongo inaonekana makubaliano ya Muungano wengi wenu hamuja yapitia ? moja ya makubaliano ni nikuuwa Tanganyika yenu na hisoria yenu sasa imebaki kuwa homeless wa Tanzania isio na mbele walo nyuma ya historia yake, pili ni ujanja mwingi mbele kiza hii ni kweli na fuatilieni sheria za Zanzibar moja ni kuto kumiliki ardhi.

Mimi ninae eleza haya ni Mzanzibar fyoko huyu huyo mwenzenu alio sema kuwa Wtanganyika wajitao Tanzania hawawezi kumiliki ardhi nikweli Artcle of Union inasema hivyo, hii ni kweli na ulozeni sheria za Zanzibar mutambiwa kuwa Shogo hawezi kumiliki ardhi wala kuowa mwanamkke wa kiZanzibar rabda a m-rape.
 
Jambo hili ni mojawapo ya matatizo ya Muungano. Lakini pia kuna jambo jingine: Wanasiasa kutoka Zanzibar wanaweza kushika madaraka ya juu nchini Tanganyika, lakini Mtanganyika hawezi kufanya hivyo huko Zanzibar. Hata Rais Mtanganyika (ambaye ndiye Rais wa Muungano) haitawali Zanzibar na wala sidhani hana ofisi yake huko. Baadhi yetu tuliopendelea serikali 3 i.e. ya Zanzibar, Tanganyika na ya Muungano, tulitaka kulikwepa tatizo hili; lakini pia kumzuia Mzanzibari anayetawala Tanganyika na timu yake wasitumie nafasi zao kujiboresha kupindukia kiuchumi; jambo ambalo labda hawakuthubutu kulifanya walipokuwa madarakani huko Zanzibar. Hoja kama hizi zinaashiria kuwepo Muungano usio na usawa. Yapo mambo mengi yenye utata na Muungano huu, lakini kwa kifupi inaelekea ni Watanganyika wanaobeba gharama kubwa za kuwabembeleza Wazanzibari wabaki kwenye Muungano. Hivi majuzi Waziri Sitta alikuwa akizungumzia deni kubwa TANESCO inayoidai Zanzibar na kuongeza kwamba kama siyo Muungano Wazanzibari wasingelimudu deni hilo. Swali ni mpaka lini? Kwa upande mwingine, Wazanzibari hawawezi kulaumiwa katika hili maana wao wanaombwa kuja huku Tanganyika kutawala katika kile kinachoweza kutafsiriwa kuwa ni 'kuimarisha Muungano'. 'Uimarishwaji' huo, unaweza kuzaa asimia fulani ya Wazanzibari wanao milki uchumi wa Tanganyika lakini bila kuwa na Mtanganyika visiwani humo anaye milki hata kiamba.
Majina ya Watanzania yanafana, na hapa tunatumia sana majina ya kutunga, labda siwe, lakini kama ndiwe Ludovick Mwijage aliyeandika kitabu kuhusu mkono wa chuma wa utawala wa awamu ya kwanza, basi nianze na kusema Heshima Yako, Mzee.

Utotoni filamu moja ambayo ilinigusa sana ni Kilio cha Uhuru, kumhusu Steve Biko, aliyepigania haki za Waafrika Kusini. Kuna sehemu Biko anatandikwa mbakora za kufa mtu, anatupwa kwenye karandinga la political police wa kaburu kuelekea mahabusu, anaenda kufa.

Nikisoma kitabu chako pale unapoelezea safari zako za kufungwa tambala jeusi usoni umetupwa nyuma ya landlover la majasusi wa Nyerere kutoka sijui Swaziland huko mpaka Ukonga, huwa nakumbuka sana filamu ya Biko, halafu roho inaniuma sana. Ahsante kwa kujitoa mhanga kwa ajili ya kizazi cha wanao na wajuu zako, ambao ndio sisi. Pole lakini angalau tunashukuru hukufa!

Haya ya Muungano ni baadhi ya mambo yaliyopitishwa kitemi temi na tawala zile, na waliokua wanawaogopa kwamba wana mawazo tofauti na mikono ya chuma ya dola basi walipata shurba bin zahma. Preventive detention na vichapo na vyumba vya giza na water boarding na kuminywa mapumbu na kadha wa adha. Usipofia mahabusu msalie mtume.

Ndio haya tumeamka sasa tunayapinga kwa wingi, bungeni na mtaani na mahakamani, na mashuleni na majumbani na makanisani, na vijiweni na mitandaoni na misikitini. Sio mmoja mmoja kama enzi zenu zile.

Unaandika sheria inayosema Mtanzania bara haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar na Wapemba wamejaa Ilala wanamiliki maduka ya kuuza vipuri nchi nzima, unategemea tujisikie vipi?

Tunasema sasa huu ujinga, hatutaki ujinga, tuna nguvu ya kupiga vita ujinga, Muungano na tunauvunja!
 
Hii habari ya mtanganyika hawezi kumiliki ardhi zenji ni kweli,na hii sio upendekleo bali ndio sheria ya ardhi ya zanzibar,mtuyoyote asiekua mzanzibari hana haki ya kumiliki ardhi ila kwa bahati mbaya imebakia vitabuni tu sheria hio,kwani wapo watanganyika kibao na pia nje ya Tanzania wapo pia walomiliki ardhi.ila ukweli utabakia kua sheria hairuhusu,
Hii musiishangae haina tafauti na ile kesi ya mafuta na gesi ya zanzibar kua ni ya muungano lakini gesi ya songo songo nk na maadini kutoka bara si ya muungano.

Kwalugha rahisi huu muungano haifai kuwepo au ukiwepo uanzishwe upya na makubaliano mapya kama kweli ipo nia safi ya muungano.vyenginevyo bora kuvunjwa tukakutana huko EAU kunatosha.
 
Mtanzania Bara haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar!

THE LAND TENURE ACT, 12 - 1992
ENACTED by the House of Representatives of Zanzibar.

Right of a Grant of land.

24.(1) The right of occupancy shall only be granted to
Zanzibaris who are above the age of eighteen.

"Zanzibari" means:

(a) any person who is a citizen of Tanzania in
accordance with the laws relating to citizenship
and that he was born or has been residing in
Zanzibar before and up to the 12th of January
1964;

(b) any person who, as from the 26th day of April,
1964 is a citizen of Tanzania and was born in
Zanzibar with both of his parents being
Zanzibaris or either his father or mother being
Zanzibari in accordance with the Zanzibari Act,
1985;

(c) any person who is a citizen of Tanzania and was
born or has been residing in Zanzibar before the
26th day of April, 1964; and

(d) any person who is a citizen of Tanzania with
both of his parents being Zanzibaris or either his
father or mother being Zanzibari in accordance
with paragraph (a), (b) or (c) above.

57: Zanzibari requirement.

If it is determined that:

(a) any grantee is, at any time, proved to be a non-
Zanzibari; or

(b) an interest holder-makes, or attempts to make, a
transfer of his right of occupancy to a non-Zanzibari;

an order of termination shall be issued by the Minister which
shall provide that the right of occupancy is terminated and
the land shall be vacated forthwith.

Ibara ya 57 ya sheria hiyo inasema ukigundulika wewe sio Mzanzibar na unamiliki ardhi utafutwa haki hiyo na kutakiwa kuondoka mara moja!

Hio ni granted right of occupany Mkuu.
 
Kanisa linawakilisha Mungu na sio nchi kaka.

Unataka kutwambia kuwa lile pale Kivukoni linawakilisha Vatican?

Utawala wa Kanisa Katoliki lina Jimbo Zanzibar chini ya uongozi wa Bishop na paroko zake kama Kanisa hilo hilo lilivyo na majimbo yake huko unakokwita Tanzania Bara.

Hakuna Kanisa la "Tanzania Bara" Mkuu

Mkuu unajichanganya jibu lako na dondoo uloanzisha vinajichanganya. pia natumaini swali langu hukulielewa ndo maana kwa majibu hayo
unajichanganya.
 
Nd.wana jf. Nasikia ati ni marufuku kwa mtu kutoka bara (tanganyika) kumiliki aridhi,nyumba au jengo huko Zanzibar. Je ni kweli?
Kama jibu ni NDIYO. Kwa nini huku Tanganyika hatujawa na sera kama hiyo kwa wazanzibar?

Wazanzibar hawapaswi kumiliki ardhi huku Tanganyika. Kwani katiba inasemaje? Si kwamba mtanzania ana uhuru wa kuishi popote ndani ya Jamhuri ya Muungano. Kwa nini watanganyika hawamiliki aridhi kule?
Huu ni uongo na uzandiki mkubwa sana.

Mimi mwenyewe si Mtanzania kwa maana ya Uraia lakini nina nyumba Shanghani na mwera hapa unguja na vile vila huko Bara nina nyumba Alikhan street , Upanga na Isamiro Mwanza.

Vile vile najua kuna wabara wengi sana wana nyumba hapa Unguja. Na hiyo nitokea enzi na enzi. Labda utoe mfano mti aliyetaka nunua nyumba kwa kufuata sheria kisha akazuiwa kwa sababu ya uraia wake. Na mimi nitakupa kwa majina kabisa wabara wenye nyumba hapa Unguja na Pemba.
 
Ndugu Taso, shukrani nyingi. Naam, mimi ndiye mtunzi wa kitabu hicho. Huo ni upande mwingine wa Awamu ya Kwanza ambao wakati huo ulikuwa hauelezwi kinagaubaga, kadamnasi. Ninamshukuru Mwenye Uweza, nilisurvive kipindi hicho cha giza jambo ambalo linanilazimu kukizungumzia kipindi hicho ili walao kuwapa sauti akraba wengine waliopoteza maisha yao na kwa hiyo hawawezi kujisemea wenyewe. Vinginevyo, kuyafahamu maovu ya wakati huo yatokanayo na matumizi mabaya ya madaraka ya kisiasa na nguvu za dola inaweza kukisaidia sana kizazi kipya cha wanasiasa kutoruhusu maovu hayo yatokee tena katika jamii yetu. Na kwa kuwa yatakuwa yanafahamika bayana, kila yanapojaribu kujitokeza, umma-hasa kizazi kipya-kitayapinga vikali: kama tunavyoona leo hii. Gurudumu la mabadiliko likishaanza kuzunguka halisimami. Mwisho umma wa Tanzania utayathibiti matendo ya mtawala yasiyofaa kabla hayajaliathiri taifa na raia wake. Hata hivyo, ni muhimu sana kuwepo usawa wa madaraka kati ya serikali na raia wake kwa jambo hili kuwezekana. Ni swali ambalo halijajibika kama katiba mpya inayozungumziwa itarekebisha kasoro hii.
Asante kwa mara nyingine na jumapili njema.
Majina ya Watanzania yanafana, na hapa tunatumia sana majina ya kutunga, labda siwe, lakini kama ndiwe Ludovick Mwijage aliyeandika kitabu kuhusu mkono wa chuma wa utawala wa awamu ya kwanza, basi nianze na kusema Heshima Yako, Mzee.

Utotoni filamu moja ambayo ilinigusa sana ni Kilio cha Uhuru, kumhusu Steve Biko, aliyepigania haki za Waafrika Kusini. Kuna sehemu Biko anatandikwa mbakora za kufa mtu, anatupwa kwenye karandinga la political police wa kaburu kuelekea mahabusu, anaenda kufa.

Nikisoma kitabu chako pale unapoelezea safari zako za kufungwa tambala jeusi usoni umetupwa nyuma ya landlover la majasusi wa Nyerere kutoka sijui Swaziland huko mpaka Ukonga, huwa nakumbuka sana filamu ya Biko, halafu roho inaniuma sana. Ahsante kwa kujitoa mhanga kwa ajili ya kizazi cha wanao na wajuu zako, ambao ndio sisi. Pole lakini angalau tunashukuru hukufa!

Haya ya Muungano ni baadhi ya mambo yaliyopitishwa kitemi temi na tawala zile, na waliokua wanawaogopa kwamba wana mawazo tofauti na mikono ya chuma ya dola basi walipata shurba bin zahma. Preventive detention na vichapo na vyumba vya giza na water boarding na kuminywa mapumbu na kadha wa adha. Usipofia mahabusu msalie mtume.

Ndio haya tumeamka sasa tunayapinga kwa wingi, bungeni na mtaani na mahakamani, na mashuleni na majumbani na makanisani, na vijiweni na mitandaoni na misikitini. Sio mmoja mmoja kama enzi zenu zile.

Unaandika sheria inayosema Mtanzania bara haruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar na Wapemba wamejaa Ilala wanamiliki maduka ya kuuza vipuri nchi nzima, unategemea tujisikie vipi?

Tunasema sasa huu ujinga, hatutaki ujinga, tuna nguvu ya kupiga vita ujinga, Muungano na tunauvunja!
 
Hii ni hatari kwa muungano!sijui faida ya huu muungano,laiti wabara tujiweke pembeni ili tuone hawa ndugu zetu wanaohitaji kujitenga watafanyeje..Ila hapa hekima zaidi na utu utumike kutatua matatizo hayo
 
Moja kati ya matatizo makubwa ya muungano ni hali ya muungano wenyewe kutofahamika vyema kwa wananchi. Hivi huu muungano kwa nini unakuwa kama wa siri hivi? mengi hayajulikani kuhusu muungano, hata waziri mwenyewe alipochanganywa na Tundu Lisu alikiri kuwa mambo mengine hayajui...(Hao unaowasema mie siwajui nawasoma tu kama wewe) ndo maana muungano utakufa, kama watu wakielimishwa vizuri wataelewa...na watatoa ushauri muungano uimarishwe vipi
 
Msikurupuke kusema uongo wakati jambo hili la ubaguzi linafanyika. Nina rafiki yangu mfanyabiashara Kariakoo, pia amefanya/anafanya biashara zake Pemba. Aliona shamba akataka kununua ili alime karafuu. Mwenye eneo alikubali, walipokwenda kwa Sheha ili waandikishiane Sheha akaleta kauzibe. Ukatokea mvutano kati ya Sheha na mwenye shamba. Ndipo Sheha akapasua, " Huyu mtu wa bara hawezi kununua ardhi huku kwetu wao wanamapori mengi". Hadi leo rafiki yangu hajapata eneo sehemu yoyote, si Unguja wala Pemba.

Kama haitoshi mwaka jana Novemba nilimwuuliza muunguja,"Hivi Unguja yote imejaa kiasi cha kwamba wazanzibari hawawezi kupata viwanja?" akasema "Haijajaa, viwanja na mashamba yapo. Watu mbona wanauziana kila uchao? Ni pesa yake mtu na maelewano na mwenye mali" Nikamuuliza "Na mimi naweza kupata nikiwa na hela ya kutosha?" Akajibu "Huwezi kupata." Nilipomdadisi zaidi kwanini siwezipata na yeye anawezakupata. Jibu lilikuwa, "Mbona wewe unatokea Bara, huwezi kupata." And I concluded on how racist are they.
Kichekesho hao Wazanzibari asili yao ni Huku bara sasa hayo ya kubagua ndugu zao nahisi itakua madhara ya utumwa na utamaduni wa kiarabu. Pole zao kwani asiye tambua na kuthamini utamaduni wake alikotoka ni mtumwa. Waendelee tu.
 
<br>
<br>
Kweli wako wazanzibari wenye asili ya bara... Lakini wanachokikataa wazanzibari ni utawala mbovu wa tz. Tanaganyika pamoja na rasilimali zote zilizopo hapa ,hii nchi imewashinda kuiongoza. Wazanzibari wanaweza kujikwamua kiuchumi kama watakua huru kufanya mambo yao wenyewe. Tanganyika isilazimishe kuwatawala watu wengine ,kwanza ijikwamue yenyewe katika janga hili la umasikini wa kujitakia.
Makosa aliyoyafanya Karume, hayatarudiwa tena na wanzanzibari wa leo.
 
Huu ni uongo uliokithiri na kushtadi.

Mfano mzuri ni maeneo ya Chake-Chake, Kusini, Pemba ambako Kanisa la Roman Catholic wanamiliki kiwanja na wamejenga kindergarten

Hapa hapa Chake-Chake, Kanisa la SDA wanamiliki kiwanja na wamejenga hospitali.

Unguja, maeneo ya Cheju, Kanisa la Roman Catholic wanajenga high school.

Lakini kubwa ni kwamba karibu mtaondoka, viwanja vya nini?

Nyie huku mje mlime tu mpaka "muungano" utakapo kata roho.
Kaka nakusaidia kidogo pia hio wamevunja katiba ya zanzbar,katiba yetu ya zanzibar hairuhusu mtu ambaye sio mzanzibari kumiliki ardhi hapa zanzibar,hii imekuja kwa sababu ardhi yetu sisi ni ndogo.

Na kama tungeruhusu kikatiba kuwa watanganyika wamiliki ardhi zanzibar tumeumia,wakija robo tu ya mkowa wa murogoro basi zanzibar is full,hatuna pa kukaa,sisi population yetu ni 1.2 milion,Watanganyika ni 41. something milion,jee mkija mkowa mmoja tu zanzibar kuhamia si vitabiruka viziwa kutokana na huo wingi wa watanganyika ? Sisi wazanzibar tutapata wapi pa kukaa na vizazi vyetu vijavyo ?

Ndio katiba yetu inavyosema na walifanya hivyo vizuri zaidi,watanganyika munavyo fahamu ni kuwa wazanzibari tulo kuja bara tunanufaika sio kweli,hapo wanaishi kama wageni ndugu zetu,wanalipa makodi,wanallipia majumba,wanalipia kila kitu kama wageni wengine wachina wakenya,wauganda.

Waache ukirindimba wa kisiasa,na ndio maana hatuutaki muungano kwa sababu hauna manufaa kwetu pia. Mmoja kumtawala mwenzi we hii hatuitaki.
 
Back
Top Bottom