Hakuna Mtanganyika (mtanzania bara) Anayemiliki Ardhi/Nyumba Zanzibar

MTAZAMO tofauti miongoni mwa wabunge umeendelea kuwa chachu ya kutaka kuvunjwa kwa muungano wa Tanzania.Hali hii imejionyesha wazi wiki hii katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma baada ya wabunge kuvutana kuhusu hatima yake, huku baadhi yao wakitaka uvunjwe na kuundwa upya na wengine kuutetea.Chanzo cha mvutano huo ni kufutia baadhi ya wabunge kutoka Zanzibar kuubeza na kuonyesha wazi kuwa Tanzania bara inanufaika zaidi kuliko visiwani.

Hoja hii si tu kwamba iliwakoroga wabunge wa bara, bali pia wananchi walioisikia wamekuwa wakihoji sababu za wabunge hao kuubeza muungano kana kwamba hauwasaidii.

Kauli tata kuhusu muungano ambazo kwa ujumla zinadhoofisha uhusiano baina ya pande hizo mbili, ulianza muda mrefu hasa baada ya nchi kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya saisa na unaendelea kukua kadiri muda unavyosonga mbele huku Serikali ikifanya jitihada za kuunusuru.


Katika mvutano ulioibika bungeni wiki hii, wabunge wa Chadema na baadhi wa Chama cha Wananchi (CUF), walioonekana dhahiri kutaka muundo wa sasa wa Muungano huo uvunjwe na kuundwa mwingine wenye serikali tatu; Tanganyika, Zanzibar na Serikali ya Muungano.

Hata hivyo, mfumo huo umekuwa ukipingwa kila mara kwa vile ni sawa na kumwondole madaraka na nguvu Rais wa shirikisho kwa vile hatakuwa na uwezo kuingilia mambo ya ndani ya serikali ya mbili zitakaozoundwa.

Hata hivyo, wakati wabunge hao wakitetea hoja hiyo, wengine kutoka Chama tawala CCM, na baadhi ya mawaziri akiwamo Samuel Sitta wa Afrika Mashairiki, walisimama kudete kuutetea.

Hoja za wabunge
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alishutumu tabia ya viongozi waliopo madarakani kuficha ukweli juu ya suala zima la muungano akiweka bayana kuwa sasa ni wakati mwafaka Watanzania wakajadili hatima ya Muungano huo.

Akitumia vitabu vya watu mashuhuri kama vile Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe na Profesa Issa Shivji, Lisu
alisema matatizo na kero nyingi zinatokana na baadhi ya mambo kutowekwa wazi.

Alitaja baadhi ya mambo aliyosema siri kuwa ni juu ya Mapinduzi ya Zanzibar na lengo hasa lililolazimu uwepo wa muungano huo.

Mambo mengine alisema ni kuingizwa kinyemela kwenye katika ya Tanzania vipengele kuanzia cha 11 hadi 22.

Halima Mdee wa Kawe, alisema kero za muungano zimekuwa hazitatuliwi kutokana na waziri mwenye mamlaka ya muungano kupuuzwa na viongozi wenye mamlaka ya juu katika kuamua kusu suala hilo.

Aliwataja viongozi hao ambao alidai hawana muda wa kutulia ili kutafuta ufumbuzi wa kero hizo kutokana na kuwa na kazi nyingi kuwa ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Alilalamika kuwa kutokana na hali hiyo ni kero sita tu zimetatuliwa, huku saba ambazo ni za msingi, zikiendelea kupigwa danadana.

Miongoni mwa kero hizo sugu, alizitaja kuwa ni suala la mafuta, ushiriki wa Afrika Mashariki na suala sahihi za waanzilishi wa Muungano huo.

"Suala la kodi mbili ni kiini macho na kwamba wananchi wengi wamekuwa wakiathirika kutokana na tatizo hilo," alieza Mdee ambaye alipendekeza Katiba ijayo kuwa na mwanga wa kutatua kero za muungano.

Mohamed Amour Chomboh (Magomeni) alitamba kuwa yeye ni miongoni mwa watu wachache walioshuhudia Mapinduzi ya Zanzibar yalivyofanyika na anatambua ni muhimu kuenziwa.

Alisema anaona kuna umuhimu wa muungano huo kuendelea kudumu lakini, akaasa kuwa kero zake zimekuwa ni tishio kubwa hasa kwa maslahi ya Zanzibar.

Alilalamikia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwa ndio moja ya kero ambazo zinaweza kusababisha Wazanzibari waje juu na hata kutaka kuvunja Muungano.

Alisema Zanzibar inategemea zaidi bishara kwa ajili ya kuimarisha uchumi wake na kwamba TRA ndiyo imekuwa ikisababisha biashara kudorora visiwani humo.

Waziri atwishwa mzigo
Jaddi Sumail Jaddi (Mkwajuni-CCM) alisema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Hassan Suluhu ,ambaye ni Mzanzibar alikabidhiwa nafasi hiyo kama mtego wa kumbebesha lawama za kero za Muungano ambazo zinalalamikiwa na Wazanzibar.

"Ndugu yangu Samia ni mchawi aliyepewa mtoto amlee akimnyonga, alamumiwe yeye," alisema Jaddi.
Sitta alisema huo ni upotoshaji na kwamba alipewa kazi hiyo kwa vile Serikali inaamini kwamba ana uwezo wa kuifanya kazi hiyo.

Yalikuwepo malalamiko kwamba Wazanzibar wanaoajiriwa Bara ni wachache, lakini Sitta alipinga akitoa mfano wa wizara yake ina maofisa wakuu wa idara 12 na kati ya hao, wanne ni Wazanzibari.

Sitta awatuliza
Munkali wa wabunge hao ni kama ulizimwa na
Sitta ambaye alifanikiwa kubadili kabisa hali ya hewa iliyokuwa inaashirikia kuwa wabunge wengi wanataka Mungano huo uvunjwe.

Akichangia mjadala huo Sitta alisema siku ambayo Watanzania wataamua kuwa na serikali tatu za muungano, itakuwa ndiyo tiketi ya kuuvunja muungano huo.

"Kuunda tena Tanganyika ni kutengeneza mbia mwingine atakayekuwa anashindana na Zanzibar," alisema Sitta.

Alifafanua kuwa hali hiyo itajenga mazingira ya mvutano kwa serikali ya Tanganyika na Zanzibar wa kila mmoja kupigania maslahi yake na Serikali ya Muungano haitakuwa na nguvu kwa sababu uwepo wake utategemea pande hizo mbili.

Alitoa mfano akisema linaweza kujitokeza suala la kuchangia uendeshaji wa Serikali ya Muungano na hapo yanaweza kujitokeza malalamiko kwamba pande zote zigharimie sawa kwa sawa na hapa Zanzibar ndiyo itakayonyanyasika.

Sitta ambaye alikuwa Spika katika Bunge lililopita alionya akisema kama ni mpango wa kuunda serikali tatu ni bora waridhie kabisa muungano usiwepo na serikali zote zijitegemee.

Alitaka ieleweke kwamba wakati inaonekana kuwa Wazanzibar ndio wanaoonekana kulalamika sana wakati huu kwamba wananyimwa maslahi yao lakini ukweli wapo Watanzania Bara ambao nao wanalalamika vivyo hivyo ila nguvu hiyo inapungua kutokana na kuwepo serikali mbili.

Amtetea Nyerere
Kuhusu Baba wa Taifa kuwa dikteta, Sitta alisema kuwa huo ni upuuzi kwa sababu yapo matendo mengi ambayo yanaonyesha hakuwa mlafi wa madaraka na badala yake alipenda haki kwa wananchi wake na bara la Afrika kwa Ujumla.

Alitoa mfano kuwa kama angekuwa dikteta angeweza kuamua kufuta kabisa uwepo wa serikali ya Zanzibar.
"Lakini alikubali iendelee kuwepo serikali ya Zanzibar ndani ya Muungano," alisema Sitta ambaye pia ni mbunge wa Urambo Mashariki.

Katika kuelezea kuwa Karume hakuwa mtu wa kuburuzwa alisema, Tanzania ilipoishiwa akiba ya fedha za kigeni na kwenda kuiomba serikali ya Zanzibar iwapatie kwa sababu wao walikuwa nazo nyingi kutokana na mauzo ya karafuu, alikataa.

Kuhusu suala la picha ya siku ya Muungano kuonekana Mwalimu Nyerere peke yake akichanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar, Sitta alisema ni suala tu la heshima ambalo alipewa kutokana na wadhifa wake wa Rais wa Muungano.

Alifafanua kuwa siku hiyo waliteuliwa watu wawili, mwanauma na Mwanamke, kutoka pande zote kushiriki katika kufanikisha tukio hilo lililoandika historia ya Tanzania.

Hoja nyingine aliyopangua ni ile ya wabunge wengi kueleza kuwa katiba ilibadilishwa ili Rais wa Zanzibar asiwe tene Makamu wa Kwanza wa Rais tofauti na makubaliano ya waasisi wa muungano kwa hofu ya CCM kwamba Rais wa visiwani anaweza kutoka chama cha upinzani.

Sitta alisema ukweli ni kwamba mabadiliko hayo yalitokea baada ya kuona kwamba nafasi hiyo ya pili itaonekana kuwa ni ya Wazanzibari tu, kwa vile serikali ya Zanzibar daima itaongozwa na mzanzibar.

Zanzibar na OIC
Kuhusu suala la kutaka Zanzibar iruhusiwe ijiunge na Jumuia ya Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) kwa vile Tanzania imeamua kutofanya hivyo, Sitta alisema tatizo ni kwamba kanuni haziruhusu.

Alisema kwamba OIC ilikataa kufanya hivyo kwa vile sheria zao ni kujenga ushirikiano na serikali ile inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Kuhusu kipengele cha kwanza hadi 11 viliundwa kwa makubaliano ya pande zote lakini baadaye kifungu cha 12 hadi 22 vikaingizwa kinyemela, Sitta alisema, sio kweli.


Kwa mujibu wa Sitta vipengele hivyo vilitokana na kuvunjika kwa Jumuia ya Afrika Mashariki 1977 ambapo baadhi ya mambo mengi yaliyokuwa yanasimamiwa na ushirikiano huo yalibaki bila usimamizi.

Alitaja miongoni kuwa ni Shirika la Posta, reli, bandari na ndege ambapo Tanzania Bara ilibidi iyabebe baada ya rais wa Zanzibar kuridhia.

Hata hivyo alisema Tanzania bara ilibeba jukumu hilo kwa gharamna zake bila kuishirikisha Zanzibar hiyo ikawa ni nafuu kwa Wazanzibar kwa sababu faida zake zinaenda pande zote za Muungano.

Kama hiyo haitoshi, Sitta alisema rais wa Zanzibar aliiomba Bara ianzishe pia elimu ya juu kwa sababu isingeweza kufanya hivyo kutokana na uwezo wa kifedha.

Akipinga malalamiko kwamba Zanzibar haina uwakilishi kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC), Sitta alisema katika vikao vyote vya majadiliano visiwa hivyo vimekuwa na uwakilishi.

Isitoshe akasema kuwa katika kuthamini Zanzbar, EAC inajiandaa kuwekza katika miradi mitatu visiwani humo ambayo ni ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa Pemba, ujenzi wa Bandari ya Maruhubi na chelezo ya kusafirisha mizigo na magari Zanzibar, Mombasa na Dar es Salaam.
 
Sio kweli.Mi nawafaham watanganyika(wabara) kibao wananyumba zenji.wengine wakiwepo ndugu na jamaa zangu wakaribu,zaidi ya hayo wapo wabara wamejenga hadi shule na wanaiendesha till today.kwahiyo ni mtazamo tu kwasababu zanzabar ni ndogo na wengi wao ni wanzanzbr wenyewe,lakini wabara wapo,na hawakatazwi kwa chochote'
 
Ardhi kubwa ni bora kuliko ardhi ndogo, inakuwaje binadamu anang'ang'ania ardhi ndogo wakati ana wasaa mkubwa katika ardhi kubwa?, mfano ungejisikiaje ungekuwa huru kwenda kuishi mahali popote duniani na kujitafutia riziki bila ya vikwazo vya viza na sheria za ukaazi za mahala hapo?, ndiyo maana mimi naona wanaotaka kujitenga wanaangalia pafupi, laiti wangeangalia mbele miaka 50, 100 ijayo wangeona ni bora kuwa wamoja katika nchi kubwa, kuliko kutengana.
 
'The man shall rise from the hills and save the people at their hour of need'.Kukiwa na mgombea Urais atakayesema atavunja Muungano kura yangu anayo hata kama ni Fisadi kama EL, nitamchagua tu kuondoa hii kero ya miaka mingi. Ee Mwenyezi Mungu inua kiongozi thabiti atakayefanya maamuzi magumu ambayo wengine wameshindwa.
Amen !
 
Msikurupuke kusema uongo wakati jambo hili la ubaguzi linafanyika. Nina rafiki yangu mfanyabiashara Kariakoo, pia amefanya/anafanya biashara zake Pemba. Aliona shamba akataka kununua ili alime karafuu. Mwenye eneo alikubali, walipokwenda kwa Sheha ili waandikishiane Sheha akaleta kauzibe. Ukatokea mvutano kati ya Sheha na mwenye shamba. Ndipo Sheha akapasua, " Huyu mtu wa bara hawezi kununua ardhi huku kwetu wao wanamapori mengi". Hadi leo rafiki yangu hajapata eneo sehemu yoyote, si Unguja wala Pemba.

Kama haitoshi mwaka jana Novemba nilimwuuliza muunguja,"Hivi Unguja yote imejaa kiasi cha kwamba wazanzibari hawawezi kupata viwanja?" akasema "Haijajaa, viwanja na mashamba yapo. Watu mbona wanauziana kila uchao? Ni pesa yake mtu na maelewano na mwenye mali" Nikamuuliza "Na mimi naweza kupata nikiwa na hela ya kutosha?" Akajibu "Huwezi kupata." Nilipomdadisi zaidi kwanini siwezipata na yeye anawezakupata. Jibu lilikuwa, "Mbona wewe unatokea Bara, huwezi kupata." And I concluded on how racist are they.

Hoja hii nimeileta sio kama mkurupukaji. Miaka ya nyuma Mch. Mtikira alilisema hili akitetea 'utanganyika'. Serikali ya Muungano wala ile ya SMZ hawakuwahi kukkanusha madai ya Mch. Mtikira.

Miaka takribani minne au mitatu iliyopita magazeti yaliripoti kesi ya mirathi huko Zanzibar. Katika shauri hilo mjane (ambaye ni mchagga) alizuiliwa kumiliki nyumba ya marehemu mumewe kwa kuwa yeye ni mtanganyika. Alishauriwa kwamba labda aiuze nyumba ile kwa mzanzibar na yeye atimwue zake kwao tanganyika.

Katika suala hili hata sharia za ndoa za kiislam zilibakwa na kufichwa.

Na madai kwamba RC,SDA, TAG nk wanamiliki aridhi na kujenga huko Zanzibar halina mashiko. Kanisa lilikuwepo Zanzibar toka enzi za usultani. Kwa hiyo,kubaguliwa kwa kanisa huko Zanzibar kumeibuka baada ya mapinduzi.

Aidha, makanisa hayawakirishi utanganyika ama watanganyika. Zanzibar pia ina raia wakristo japo kwa uchache. Kwa hiyo, kuwepo kwa makanisa huko ni kwa ajiri ya wazanzibar na sio watanganyika.

Kimantiki, kama ni kweli kwamba raia wa tanzania bara hawamiliki aridhi wala majengo huko zanzibar ninapata wasi wasi kwamba katiba imevunjwa. Na kama katiba inayosimamia Jamhuri ya Muungano imekiukwa na upande mmoja wa muungano. MUUNGANO HUO HAUPOOO!
 
Sidhani kama ni kweli. Mabagala Senior ana ardhi ya kutosha tu huko visiwani! Lakini yeye yupo huko tangu 1978, ina maana si mzanzibari?
 
Huu ni uongo uliokithiri na kushtadi.

Mfano mzuri ni maeneo ya Chake-Chake, Kusini, Pemba ambako Kanisa la Roman Catholic wanamiliki kiwanja na wamejenga kindergarten

Hapa hapa Chake-Chake, Kanisa la SDA wanamiliki kiwanja na wamejenga hospitali.

Unguja, maeneo ya Cheju, Kanisa la Roman Catholic wanajenga high school.

Lakini kubwa ni kwamba karibu mtaondoka, viwanja vya nini?

Nyie huku mje mlime tu mpaka "muungano" utakapo kata roho.

Sijakurupuka katika kuileta hoja hii jamvini. Miaka kadhaa iliyopita Mch. Mtikira aliwahi sema watanganyika hawaruhusiwi kumiliki aridhi wala nyumba huko Zanzibar. Aliyasema hayo akitetea uwepo wa serikali ya Tanganyika. Si serikali ya Muungano wala ile ya SMZ iliyokanusha madai ya Mch. Mtikira.

Aidha, miaka takribani, minne iliyopita magazeti yaliripoti juu ya mwanamke mmoja mjane (mchagga) aliyekuwa ameolewa huko Zanzibar. Mjane huyo alikataliwa kumiliki nyumba ya marehemu mumewe kwa kuwa alikuwa mtanganyika. Katika sual hili la mirathi hata sharia za kiislam za kislam kuhusu ndoa na mirathi zilibakwa na kufujwa.(mjane na marehemu wote walikuwa waislamu)

Kwa makanisa ya SDA, TAG, RC, KKKT nk kumiliki aridhi huko Zanzibar halina mashiko katika hoja hii. Makanisa sio watanganyika na wala hayawakirishi watanganyika.

Aidha, makanisa yalikuwepo huko Zanzibar tangu enzi za usultan wa waaraabu. Ubaguzi dhidi ya watanganyika labda ummeanzishwa huko baada ya Muungano.

Na makanisa yaliyotajwa yapo kwa ajili ya wazanzibar wakristo japo ni wachache.
 
Huu ni uongo uliokithiri na kushtadi.

Mfano mzuri ni maeneo ya Chake-Chake, Kusini, Pemba ambako Kanisa la Roman Catholic wanamiliki kiwanja na wamejenga kindergarten

Hapa hapa Chake-Chake, Kanisa la SDA wanamiliki kiwanja na wamejenga hospitali.

Unguja, maeneo ya Cheju, Kanisa la Roman Catholic wanajenga high school.

Lakini kubwa ni kwamba karibu mtaondoka, viwanja vya nini?

Nyie huku mje mlime tu mpaka "muungano" utakapo kata roho.

I hate your gut!
 
Nd.wana jf. Nasikia ati ni marufuku kwa mtu kutoka bara (tanganyika) kumiliki aridhi,nyumba au jengo huko Zanzibar. Je ni kweli?
Kama jibu ni NDIYO. Kwa nini huku Tanganyika hatujawa na sera kama hiyo kwa wazanzibar?

Wazanzibar hawapaswi kumiliki ardhi huku Tanganyika. Kwani katiba inasemaje? Si kwamba mtanzania ana uhuru wa kuishi popote ndani ya Jamhuri ya Muungano. Kwa nini watanganyika hawamiliki aridhi kule?


Tanganyika iko wapi? Rais wake nani?
 
Mi Msambaa pyua mbona nna kiwanja FUONI kule Zanzibar? na naendelea na ujenzi vizuri tu!
 
Mtikila anajulikana kuwa ni mzushi na mfitinishaji. During the First Multi Party Elections in 1995 alikuwa anawazungumzia MAGABACHORI; leo imekwisha issue ya MAGABACHORI; he has cashed in. He is cheap and has controversial views. I would not view any issue he utters as credible.

La Msingi; iwekwe sera ya Ardhi ya Zanzibar hapa Jamvini.


Sijakurupuka katika kuileta hoja hii jamvini. Miaka kadhaa iliyopita Mch. Mtikira aliwahi sema watanganyika hawaruhusiwi kumiliki aridhi wala nyumba huko Zanzibar. Aliyasema hayo akitetea uwepo wa serikali ya Tanganyika. Si serikali ya Muungano wala ile ya SMZ iliyokanusha madai ya Mch. Mtikira.

Aidha, miaka takribani, minne iliyopita magazeti yaliripoti juu ya mwanamke mmoja mjane (mchagga) aliyekuwa ameolewa huko Zanzibar. Mjane huyo alikataliwa kumiliki nyumba ya marehemu mumewe kwa kuwa alikuwa mtanganyika. Katika sual hili la mirathi hata sharia za kiislam za kislam kuhusu ndoa na mirathi zilibakwa na kufujwa.(mjane na marehemu wote walikuwa waislamu)

Kwa makanisa ya SDA, TAG, RC, KKKT nk kumiliki aridhi huko Zanzibar halina mashiko katika hoja hii. Makanisa sio watanganyika na wala hayawakirishi watanganyika.

Aidha, makanisa yalikuwepo huko Zanzibar tangu enzi za usultan wa waaraabu. Ubaguzi dhidi ya watanganyika labda ummeanzishwa huko baada ya Muungano.

Na makanisa yaliyotajwa yapo kwa ajili ya wazanzibar wakristo japo ni wachache.
 
Nimeisoma habari iloandikwa hapo juu na nd. Ghibuu imenishangaza sana hasa kipande kilichosema kwamba:- Katika mvutano ulioibika bungeni wiki hii, wabunge wa Chadema na baadhi wa Chama cha Wananchi (CUF), walioonekana dhahiri kutaka muundo wa sasa wa Muungano huo uvunjwe na kuundwa mwingine wenye serikali tatu; Tanganyika, Zanzibar na Serikali ya Muungano.
Hata hivyo, mfumo huo umekuwa ukipingwa kila mara kwa vile ni sawa na kumwondole madaraka na nguvu Rais wa shirikisho kwa vile hatakuwa na uwezo kuingilia mambo ya ndani ya serikali ya mbili zitakaozoundwa.

Hapa hakuna ukweli kabisa (in bold) na sijui mwandishi anajua alichokiandika au kweli ndiyo mawazo ya wabunge. Hivi kweli hawa wabunge hawatazami nguvu ya marais kama Obama na hata waziri mkuu wa Uingereza? Nguvu gani ya kitaifa ambayo rais anaihitaji ikiwa huyo JK au kiongozi mwingine yeyote toka tupate Uhuru hana muda wa kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja. Ni vigumu sana kupanga maendeleo ya nchi mbili kwa mfumo uliopo laabila kuitreat Zanzibar kama mkoa.

Sii kweli kabisa kwamba rais wa Jamhuri atapoteza nguvu zake bali itampa nafasi kubwa ya kutazama maswala makubwa kwa ujumla wake isipokuwa tu kabla ya kuweka serikali tatu ni muhimu kufahamu kwamba haiwezekani upande mmoja ukawa na maamuzi tofauti na upande wa pili ktk baadhi ya maswala ya Kitaifa. After all kupoteza nguvu kwa rais kunahusiana vipi na kupoteza uwezo wake wa kufanikiwa kuleta maendeleo maanake ndio dhamira ya msingi.

Na labda ningewaomba wakuu wa serikali yetu watume ujumbe kwa serikali ya Canada kuomba kuja kujifunza jinsi ya kuunda serikali mbili chini ya serikili kuu kama wanavyofanya wao. Canada pia bado kuna matatizo kama yetu hasa Quebec ambao wanadai kutambuliwa kama a distincty society kama ilivyo Zanzibar. Na wenzetu Quebec ni mwanachama wa jumuiya ya nchi za Kifaransa hali the rest of Canada hawaafiki na wala hawana mahusiano, Pia ingawa Taifa zima ipo chini ya Malkia ingawa Quebec hawaafiki.

Kwa mtazamo huo Tanzania ni member wa jumuiya ya Commonwealth lakini Zanzibar ilokuwa ikitawaliwa na Sultan wa Oman (Quebec na France)hivyo kuna kufanana sana ktk hatua za uasilia wetu. Ni vizuri sana kujifunza toka kwa wenzetu kisha tunatazama WATU na MAZINGIRA yetu yapi yatatufaa na yapi itabidi tuyaache lakini swala la serikali tatu halina mjadala.. Na pengine nikitumia maneno ya Lowassa, huu ndio mjadala ambao viongozi wetu wanatakiwa kuchukua maamuzi magumu kuliko kuacha ilivyo kwani itafikia wakati Wabara na Wazanzibar watachoka na hizi chokonoa chokonoa wakaanza kutiana vidole vya macho.

Cha ajabu kabisa ni pale viongozi wa CCM wanapokazania kwamba Zanzibar haiwezi kujikimu bila Bara ambao wanalipia gharama nyingi za visiwani. maneno haya tu yanatia hasira pande zote. Kwa bara inawashinda kuelewa kwa nini kodi zao zitumiwe kuwanusuru Zanzibar hali huku bara kwenyewe hakuna unafuu wowote wa kimaisha. na zanzibar ni matusi kuwalaghai ktk Muungano kwa sababu ya Fedha! Zanzibar haikuungana na bara kwa sababu hawana rasilimali za kuwawezesha kimaisha! haya ni matusi.

Mimi ningependa sana mtu aje hapa anieleze hatari ya kuwepo na serikali tatu! anipe historia au mifano mibaya ilowahi kutokea maanake nijuavyo mimi haya maswala ya kung'ang'aniza serikali kuu kuchukua madaraka yote ya kiutawala ndio yaliyoibomoa Russia, Yugoslavia, Ethiopia, Somalia na sasa Sudan ingawa mimi naamini kabisa kwamba kulikuwepo na mkono wa sheitan sehemu zote (US), lakini hata hivyo ni malalamishi madogo madogo kama haya hupelekea uhasama baina ya watu wakati ingewezekana kabisa sehemu hizo kupewa dhamana ya kupanga maendeleo yao kutokana na kodi zao na kama watashindwa kuendelea watambana mtu wao zaidi ya kiongozi wa Kitaifa ambaye kwa ujumla ndiye mwenye mamlaka makubwa.


Mfumo uliopo hata Kitaifa haufai kabisa! Haiwezekani mkoa uloshikwa na CUF au CDM upewe RC au DC wa chama kilichoshindwa tena kwa kuteuliwa na rais! Huyu ataweza vipi kukubaliana na sera,ilani za chama kingine zitumike mkoani au wilayani kwake hali yeye ndiye kiongozi!. Ni ktk hali hiyo hiyo inatatanisha ktk Muungano na wengi tunashindwa kutazama upande wa Zanzibar kwa sababu JK au niseme huyu RC ni wetu kutoka bara. Na hakika ukimuuliza mwanaCCM kwa nini tuna RC/DC ktk mkoa/wilaya ambayo CUF wameshinda (Pemba) watakwambia tumeshika hatamu na hakuna ubaya!
 
kule huwa twatimuliwa, wazenji hawapo kimuungano kabisa, machoni mwao ni kama vile watanganyika ndio maadui zao. Nashangaa wajapo kwetu humiliki mali na majumba ya gharama, viwanja na maduka makubwa! They are more selfish!
 
Back
Top Bottom