Hakuna kosa wala dhambi kumkumbuka Magufuli, aliiweza nchi, kwa sasa kuwa na uhakika wa mambo ya kesho, haijulikani

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,940
4,122
Ni ujinga kulazimishwa eti tusikumbuke uzuri wa ilivyokuwa awamu ya Magufuli

Ni ujinga kuendelea kutiana moyo kwamba, eti tupo pazuri na tunaelekea pazuri zaidi

hivi, Magufuli alitumia miujiza gani kwenye suala la Umeme na mgao kutokuwepo?

Yeye alifanyeje kumeneji suala la mlipuko wa bei za vyakula mbali na kuwa kwenye janga la Korona dunia nzima?

Alitumia mbinu gani kufanya nishati ya mafuta isipande na nauli kuwa juu, licha kwamba kipindi cha Korona meli nyingi zilipaki?

Sukari nayo imeshindikana sasa kushuka licha ya kuwa na kiwanda cha Bagamoyo sugar na kikubwa kulikoni vyote East Africa, sukari kg 4000 mpaka 4500, kweli???

Tunatafutana nini hapo?

kila mtu anayetokea mikoa ya mbali atakubaliana nami kwamba, kwa sasa suala na safari kutoka mkoa hadi mkoa, ni kama adhabu ya ndogo ya jehanamu

Kutoka kuwa na nauli ya tsh 70,000 kwenda Bukoba hadi 100,000+

Kutoka nauli ya 300 jijini Dar hadi 900 na 1100??

Halafu kuna mpuuzi mmoja anaendelea kusema ni sawa?

Kutoka kuwa na matibabu ziro kwa wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka 0 hadi 5, leo ni pesa??

Kutoka kuwa na umeme 27,000 wa REA hadi kutojulikana kama kuna REA au hakuna, maana bei ni ileile 310,000, bado kuna mjinga anaona ni sawa?

Tusikumkumbuke Magufuli kwa sababu ya wajinga wachache aliowatimua kazini?

Kwa sababu tu aliwadhibiti waliokuwa wanajilipa mapesa kupitia watumishi hewa?

Hao ndio watufanye tusisemee mazuri hayo kwa sababu ya matusi yao mitandaoni?

Mnataka tuwasifu kwenye lipi sasa ikiwa kila kitu kimepanda bei?

Watu hawalazimishwi kusifia, wafanyie mambo mazuri wakusifu, kwa sasa tusifu nini na tumsifie nani na kwa lipi?

2025 nayo ile palee, kila kitu kimegoma kurudi mahali pake,, mtatuambia nini wapiga kura sisi?

Tisheti na kanga?

Na bahati mbaya hata makanisani na misikitini huwa mnakwenda kumzuga padri, Asikofu na shekhe ili hali mkijua njia yenu ni ovu kuliko waovu wote, mnasubiri muibe kura 😂 na mjitangaze mmeshinda kwa kishindo!!

Mnakula mema ya nchi mkiendelea kuwahadaa wananchi walala hoi kwamba mnawatengenezea maisha bora? Njia zenyewe ndio hizo za kupandisha gharama kwenye kila bidhaa??

Mungu ilinde Tanzania kwa mkono wako wa chuma!

Uwabariki viongozi wetu waçhache wanaomaanisha kuwatumikia wananchi
 
Ni ujinga kulazimishwa eti tusikumbuke uzuri wa ilivyokuwa awamu ya Magufuli

Ni ujinga kuendelea kutiana moyo kwamba, eti tupo pazuri na tunaelekea pazuri zaidi...
Aliyesababisha Hadi Sukari kutoa 1500-2000 Hadi 3000-3500 ni Magufuli.

Huko kwenye umeme hakuna miujiza yeyote sana sana ni kwamba matumizi ya umeme yalipungua Kwa sababu watu walikimbia na kufunga biashara hivyo grid haikuwa na pressure tofauti na Sasa ambako kila kitu kimefunguka.

Hakuna wakati wowote Nchi hii Iko pazuri kushinda awamu ya 6,Kumlinganisha mtu aliyepora pesa za wafanyabiashara na Watumishi Kwa sababu ya kufilisika ni kumkosea heshima Samia.

Mwisho hakuna mtu anakukataza kumuwaza Mwendazake,wenzako wanaomtumia kama.kete ya siasa Kwa wajinga wewe unamkumbuka kushinda Muumba wako,hapo ndipo laana itakutafuna.

View: https://youtu.be/ccHxgZ05aNk?si=A0DuEkI_oM5mITNf
 
Aliyesababisha Hadi Sukari kutoa 1500-2000 Hadi 3000-3500 ni Magufuli.

Huko kwenye umeme hakuna miujiza yeyote sana sana ni kwamba matumizi ya umeme yalipungua Kwa sababu watu walikimbia na kufunga biashara hivyo grid haikuwa na pressure tofauti na Sasa ambako kila kitu kimefunguka...
Watu kama wewe mnajulikana kabisa hadi kazi mliopewa na hao mnaowatumikia! Sikulaumu, maadam unalipwa na familia yako inapata chakula, endeleeni bhana
 
Watu kama wewe mnajulikana kabisa hadi kazi mliopewa na hao mnaowatumikia! Sikulaumu, maadam unalipwa na familia yako inapata chakula, endeleeni bhana
Kazi gani? Kwani kipi Cha uongo nimeandika?

Mwendazake alikuwa hapori watu pesa? Alikuwa hafungii accounts na kuchota pesa? Hajawahi tamka kwamba atabadili pesa ili walizotoa pesa banki ziwadodee?

Na upuuzi mwingi kama huo.
 
Magufuli alikuwa ni disaster;
1. Alitangaza vita vya vyeti fake huku akilinda baadhi ya watumishi wakuu na idara nyingine wasiguswe.

2. Alihubiri kuangamiza rushwa lakini akiwaruhusu traffic police kupewa pesa za hongo alioiita pesa ya kupiga brush viatu.

3. Alianzisha elimu bure matokeo yake darasa la kwanza wanafunzi kwenye chumba kimmoja walijaa zaidi ya 200.

Hata pale vilipopatikana au kujenga vyumba vya madarasa hakuajiri walimu wapya kuendana na wingi wa madarasa.

4. Aliomba mkopo/msaada wa Elimu wenye thamani ya 400 million dollars uliokuwa na sharti ya kuruhusu waliozaa kurudi shuleni kuendelea na masomo,lakini ulipokuwa tiyari akauruka kimanga.

5. Akiwa waziri wa miundo mbinu wakati wa Jk,aliufagilia mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo,lakini alipoukwaa uraisi akaukana kabisa.

6. Alitumia pesa nyingi kujenga uzio wa kuzunguka eneo zima la madini ya Tanzanite huko Merelani ili kudhibiti utoroshaji wa madini hayo,kumbe wajanja wakachimba mahandaki kama ya wa Palestine ukanda wa Gaza,wakaendelea kutorosha madini hayo kwa njia za chini kwa chini.

7. Alihamia Dodoma kwa kuhamisha serikali yake na Taasisi mbali mbali tokea Dar kwa kile alichodai makao makuu ya nchi,lakini kwa nyakati mbali mbali akaifanya Chato kufanya shughuli mbali mbali za kitaifa hata kuliko Dodoma.

8. Hakupenda kukosolewa lakini yeye akiwakosoa waliomtangulia na viongozi wengine kwenye serikali yake.

9. Alikataa safari za kwenda nchi za nje za mbali akidai anapunguza matumizi kumbe alikuwa na kitufe Pacemaker chenye kurekebisha mapigo ya moyo ambacho kinaweza kuadhirika sana kwasababu ya mitambo ya electronic ya ndege.

10. Tuliambiwa tunadai ushuru wa makanikia sh 360 trillion tukaambuli sh 700 billion hata trillioni mmoja haijafika.

Kibaya zaidi Barrick waliitoa pesa hiyo kwa awamu wakisema ni msaada wa maendeleo wala si kodi ya makanikia hawadaiwi.

11. Alituhamasisha ataleta maendeleo kwa wananchi wote, kuwa hajali mwananchi anatokea chama gani lakini wakati mwingine akidai kuwabomolea nyumba ambao hawakumchagua.

12. Takwimu za viwanda alivyodai 8000 vimejengwa wakati wa utawala wake haikuwa sahihi.
 
Aliyesababisha Hadi Sukari kutoa 1500-2000 Hadi 3000-3500 ni Magufuli.

Huko kwenye umeme hakuna miujiza yeyote sana sana ni kwamba matumizi ya umeme yalipungua Kwa sababu watu walikimbia na kufunga biashara hivyo grid haikuwa na pressure tofauti na Sasa ambako kila kitu kimefunguka...
Eti matumizi ya umeme yalipungua kwa sababu.....

Sasa huu ndio uchawa professional, you have to think deep to serve your master to the maximum, damn damn!
 
Sukari sasa hivi inauzwa elfu 4,500 toka 3500
Mafuta yanuzwa elfu 5000 toka 3500
Petrol na dizel inauzwa elfu 400 toka 2000

Ni wazi wewe ni taahra
Bei hizo zimepanda mwezi huu ila kabla haikuwa hivyo na sababu ni viwanda kusimamisha uzalishaji sababu ya Mafuriko.

Serikali imeagiza tani 50,000 by February zinakuja bei itashuka.

Mwisho hakuna mwaka awamu ya 5 Sukari haijawahi kuadimika aunkupanda wengine tuna kumbukumbu nzuri,walikuwa wanasingizia sukari kufichwa na kuanza msako Kila mwaka ila sukari haijawahi shuka chini ya 3,000.

Pia simenti iliadimika mwaka 2019/2020 na ikawa Mwanzo wa kupanda bei Hadi Leo hii.
 
Yeye alifanyeje kumeneji suala la mlipuko wa bei za vyakula mbali na kuwa kwenye janga la Korona dunia nzima?
Sukari ilipanda bei kipindi chake, bundle lililpanda bei kipindi chake, au ulikua nchi gani?
hivi, Magufuli alitumia miujiza gani kwenye suala la Umeme na mgao kutokuwepo?
Mgao ulikuwepo sema tu ulikua hautangazwi, mfano nikiwa Dar between 2017 na 2019 tulikua hatupati umeme jumamosi na jumapili wakisema wanatengeneza "mradi mkubwa kigamboni".
Alitumia mbinu gani kufanya nishati ya mafuta isipande na nauli kuwa juu, licha kwamba kipindi cha Korona meli nyingi zilipaki?
Kipindi cha Covid 19 bei ya mafuta ilishuka sana maana demand ilikua hamna. Sasa mafuta utamuuzia nani bei ya juu wakati wazungu wote walikua kwa lockdown?
Ni ujinga kulazimishwa eti tusikumbuke uzuri wa ilivyokuwa awamu ya Magufuli
Nani kakukataza? Mlifanya maadhimisho ile 17 March pale chato ila hamkufika watu 60!! Badala ya kelele nyingi humu nendeni Chato mkaadhimishe sio mnajazana upepo humu alafu ikifika 17 March mkawa busy kujadili kifo cha Bob Junior mkamsahau JPM!!
 
Suala la cement kuadimika ilikuwa ni haki, miradi ilikuwa ikitumia saruji nyingi kiasi cha kufanya iadimike
As for now miradi inaendelea na mingine Mingi imeanzishwa Kwa nini saruji isiadimike?

Unakumbuka Dangote alitaka kutimkia? Mwendazake hakuna alivhoweza Kila mtu alikuwa mbaya kwake.

Wakitaka kumpora pesa Dangote shenzi zenu.

Mimi huwezi nidanganya awamu ya 5 Nina kumbukumbu vizuri.

Hata Mafuta ya kula yamianza kupanda 2019,Mafuta ya magari Kuna mwaka yaliadimika
 
Ni ujinga kulazimishwa eti tusikumbuke uzuri wa ilivyokuwa awamu ya Magufuli

Ni ujinga kuendelea kutiana moyo kwamba, eti tupo pazuri na tunaelekea pazuri zaidi

hivi, Magufuli alitumia miujiza gani kwenye suala la Umeme na mgao kutokuwepo?

Yeye alifanyeje kumeneji suala la mlipuko wa bei za vyakula mbali na kuwa kwenye janga la Korona dunia nzima?

Alitumia mbinu gani kufanya nishati ya mafuta isipande na nauli kuwa juu, licha kwamba kipindi cha Korona meli nyingi zilipaki?

Sukari nayo imeshindikana sasa kushuka licha ya kuwa na kiwanda cha Bagamoyo sugar na kikubwa kulikoni vyote East Africa, sukari kg 4000 mpaka 4500, kweli???

Tunatafutana nini hapo?

Mara unasikia nishati ya mafuta imwshuka, ila nauli zinazidi kupaa juu tu, inamaana wafanya biashara ndio wanaoongoza nchi kwa sasa??
Kazikwe naye
 
Back
Top Bottom