Habari wana JF
Ni muda sasa, tangu mwezi wa sita hivi nimekuwa nikisikia kwamba Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuzuia wafanyakazi wa sector binafsi kuchukua NSSF zao mpaka wafikishe umri wa kustaafu uliowekwa na seerikali, like 60yrs.
nilisikia kwamba mpango huu ulikuwa uanze mwaka huu mwishoni, lakini ikashindikana kutokana na maandalizi kutokuwa yamekamilika vizuri.
Nimesikia tena leo mjadala huu ukiendelea kwenye forum moja ya watu wanaofanya kazi kampuni mmoja through outlook mails kwamba mpango huu utakuwa implemented kuanzia 1st march 2012 bila kukosa.
Nilisikia pia kupitia wana forum hao kwamba bunge lilipisha muswada huu na Rais kuusaini kinyemela tangu mwaka jana, kitu ambacho kinaniumiza kichwa, inakuwaje muswada nyeti kama huu upitishwe kwenye bunge hili la sasa la ushindani wa kisiasa na hoja zenye mantiki kutoka upinzani bila wanachi kufahamu.
mwenye uhakika na suala hili please naomba unifahamishe vizuri.
Itakuwa ni vizuri zaidi kama utaleta na official data kuleta uhakika zaidi.
Aksanteni.
Ufafanuzi Kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhitibi wa Hifadhi ya Jamii
Ni muda sasa, tangu mwezi wa sita hivi nimekuwa nikisikia kwamba Serikali ipo katika hatua za mwisho za kuzuia wafanyakazi wa sector binafsi kuchukua NSSF zao mpaka wafikishe umri wa kustaafu uliowekwa na seerikali, like 60yrs.
nilisikia kwamba mpango huu ulikuwa uanze mwaka huu mwishoni, lakini ikashindikana kutokana na maandalizi kutokuwa yamekamilika vizuri.
Nimesikia tena leo mjadala huu ukiendelea kwenye forum moja ya watu wanaofanya kazi kampuni mmoja through outlook mails kwamba mpango huu utakuwa implemented kuanzia 1st march 2012 bila kukosa.
Nilisikia pia kupitia wana forum hao kwamba bunge lilipisha muswada huu na Rais kuusaini kinyemela tangu mwaka jana, kitu ambacho kinaniumiza kichwa, inakuwaje muswada nyeti kama huu upitishwe kwenye bunge hili la sasa la ushindani wa kisiasa na hoja zenye mantiki kutoka upinzani bila wanachi kufahamu.
mwenye uhakika na suala hili please naomba unifahamishe vizuri.
Itakuwa ni vizuri zaidi kama utaleta na official data kuleta uhakika zaidi.
Aksanteni.
Na Hellen Mwango | 23rd July 2012
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), imesema kuanzia sasa mwanachama wa mfuko wowote hataruhusiwa kuchukua mafao yake kutokana na sababu yoyote mpaka hapo atakapofikisha miaka 55.
Hata hivyo, licha ya kuzuia fao la kujitoa na kutoruhusiwa kuchukua mafao yao, mwanachama wakiwamo wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) na Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma NSSF) atapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye sheria ya SSRA.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka, mabadiliko hayo yametokana na sheria za mamlaka hiyo kufanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge Aprili 13, mwaka huu na kwamba imeshasainiwa na Rais Jakaya Kikwete na imeanza kutumika rasmi.
Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo.
"Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi lakini kuanzia sasa mwanachama wa mfuko atapata mafao yake pale atakapofikisha umri wa kustaafu kwa hiari (55) au kwa lazima (60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu" ilisema taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na kufafanua kuwa:
"Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni.
Taarifa ya Mkurugenzi huyo iliendelea kusema kuwa mafao ya kujitoa yanapunguza na kuondoa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.
Hata hivyo, ilisema pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya madini yataendelea kutolewa kama kawaida ikiwemo kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu.
Ilisema wanachama wanatakiwa kuwa watulivu kuhusiana na mabadiliko hayo na kwamba maslahi yao yatalindwa na hakuna atakayepunjwa kutokana na utaratibu huo.
CHANZO: NIPASHE
Ufafanuzi Kutoka Mamlaka ya Usimamizi na Udhitibi wa Hifadhi ya Jamii
UFAFANUZI KUHUSU FAO LA KUJITOA KATIKA MAREKEBISHO YA SHERIA ZA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII.
Ufuatao ni ufafanuzi mfupi kuhusu marekebisho ya Sheria za Mifuko hasa kuhusu fao la kujitoa.
20 JULAI, 2012
1. Kama mtakumbuka Sheria za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii pamoja na Sheria ya Mamlaka zimefanyiwa marekebisho na kupitishwa na Bunge tarehe 13 Aprili, 2012. Sheria hiyo tayari imeshasaininiwa na Mheshimiwa Rais na imeanza kutumika rasmi. Marekebisho haya yanawahusu wafanyakazi wote nchini mwetu bila kubagua sekta yoyote ile.
2. Kwa mujibu wa marekebisho hayo fao la kujitoa (withdrawal benefits) yamefutwa na kuanzia sasa hayatakuwepo. Mafao hayo yalikuwa yanatolewa pale mwanachama alipokuwa anaacha kazi. Sasa mwanachama wa Mfuko atapata mafao yake pale atakopfikisha umri wa kustaafu kwa hiari (miaka 55) au kwa lazima (miaka 60) au pale anapopata ulemavu wa kudumu.
3. Kwa kuzuia fao la kujitoa mwanachama anapata fursa ya kupata mikopo ya nyumba kwa kutumia dhamana ya michango yake kama ilivyoelezwa kwenye Sheria ya SSRA kipengele cha 38.
4. Marekebisho hayo kuhusu kuzuia mafao ya kujitoa yamefanyika ili kutimiza lengo na madhumuni ya hifadhi ya jamii ambayo ni kuhakikisha kuwa mwanachama anapostaafu anapata mafao bora yatakayomwezesha kumudu maisha ya uzeeni wakati ambapo nguvu ya kufanya kazi tayari imeshamwishia.
Mafao ya kujitoa yanapunguza na hata kuondoa kabisa kinga ya mfanyakazi pale anapoumia kazini au anapofika uzeeni.
5. Tunawaomba muwaelimishe wafanyakazi umuhimu na madhumuni ya mafao ya hifadhi ya jamii. Hifadhi ya jamii ni nyenzo mahususi iliyowekwa kuwasaidia wafanyakazi kuendesha maisha yao wakati wanapokuwa wameishastaafu tayari. Umasikini wa kipato wakati wa uzee ni mojawapo ya changamoto ngumu kukabiliana nazo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Tunawasihi tena muelimishe wafanyakazi kuhusu jambo hili. Tafadhali msisite kuwasiliana na Mamlaka pale ufafanuzi zaidi utakapohitajika
6. Kwa kuwa marekebisho hayo yamesainiwa na kuanza kutumika rasmi kama sheria, mafao ya kujitoa hayawezi kutolewa tena na wafanyakazi watakaoacha kazi kwa sababu ya marekebisho ya kipengele hicho watakuwa hawajaijitendea haki wao wenyewe na pia itakuwa ni kunyume cha Sheria.
Mamlaka inaandaa kanuni za mafao ambayo lengo lake ni kuboresha maslahi ya wanachama, kanuni hizo zitajadiliwa na wadau wakiwemo vyama vya wafanyakazi na waajiri ili kupata maoni yao.
7. Tafadhali muwaelimishe wafanyakazi kwamba pamoja na kuzuia fao la kujitoa, mafao mengine ambayo ni muhimu kwa sekta ya Madini yataendelea kutolewa kama kawaida. Mafao hayo ni Kama vile kuumia kazini pamoja na fao la ulemavu
8. Tumesikia kwamba tayari kuna hofu imejijenga kwa wanachama kuhusiana na fao la kujitoa. Ikumbukwe kwamba baadhi ya Mifuko ilikuwa inatoa fao hilo kinyume cha Sheria kwani katika Sheria zao hakuna fao la kujitoa. Tunapenda kusisitiza kwamba wanachama wawe watulivu wakisubiri miongozo.
9. Tunapenda kuwahakikishia kwamba katika hili maslahi ya wanachama yatalindwa na hakuna mwanachama atakayepunjika kutokana na utaratibu huo.
Mamlaka imepanga kutembelea wafanyakazi wa sekta ya madini katika juma la kwanza la mwezi Agosti 2012 ili kutoa ufafanuzi zaidi kwa wanachama wote.
Tunatanguliza shukrani za dhati kwa ushirikiano.
Wenu.
Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii
Irene Isaka
MKURUGENZI MKUU