Hakuna mama mkwe anaempenda mkwe wake 100%

Tatizo huwa linaanza wakikaa pamoja hata wiki tu. Kama mmoja wao anachonga ngenga sana lazma watibuane.

Kikubwa ni wakae mbali mbali kila mtu aishi na familia yake.
 
Kuna situation nyingine inalazimu kukaa nyumba moja. Pengine mzee alishafariki, na wewe ndiye mtoto wa kiume pekee na mama mgonjwa. Wote ni muhimu kwako.

Ni kuvumilia tu.
 
Mi nadhan sisi wadada tunaoolewa ndo tuna matatizo kuweka negative perspective kwa wamama wa waume zetu/mawifi/mashemeji na hii nadhan inatokana na kukaririshwa na jamii inayotuzunguka kiasi unakuta mtu anajiandaa kabisa kutoa negative reaction kwa huo upande lengwa...tunawapa wakat mgumu sana waume zetu kutengeneza balance ya upendo na wengi wao maamuzi yao ni kuhama kukaa mbali na wazazi wao.. lakini wengi wetu hatujawahi na hatujiulizi sisi hatuna wazazi?? Hawatukwazi??

Hawatuendeshi?? tulishawahi kutaka kuwakimbia??.. kama uliweza Kum tolerate mzazi wako why not mzazi wa mwenzio mnaeshare nae kitanda kimoja kwa shida na raha!!tujue kabisa huyo unaemuona mume wako ni mtoto wa mwenzako umekutana nae akiwa na meno 32,amelelewa kuna wamama wengine wamesacrifice a half of their youth age ili kutengeneza huyo responsible man unaemwita mume wangu kwa shida na tabu..

Bas usimbane 24/7 hebu mpe muda wa Ku spend na mama ake bila ya wewe kuwepo, bi mkubwa ajielezee wee mpaka hamu imuishee.. af uone kama kutakuwa na troubles... Shida ni moja tu wakaka mkishaoa hamna mda wa kukaa na mama zenu wawadekee na kuwaeleza shida zao private mda wote ukitoka kazin umekula zaidi ya shkamoo mama upo ndan na mkeo kwanini wazazi wenu wasiseme wamemwagiwa maji ya moto ili angalau kupata ile attention yenu.. hiv hamjui mtoto wa kiume akishakuwa mkubwa anakuwa like a second husband to his mum hebu wakaka zetu mjitahidi angalau kwa wiki mara moja mjitengee ka muda ka kukaa private na mama zenu ati ha ha haaaa
 
Watu wa mkoa wa Mara kwa magomvi. Hamuachagi
Hakuna pa mahali wote hawatupendi sisi wakwe zao.
Mimi namama mkwe ni paka na panya,simba na fisi.
Yaani mtoto wake humuwezi akiwepo mama yake ila baba yake akiwepo ninafuu.
Kwenye ndoa toaga mahali wote wapo tu sawa.
 
Mi nadhan sisi wadada tunaoolewa ndo tuna matatizo kuweka negative perspective kwa wamama wa waume zetu/mawifi/mashemeji na hii nadhan inatokana na kukaririshwa na jamii inayotuzunguka kiasi unakuta mtu anajiandaa kabisa kutoa negative reaction kwa huo upande lengwa...tunawapa wakat mgumu sana waume zetu ku
Nimeshafanya hivyooo vyote.
Zawadi
Kumpa upendo kuwaletea wajukuuu.
Kumsaidi shughuli za nyumbani ila tatizo anawivu .
Anaona unamnyima haki ya kukaa na mtoto wake.
 
Vipi mama wa mwanamke nae kumpenda Mme wa mwanae sababu hapo umeongelea tu upande wa mama mzaa mume wa mtu.
 
Nimeshafanya hivyooo vyote.
Zawadi
Kumpa upendo kuwaletea wajukuuu.
Kumsaidi shughuli za nyumbani ila tatizo anawivu .
Anaona unamnyima haki ya kukaa na mtoto wake.
Hilo ndo analolitaka huo wema wako kwake anauona hauna maana if kama humpi nafasi ya kukaa chemba na mwanae.. kwan unaumia nini siku baba jairo akiwa nyumban ukatafta kasafari ka uongo na kweli ka masaa hata kumi ukawaacha wawili tu nyumban wapige story zao....ukijenga hayo mazoea wala hupati tabu...

Pili kila kituko sio cha kukibeba rohoni mengine ni ya kuyaacha yaende na mwendazake kila binadamu ana matatizo yake imagine angekuwa mama ako mzazi ungefanyaje?tusipende kuvibeba vitu ambacho tunajua kabisa hatuwez kuvitatua acha mda utatue wenyewe
 
hivi kwa nini huwa mnaoneana wivu?
Kwasababu kila mmoja ni mmiliki wa huyo mwanaume....
Mama - huyu ni mtoto wangu kipenzi
Dada- huyu ni kaka angu kipenzi
Mke- huyu ni mume wangu kipenzi i can't live without him

Sasa hapo unadhani kuna kupendana???
 
Mbona umebase upande mmoja? Hii hata kwa wanaume; mama mkwe si rahisi kumpenda mume wa mwanaye wa kike
 
Mkwe atakupenda endapo utakuwa unatuma 50k-100k kila mara, otherwise utanafikiwa tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom