KakaKiiza
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 11,587
- 8,622
Je kama mimi ni mwanachama nafanya sekta binafsi nimefukuzwa kazi na nipo kijiweni je mimi nitakuwa kundi gani??je na pesa yangu ndiyo itakaa huko hadi nifikishe miaka 55???au inakuwaje?Bargain,
Hii sio tetesi maana haijawa kama hivyo. Lakini umefanya vizuri kuleta hii habari katika kipindi hiki na kuwafanya waajiriwa wote Tanzania wakae mkao wa kula.
Ukweli ni kwamba serikali ina mpango wa kupeleka bungeni marekebisho ya muswada wa sheria wa mafao ya wafanyakazi kama ulivyopitisha ba bunge ili sasa kufanya wafanyakazi wote wanaokatwa akiba ya mafao (PPF,NNSF, PSPF,LAPF,GEPF n.k) kulazimika kutopata mafao yao kama hawajatimiza umri wa kustaafu(55-60).Mpango huu unaletwa kwa sababu serikali yenu haina namna ya kufanya na ingependa kupata boost ya mapato toka mifuko hii ili kuleta pesa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Mpango huu wa aibu na kandamizi utawaathiri wafanyakazi zaidi ya 700000 serikalini lakini kwa kipekee utaathiri na kuua ndoto za wafanyakazi zaidi ya 3000000 walio katika sekta binafsi kama vile makampuni, NGOs na wale waliojiajiri wenyewe na ambao wanatumia mifuko hii.
(Una imani kubwa kwamba wabunge wetu hasa wa upinzani wataupigia ngumu mpango huu nyonyaji ambao ni wa aina yake katika nchi zote za Afrika. Hii pia inatoa fursa kwa wafanyakazi wote nchini (hasa vijana) kutafakari na kuona jinsi serikali yenu inavyopanga kufifisha mipango yenu ya muda mfupi na ile ya kati. Kazi kwenu simameni na Chukueni Hatua Sasa.
HABARI NDO HIYO