Hakuna mtakatifu miongoni mwetu

Dr criminal

JF-Expert Member
May 16, 2022
2,278
4,270
Ukiwakuta wanaume utawaskia wanasema,,,

"Mwanamke unampa pesa, show Kali na mda wa kutosha mwisho wa siku anaenda kuliwa na boda"

"Mwanamke mnaweza Kuta mmezaa watoto watano, pale angalau wawili sio wako"

"Mwanamke hatongozwi mara mbili, wale ma-ex wake watakuja tu wamle"

"wanawake wa siku hizi kuomba omba hela kama mayatima"

"Mwanamke ndio kiumbe cha kuogopwa zaidi duniani, unaweza ishi na mkeo nyumba ya kupanga unalipa Kodi Kila mwezi mwisho wa siku unakuja kugundua nyumba ni huyo mke wako"

"Wanawake wabinafsi sanaaaa"

"Mwajuma yule malaya wa kutupwa mtaa mzima huu wamepita naye"

"Wanawake hawana haya hata kidogo, wanajiuza ndio waishi"

Ukiwakuta wanawake utawaskia wanasema...

"Wanaume wote mbwa"

"Wanaume wote ndo wale wale tu, ataku-care akiichakata tu humuoni"

"Hakunaga mwanaume mwenye mwanamke mmoja"

"Wanaume wakatili sana, mtu mnafanya mapenzi mnarekodi video Kwa mapenzi yenu mwisho wa siku anazivujisha"

"Mwanaume atakutumia wewe neema ataenda kumuoa mwajuma"

"Mwanaume kama hakupi hela hakupendi huyo"

"Wanaume wengi waliopo kwenye ndo wana watoto uko nje"

Come on guys!!!!!!!!!!!!

Tuache kutupiana mipira jamani, swala ni...

1.Kuna wanaume wa hovyoooo

2.Kuna wanawake wa hovyoooo,,full stop.

Lakini ukweli ni kwamba leo hii asilimia kubwa ya watu Kwa ujumla wetu ni watu wa hovyoooooo..

Kwahiyo tuache mbambamba, Kuna wanawake ni washenzi yaani ni washenzu mpaka shetani haoni ndani, lakini kuna wanawake ni watulivu, wastaarabu, waelewa, wanyenyekevu, wasemehevu, wasikivu mithili ya malaika.

Vivyo hivyo Kuna wanaume ni nyoko, yani ni nyoko, nyoko nyoko kweli, mtu amepinda hana sijui cha utu, ustaarabu, ubinadam, wala huruma, lakini wanaume wengine kwanza wanajitambua, wanatimiza majukum yao, wana-care, wana huruma, upendo na Kila sifa njema ya kuwa baba wa familia au mpenzi wa mtu.

Tuache hii tabia ya kujifanya jinsia moja ni safi, au takatifu sana ukilinganisha na jinsia nyingine, ni tabia ya mtu mwenyewe (myao mmoja aliulizwa, kwann nyie kwenye "m" mnatamka"n" mnapoongea, akajibu "Hapana, sio wote, Kuna ntu na ntu wake), kwahiyo Kuna ntu na ntu wake jamani, Kila jinsia ina uchafu wake na mazuri yake ambayo ni tabia ya mtu mmoja mmoja.

WANAUME WOTE MBWA
WANAWAKE WOTE MALAYA

#KunaNtuNaNtuWake
Dr Criminal.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuuh thread Haina comment Ina ukungu mwingi acha niipe
JamiiForums2146844703.jpg
 
Back
Top Bottom