Nd.wana jf. Nasikia ati ni marufuku kwa mtu kutoka bara (tanganyika) kumiliki aridhi,nyumba au jengo huko Zanzibar. Je ni kweli?
Kama jibu ni NDIYO. Kwa nini huku Tanganyika hatujawa na sera kama hiyo kwa wazanzibar?
Wazanzibar hawapaswi kumiliki ardhi huku Tanganyika. Kwani katiba inasemaje? Si kwamba mtanzania ana uhuru wa kuishi popote ndani ya Jamhuri ya Muungano. Kwa nini watanganyika hawamiliki aridhi kule?
=========
June 2012:
Kama jibu ni NDIYO. Kwa nini huku Tanganyika hatujawa na sera kama hiyo kwa wazanzibar?
Wazanzibar hawapaswi kumiliki ardhi huku Tanganyika. Kwani katiba inasemaje? Si kwamba mtanzania ana uhuru wa kuishi popote ndani ya Jamhuri ya Muungano. Kwa nini watanganyika hawamiliki aridhi kule?
=========
June 2012:
July 2013:ACTUALLY, NAANDIKA HII MADA KWA MAKUSUDI ILI TUJADILI...
Watz bara wanakatazwa kunujua ardhi kule visiwani, lakini wavisiwani wanaweza kununua ardhi kubwa kiasi wakipendacho hapa bara....swali langu ni, kuna haki hapo? pia, wazanzibari waliojenga bara (tukianza na mwinyi na familia yake wenye majumba mengi mikocheni na maeneo mengine dsm), wenye mashamba mengi hapa tz, siku muungano ukivunjika kama wazenji wanavyotaka, wataendelea kumiliki au ndo watavirudisha kwa wazanzibari...
Wapemba wenye maduka kila kona dsm watafungasha virago au watabadilisha kuwa wawekezaji kupitia kituo cha uwekezaji TIC.....wawe na mtaji si chini ya milioni 300 ambazo nina uhakika hawana......wataondoka wote kurudi makwao wakarundikane kwenye mitaa?...
Mbona viongozi kama mwinyi na wengine wamenyamaza kimyaaa, au ukivunjika wao wataomba uraia wa tz....
Wapendwa Watanzania wenzangu,
Zanzibar tangu enzi Dr Amani Karume alibadilisha katiba ili Watu wenye Asili ya Tanganyika wasimiliki Ardhi Zanzibar, badala yake wakodishwe na serikali kwa masharti ya uwekezaji sawa na wawekezaji we Nchi nyingine duniani.
Je, katiba ijayo itawarudishia Watanzania haki sawa? Au ndio na Wazanzibari walio wengi Tanganyika walipie kama kodi mahekalu, mashamba na Viwanda wanavyomiliki?
Ardhi si mali ya Muungano:
"Mwanasheria anena na JAMHURI"
"Sheria ya Ardhi ya Zanzibar ya mwaka 1992 hairuhusu mtu asiye Mzanzibari (wakiwamo Watanganyika) kumiliki ardhi Zanzibar."
Wazanzibari wanajidanganya kama wanakimbia kununua ardhi katika maeneo mbalimbali ya Tanganyika , kwani watapoteza fedha zao bure.
¡°Bila hata kubadili sheria ya sasa, kitakachobadilika katika sheria za ardhi Na. 4 na Na. 5 za mwaka 1999 ni jina kutoka Tanzania kwenda Tanganyika.
Sheria iko wazi, kuwa mtu ambaye si Mtanganyika ataruhusiwa kupewa ardhi ya Tanganyika iwapo tu anafanya kazi ya uwekezaji.
¡°Inatamka wazi kuwa ardhi ya Tanganyika si kwa ajili ya watu kuja kujenga makazi, bali uwekezaji. Hivyo kama kuna Mzanzibari anayejidanganya kuwa akinunua ardhi Tanganyika atajenga na kuishi hapa kama si mwekezaji anapoteza kuda na fedha zake.
Ardhi hiyo itachukuliwa na Rais wa Tanganyika bila kulipwa fidia. Wazanzibari wameyataka haya, lazima tuelezane ukweli mgumu,¡±
¡°Umiliki wa ardhi, haki za wenyeji na mipaka ya matumizi ya ardhi kwa wageni utawekwa wazi."
Na sasa wageni ni pamoja na Wazanzibari. Nasema Tanganyika wana haki ya kutunga sheria yao na wana haki ya kuweka mipaka kwa walio wageni.
¡°Wageni hawatapewa haki ya kumiliki ardhi ila watakuwa na haki ya kutumia ardhi. Zanzibar kilichowapa access (umiliki) wa ardhi ya Tanganyika awali ni kwa sababu sisi Tanzania Bara imo ndani ya Muungano. Itabidi Wazanzibari wajue kuwa nao ni wageni wakija Tanganyika."
¡°Tuliwatahadhalisha na tunaendelea kuwatahadharisha kuwa hata ukinunua ardhi Katiba ya Tanzania Bara (Tanganyika) itakuwa na haki ya kufuta umiliki wa ardhi."
"Mzanzibari atatumia ardhi kama mwekezaji ila si makazi, au kilimo cha kujikimu."
¡°Ni kama ambavyo Wakenya wanakuja wananunua ardhi na nyumba kumbe wanapoteza fedha zao, hata wakikimbilia kununua wanapoteza hela zao bure,¡±
Sheria ya Ardhi ya Zanzibar ya mwaka 1992 hairuhusu mtu asiye Mzanzibari (wakiwamo Watanganyika) kumiliki ardhi Zanzibar.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi, alipoulizwa na JAMHURI juu ya mshikemshike wa ardhi na kuhamishwa kwa makao makuu ya Serikali ya Tanzania kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam, alisema kwa ufupi, ¡°Mawazo haya yalikuwapo na yalizungumzwa, ila tusubiri wananchi ndiyo waamue.¡±
Tafsiri rahisi juu ya mabadiliko haya ina maana Wazanzibari waliojenga Tanganyika wanaokadiriwa kufikia 600,000 wanaweza kulazimika kurejea Zanzibar kwanza na kurudi Tanganyika baada ya kuomba, ama kibali cha ukaazi, au uwekezaji kupitia Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na kukubaliwa kupewa ardhi baada ya kutimiza masharti.
Moja ya masharti ya uwekezaji watakayopaswa kuyatimiza kupitia TIC ni kwamba lazima mwekezaji kama anataka kwenda kuwekeza Tanganyika awe na mtaji usiopungua dola 100,000 sawa na Sh milioni 160 za Tanzania ndipo apewe vibali vya kuishi. Wazanzibari wanaweza kutakiwa kutekeleza sharti hilo la kisheria.
JAMHURI