HakiElimu vs Govt: The saga

Kuntakinte,

Logic unayotumia hapa si sawa. Masista hawana watoto wanaosoma kwenye shule za manispaa zetu. Lakini ni wadau wa dhati wa Elimu. Wanasomesha vizuri sana watoto wetu huko St. Joseph Mbeya, na kwingineko.

Mtu akishutumu magereza yanavyoendeshwa ni lazima awe na mtoto aliyefungwa kwanza? Ili ukubalike katika kupinga utoaji mimba ni budi uwe umeshiriki hicho kitendo kwanza?

Mimi nakubaliana na Kamundu kwamba HakiElimu inaweza kuwa ndio NGO yenye manufaa kuliko zote Tanzania. Inataka kuinua kiwango cha Elimu. Na ukifanya hivyo unaliinua taifa lote.

Augustine Moshi
 
Mtu akishutumu magereza yanavyoendeshwa ni lazima awe na mtoto aliyefungwa kwanza? Ili ukubalike katika kupinga utoaji mimba ni budi uwe umeshiriki hicho kitendo kwanza?
Augustine Moshi

teh teh teh

tupende tusipende HAKIELIMU ni modeli nzuri.......yafaa watu kama REDET ijifunze kutoka kwao. ukitumia data za REDET ku-customize modal ya demokrasia kwa mazingira ya kwetu always you wil end up gettuing wrong results (wrong reflection), ukichukua data za HAKIELIMU ukaweka ktika modal ya mendeleo ya elimu Tanzania = true reflection

hongera HAKIELIMU
 
sawa Baba Nimekubali Ila Kwa Ushauri Basi Angekuwa Kwenye Matangazo Yake Mwishoni Anatupa Angalau Mawazo Mbadala Saidizi Yakukabiliana Na Tatizo Na Sio Kutuacha Njia Ya Panda.
 
Kama wachangiaji wengine walivyoeleza si lazima sana kuwa na mtoto kwenye shule za serikali ndio uwe na uchungu wa elimu yetu, kwa kuwa yeye ni mtanzania anayo haki ya kutoa maoni yake pale anapoona kuna kasoro. Na huu ndio moyo tunaotakiwa kuwa nao kama watanzania pindi tuonapo kuna kasoro hatuna budi kuondoa jambo hilo kwa midomo yetu (kwa kuongea), kwa mikono yetu ( kuandika kama tufanyavyo sisi) au kuonyesha basi kwamba tunalichukia jambo hilo kuwa ni baya.

Mrisho
 
kwa mnaosema haki elimu haina mawazo inamaana hamjasoma hiyo power point

5. Way Foward


1. Simplify, simplify, simplify education budget
. One source
. One plan
. One report
2.Enhance transparency
. central level
. District level
. School level
3. Allocate the funds to learning outcomes not just inputs.
4. Make flows to school clear and predictable in advance.
5. Strenghen independent evaluation.

Hayo ndiyo mawazo na kusema hawa Haki Elimu wanapinga tu si kweli, labda hujasoma au mna agenda binafsi.
 
sawa Baba Nimekubali Ila Kwa Ushauri Basi Angekuwa Kwenye Matangazo Yake Mwishoni Anatupa Angalau Mawazo Mbadala Saidizi Yakukabiliana Na Tatizo Na Sio Kutuacha Njia Ya Panda.

Ha ha- akitokea!!.........hadi Nakosa cha Kuandika..
Kwa kifupi Nina mashaka na Na jinsi gani Hakielimu wanavyo Zingua Wananchi!!...

Ok!! aanze Kutokea Ili tupime Uzalendo wake!!
 
Ila Augustine Nakubaliana na wewe ila wakale walisema ukitaka kujua Uhondo wa Ngoma uingie Ucheze na kama ni hivyo Bwana Rakesh alitakiwa awe na experience hata ya Mtoto 1 ndani ya shule moja ya Manispaa.

Ili Hata Watoto wake Watusaidie....Kwasabau Bila haki Elimu leo Tusinge wasiliana kama hivi tunavyo heshimiana kwenye hii Thread!!...

Mimi Babo nina Amini-Ni-vizuri kwa Mkosoaji nae a-kosolewe!!
Mi Nina Fikiri (Haki elimu) Ni mentality Yake Huyo Boss!! Sijui anaitwa - Rakesh!!atu ambie ali itoa wapi hilo wazo!! kwenye Makabila au kabila gani !!?
 
Kuntakinte,

Mtu akitoa tangazo kusema kuna udanganyifu, ni lazima atoe tena mawazo akuambie ufanyeje ili uache kuwa muongo?

Kama serikali ilisema ingetumia shilingi bilioni kadhaa kwenye mradi fulani wa Elimu na haikufanya hivyo, HAKIELIMU wakituelewesha kuhusu huo udanganyifu inatosha. Mdanganyifu anatakiwa apewe mawazo mbdala zaidi ya kuambiwa aache udanganyifu?

Kama serikali inapanga fedha finyu kwa ajili ya Elimu, wazo mbadala la kitu hicho ni nini? Labda ni kutenga fedha zaidi kwa ajili ya Elimu. Lakini hilo linaingia lenyewe ukishasema fedha zimetengwa chache.

Augustine Moshi
 
Gigo sijafurahishwa sana na mawazo yako kwa sababu zifuatazo.

1. Umekua ukijali zaidi huyo jamaa wa Haki Elimu hasili yake baada ya mawazo ya haki Elimu.Kitu ambacho nafikiri si vizuri kwa miaka hii kusema kuhusi hasili ya mtu badala ya maendeleo ya nchi.
2. Ulisema Haki Elimu wanakosao kuliko kuelimisha lakini nimekupa mawazo hapo juu ambayo wametoa, hivyo kama ungepingana nayo ingekua vizuri utoe sababu za msingi kama watu wengine kuelimishana.
Nilazima tuelewe kuna watu wenge Watanzania wenye hasili tofaouti lakini wanafanya vitu vinavyo hitaji sifa nyingi na hii ni mojawapo kwa huyo kiongozi. Sio watu wote wenye asili ya kiasi ni richmond type. Tunatakiwa tufikirie above race zetu kama binadamu ni si kuweka vimaswali na kutokuaminiana kwa sababu ya rangi au hasili ya mtu yeyote, kwa kweli sijafurahishwa na Gigo unavyo msema huyu jamaa wa haki elimu kwa kweli si vema na unatakiwa kuomba msamaha.
 
teh teh teh

tupende tusipende HAKIELIMU ni modeli nzuri.......yafaa watu kama REDET ijifunze kutoka kwao. ukitumia data za REDET ku-customize modal ya demokrasia kwa mazingira ya kwetu always you wil end up gettuing wrong results (wrong reflection), ukichukua data za HAKIELIMU ukaweka ktika modal ya mendeleo ya elimu Tanzania = true reflection

hongera HAKIELIMU

Tatizo la Watanzania ni kutokuwa na tafakari ya mbali,binafsi sina tatizo na kazi za Hakielimu,lakini kama wadau wengine walivyochangia kuonyesha dalili za tatizo ni moja lakini kwenda mbali zaidi na kutafuta chanzo cha tatizo na namna ya kutatua. Mfano ukienda hospitali ukihisi homa,Daktari atakusikiliza anaweza akakisia tatizo kwamba inawezekana kwa jinsi ulivyojieleza ukawa na malaria,pamoja na hisia hizo haishii hapo atakuelekeza kupita kwanza maabara ukitoka maabara unarudi tena kwake akishajiridhisha kwamba hilo ndilo tatizo lako hatua ya mwisho ni kukuandikia dawa zinazofaa kwa tatizo lako. Sasa narudi kwa Hakielimu, na mfano hapa ninaotaka kuutumia ni wa Kanumba mtoto wa shule kutoka familia maskini,sasa hapa wanachotaka kutuambia ni nini? na suluhisho lake ni lipi? Huo ndio ukweli kwamba tuna matabaka ya wenye nacho na wasionacho,sasa uchambuzi mzuri ni ule unaochimbua mzizi na kutupa suluhisho,waache uwoga na hofu ya kuitwa wachochezi. Kuhusu REDET sina uhakika kama huyu mdau anajua anachokisema ama amewahi kushiriki tafiti za REDET hata mara moja, ok inawezekana dodoso zinazoandaliwa zikawa hazijitosherezi lakini ni kazi ya Mtafiti husika kwenda mbali zaidi na kutoa tafakari pana zaidi ya kile alichokipata ama kukiona katika eneo aliliopangiwa kutafuta data.
 
Utu, hapa goverment inataka kutatua matatizo ya wananchi na katika hili Haki Elimu inapinga budget ya serikali na silo lingine. Haki Elimu inaonyesha sehemu zilizo pungufu kwenye budget na hii ni topic ya hilo, hivyo tuwe makini na point hapa. Mawazo yao ni haya hapa (Ya budget)2007-2008

5. Way Foward
1. Simplify, simplify, simplify education budget
. One source
. One plan
. One report
2.Enhance transparency
. central level
. District level
. School level
3. Allocate the funds to learning outcomes not just inputs.
4. Make flows to school clear and predictable in advance.
5. Strengthen independent evaluation.

Sasa kwa mambo mengine kama ambayo hayana uhusiano na budget ni vizuri ukaenda kwenye website yao badala ya kutoa mifano ya ugonjwa na hospitali, kuna mifano ya ukweli kwenye website yao, kama unataka nitatuma hapa.Hawa jamaaa hawajafanya kitu chochote kibaya na ni vizuri wanashughulikia elimu na ni mfano wa kuigwa.Ni lazima ujue haki elimu nia yake ni nini na ni chama cha nini kabla hujaanza kukosoa.
 
Lengo kuu la HakiElimu ni kuchangia katika kuhakikisha kuwa kila mtoto nchini Tanzania - bila ubaguzi wa aina yoyote ile- anapata haki yake ya elimu bora ya msingi na sekondari. Hapa tunasisitiza kuwa si elimu ya aina yoyote tu, bali ile inayokuza utamaduni wa kuheshimu haki za binadamu, demokrasia na uzalendo wa dhati ikiwa ni pamoja na uraia unaotambua na kuzingatia haki na wajibu wake na kuweza kuhoji pale haki hizo zinapokiukwa. Kwa mtazamo wetu shule nzuri ni ile inayomjali mtoto, yenye kujali na kuheshimu haki na usawa wa kijinsia (angalia maelezo kuhusu Shule Nzuri ni Ipi (Kuweza kusoma faili hili, unahitaji Acrobat Reader Bonyeza hapa). Shule ni mahali ambapo watoto wanakua na kujifunza kufikiri mambo kwa undani na kuwa wabunifu, ni mahali wanapopata stadi za maisha na kujenga hali ya kujiamini na ambapo wanaheshimiwa na kujifunza kuwaheshimu wengine.

Maono au dira hii ndiyo sababu ya msingi ya kuanzishwa kwa HakiElimu. Uchambuzi wa hali halisi uliotolewa katika sehemu iliyopita unaelezea uchaguzi wa mkakati wetu wa kufikia dira hii. Utaratibu na mbinu yetu katika utekelezaji wa azma hii unaondokana kabisa na dhana ya kuendesha programu yetu kama shughuli ya hisani (welfare) au mradi. Hatuamini kuwa itasaidia sana kuanzisha miradi midogo midogo ya kutoa huduma za kuboresha shule bila kwanza kushughulikia tatizo la msingi linalosababisha kuzorota kwa elimu. Badala yake, tukizingatia uchambuzi wetu, HakiElimu inaelekeza jitihada zake katika kuwezesha na kuimarisha zaidi ushiriki wa wanaume, wanawake na watoto katika utawala wa elimu nchini Tanzania. Tunaamini kuwa kufufua na kuimarisha utawala bora ni jambo muhimu sana katika kuleta mageuzi katika elimu, ikiwa ni pamoja na kufanikiwa kwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP).

HakiElimu inaendesha shughuli zake ili kufikia lengo hili katika ngazi tatu za kimkakati kama inavyoainishwa hapo chini.

1. Utawala wa Jamii: HakiElimu inawezesha wadau katika ngazi ya chini kabisa kuwa na usemi wakati wa kufanya maamuzi na kubadilisha shule zao kwa kuwezesha ushiriki wao kamilifu katika utawala wa shule na jamii zao. Kwa kuanzia kazi hii inatekelezwa katika wilaya mbili na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2003 itakuwa ikitekelezwa katika wilaya nne ambazo zinaonekana kuwa na mfumo duni wa elimu na ambazo HakiElimu imeweza kufikia makubaliano nazo kuhusu namna ya kushirikiana ili kuleta maendeleo. HakiElimu imeweka waraghibishi wawili wa jamii katika kila wilaya ili kuratibu kazi hiyo. Mafunzo yanayojitokeza katika utekelezaji wa kazi hiyo yanawekwa katika kumbukumbu na kuchapishwa kwa namna ambayo itakuwa rahisi kuwafikiwa watu wengi zaidi na hatimaye kusambazwa Tanzania nzima hivyo kuwa na matokeo makubwa zaidi.

Lengo la msingi ni kuchochea na kuhimiza demokrasia katika kamati za shule, hii ni katika muundo wake (wajumbe wake nk) na utekelezaji wa majukumu yake. Umuhimu wa kipekee unawekwa katika kuyahusisha makundi ambayo yanawekwa pembezoni na kunyimwa haki zao za kimsingi, ikiwa ni pamoja na watoto, vijana, watu wenye ulemavu, wanawake na masikini, na kuhimiza usawa wa kijinsia. Kamati zinasaidiwa ili ziishirikishe zaidi jamii na kuzifanya ziwajibike zaidi kwa jamii zao, ikiwa ni pamoja na kusikiliza na kushughulikia maoni na hata kero zinazotolewa na wanajamii husika.

HakiElimu inasaidia pia wadau wengine muhimu, hususan wanafunzi na walimu kuanzisha au kujiunga na vyama vyao katika maeneo yao. Ujenzi wa mitandao, upashanaji habari na mafunzo ni mambo yanayohimizwa na kuendelezwa ndani ya wilaya na baina ya wilaya moja na nyingine. Mbinu za uwezeshaji shirikishi na matumizi ya michoro na vielelezo mbalimbali (animation) zinatumika wakati wote ili kuondoa vikwazo vya mfumo wa kufanya maamuzi wenye urasimu na ngazi nyingi za madaraka. Azma ya HakiElimu ni kuimarisha uwezo wa taasisi za wananchi katika maeneo yao ili kuwezesha kufuatilia kwa makini na kuwa na usemi kuhusu utoaji wa huduma ya elimu, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha uwajibikaji wa viongozi katika jamii husika na uwazi katika matumizi ya fedha.

2. Ushiriki wa umma: HakiElimu inachangia katika kuanzisha na kuendeleza harakati za kitaifa aa mabadiliko ya kielimu na kijamii kwa kuchochea na kuhimiza ushiriki mpana zaidi wa jamii, upashanaji habari, kuanzisha na kukuza uanachama na kujenga mitandao ya wanachama. Kazi hii inatekelezwa Tanzania nzima, na ina vipengele vikuu viwili:

Kipengele cha kwanza kinahusu kuibua na kuhamasisha mjadala wa umma kuhusu masuala muhimu katika elimu ya msingi kwa kutumia machapisho mbalimbali, vyombo vya habari vyenye ubunifu na mikutano na makongamano ya umma. Mjadala huu umeanza kwa kuangalia kero au mambo ambayo jamii zingependa yashughulikiwe lakini pia unaingia kwa undani zaidi na kuangalia masuala ya msingi kama vile 'nini malengo ya kwenda shule' na 'mtoto aliyeelimika ni yupi'. Aidha, mjadala huu unaangalia pia masuala mbalimbali yenye mkanganyiko, mathalan, 'iwapo elimu ni muhimu, kwa nini tunawatendea walimu vibaya na kutowathamini'. Mbinu inayotumika ni ile ya kuuliza maswali na kuchochea mijadala badala ya kuhutubia au kuhubiri na kutoa majibu. Umma unahimizwa kuchambua hali mbaya inayoikabili elimu na hatimaye kupendekeza utatuzi wake.

Kipengele cha pili, ambacho pengine ni kipengele cha mkakati wa HakiElimu chenye malengo makubwa sana, ni kujenga msingi imara na kupanua wigo wa uanachama wake miongoni mwa watu binafsi na taasisi zinazojali maendeleo ya elimu kutoka sehemu zote nchini, katika chombo kinachoitwa 'marafiki wa elimu'. Msisitizo unawekwa katika ushiriki kamilifu wa wanawake, wanaume, watoto na vijana. Marafiki wa Elimu wanaweza kuchangia maoni yao na mambo wanayoyatilia shaka na kupatiwa majibu haraka kwa maswali mahsusi wanayoyauliza. Aidha, wanapatiwa taarifa za mara kwa mara kuhusu masuala ya kisera na maoni kuhusu mambo yanayoweza kufanyika ili kuinua elimu katika jamii yao. HakiElimu inawaunganisha marafiki na kuwapatia fursa ya kubadilishana mawazo na uzoefu, kujifunza na kuchukua hatua za pamoja. Vyama vya wananchi na mitandao yao iliyo na isiyo rasmi, itasaidiwa ili kuinua zaidi hamasa na mwamko wao kuhusu elimu nchini. Baada ya muda marafiki wanachama watakuwa ni chombo kikubwa cha wananchi wenye ufahamu wa hali ya juu, waliojiunga pamoja, wanaoweza kuwaelimisha wengine na kutoa shinikizo la kijamii kwa mamlaka zinazohusika na utoaji wa elimu. 3.Uchambuzi wa Sera na Utetezi: HakiElimu inajitahidi kupata fursa ya kutoa mchango wa mawazo na ushauri katika uundaji na utekelezaji wa sera za kitaifa kuhusu elimu na masuala mengine yanayohusiana nayo, na kuinua kiwango cha ushiriki wa umma katika utayarishaji wa sera kwa kupitia programu za utafiti, uchambuzi, utetezi na kujenga mitandao. Hii inajumuisha uchambuzi wa athari za sera za kitaifa katika elimu na kuelimisha umma na wote wanaohusika katika utengenezaji wa sera kuwa demokrasia na elimu bora ni mambo ya msingi kabisa katika kazi ya kuondoa umasikini, kuleta usawa wa kijinsia na utawala bora.

Programu hii ina vipengele vikuu vitatu, kipengele cha kwanza kinahusika na ujenzi na uimarishaji wa uwezo wa HakiElimu katika kufanya utafiti na uchambuzi madhubuti, ikiwa ni pamoja na kuwa na maktaba inayojitosheleza yenye nyaraka zote muhimu. Matokeo ya tafiti mbalimbali na uchambuzi huo wa sera yanawasilishwa katika taarifa ya kila mwaka itakayoitwa- Hali ya Elimu Tanzania- na katika nyaraka maalumu kuelezea msimamo wa kisera.

Kipengele cha pili ni kile cha kuwezesha ushiriki wa wahusika wengi kwa kadiri iwezekanavyo katika utayarishaji wa sera za kitaifa na ufuatiliaji wa utekelezaji wake. Hii ni pamoja na kuwezesha uwasilishwaji wa mawazo na maoni ya wananchi kutoka katika ngazi ya chini kabisa na umma kwa ujumla katika michakato muhimu ya kufanya maamuzi ya kisera, na katika kuuliza maswali muhimu kuhusu mambo ambayo kwa sasa hayashughulikiwi kikamilifu.

Kipengele cha tatu kinahusu uundwaji wa programu shirikishi na za kibunifu za utetezi na ushawishi kwa lengo la kuhimiza mabadiliko ya kijamii katika elimu. Programu hii inalenga katika kujenga ushirikiano maalumu wa kimkakati na mashirika mengine yasiyo ya kiserikali, taasisi za utafiti, wanaharakati wa masuala ya kijamii, vyama vya wafanyakazi, viongozi wa serikali na jamii wenye uchungu na hali ya elimu nchini, vyombo vya habari na wadau wengine. HakiElimu inaanzisha ushirikiano na kampeni mbalimbali za kitaifa na kimataifa, mathalan, kampeni ya kuzingatia masuala ya jinsia katika utayarishaji bajeti, Elimu kwa Wote na Jubilee 2000 yenye lengo la kuzishawishi nchi tajiri kuzifutia madeni yote nchi masikini. Msisitizo unawekwa katika kuwapa taarifa wabunge na viongozi wengine wa kuchaguliwa. Aidha, utaratibu unawekwa wa jinsi ya kushughulikia haraka na kwa ufanisi masuala na fursa mbalimbali zitakazojitokeza.

Kwa pamoja vipengele hivi vitatu vinaiwezesha HakiElimu kuwa 'kurunzi' makini katika sekta ya elimu. Jukumu hili la kufuatilia kama mambo yanakwenda sawa na kubainisha pale penye matatizo ni muhimu sana katika uendeshaji jamii kidemokrasia, hususan, katika zama hizi ambapo masuala mbalimbali ya kijamii yanashughulikiwa kisekta, kama ilivyo kwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu ambao fedha za wafadhili kusaidia sekta hiyo zinatolewa moja kwa moja kwa serikali.

Uhusiano unajengwa kati ya programu tatu za HakiElimu - Utawala wa Jamii/Umma, Ushiriki Umma na Uchambuzi wa Sera na Utetezi ili kuwezesha wahusika wote kujifunza kutoka kwa kila mmoja na kujiimarisha kimkakati katika ngazi zote. Vipengele vikuu vya mkakati na uhusiano baina yao vinaelezwa kwa kifupi katika kielelezo kifuatacho.
 
Habari zilizopo za haraka haraka kabla sijaleta Mafaili ya Uthibitisho ambazo ni zakuaminika 90% Mzee wa Kihindi kachemsha baada ya kujulikana kwamba anatoa Mafunzo na Ufahamu mzuri kwa wanajamii wa kitanzania kuhusu Elimu imethibitika anang'atuka mwezi September baada ya shinikizo kutoka kwa Wafanyakazi wake wakidai ya kuwa NI DIKTETA NA MBINAFSI HASA PALE INAPOFIKIA SUALA LA MISHAHARA YAO na sababu nyingine ambazo nitazileta baadae.

Sasa najiuliza ina maana kumbe UNAWEZA UKAWA NA ELIMU YA KUELIMISHA HALAFU WEWE MWENYEWE USIWE UMEELIMIKA? Na kwasasa ndio anajaribu kukamilisha taratibu za kung'atuka baada ya skendo hilo linalokwenda chini kwa chini likionekana kama linafichwa fichwa na atamkabidhi Mwanamama ambaye nitalileta jina lake soon nitakapokamilisha Habari

Nilishasema HAKI ELIMU NI NZURI SANA ILA TATIZO HAWATOI MAWAZO JENZI JUU YA SUALA WANALOLIMULIKA NDANI YA JAMII KAMA USHAURI NA WAO WENYEWE KUJIANGALIA NDANI NA NJE KAMA WANAELIMU SAWA NA WANAYOITOA. Ila Mama naona anakuja kulisawazisha hilo.

Najua wapo wana forum wengi humu tena kwa majina nawajua wanayajua haya tena wameyajua Kabla yangu sasa sijui ni utashi au ndio hawataki tuujue ukweli sasa mimi Nitaanika HADHARANI.

Kunguru Kukunyea sio kwamba anashabaha.....

Habari zaidi zitakuja soon....
 
Ni kweli kabisa.
Nilishakutana na mfanyakazi wa haki elimu, alieleza jinsi gani wananyanyaswa na huyu bwana. Alisema yupo pale kwa kujifunza kazi tu na si kitu kingine. Anaeshika alitolewa gazetini kwa jina na picha - ni Betty Misokia.
AF
 
Tatizo watanzania tumeshazoea kuchukulia NGOs kama sehemu ya kula hela za wafadhili. Sasa huyu jamaa ambaye ni mmoja wa the remaining UNREPENTING SOCIALISTS ni mgumu mno wa kutoa ulaji na vilevile kazi kwake ni suala la masaa 24. Si bure mambo yakawa mabaya kwa kina sisi tunaona tuna haki ya kujifaragua na mabilioni ya "wafadhili".

Kitu kimoja ni kuwa kuondoka kwake huyu jamaa ambaye anaitwa RAKESH RAJANI ni mwanzo wa mwisho wa HAKIELIMU kama sauti ya kweli ya mnyonge. WADENNISH wataacha kutoa support na kidogo kitakachoendela kupatikana kitaliwa in the name of "ALLOWANCES"

Waliokaliwa kooni na HAKIELIMU watashangilia....Tanzania yetu inasonga muda..

Tanzanianjema
 
..ni maarufu kwa kuwanyima maslahi mazuri waswahili!

..ila mzigo wanapiga. sasa,betty atakuwa na jeuri kama ya rajani?au ndo rajani ataondoka na umaarufu wa hakielimu!
 
Man!
the guy is famous, anajulikana sana.
Naamini Betty will equally be, we ladies can do whatever men can. OK?
AF.
 
Hapa hakuna suala ladies ama gentlemen. Anayoyafanya RAKESH ni makubwa hata kwa mamilioni ya wanaume tulionao Tanzania. Its about committment, passion, creativity and more so guts to stand were many could not dare....

Na sio kuwa ni famuos bali anaaminika sana miongoni mwa watu waliopo katika asasi za kiraia...kulikojaa manyang'au wanafiki ambao ni wabaya kuliko hao wanaoiba kwa ukweli na uwazi..

Tanzanianjema
 
AF,
Mbona nilisikia watu wengine wanaofanya HAHIELIMU wanasema kuko poa? Hata maslahi sii mapaya?
Usije ukakuta hayo wanayoongea ni majungu!
Kwani Mhindi sii Mtanzania?
Unataka kuniambia if you have a barometer kupima uzalendo- Prof. Issa Shifji na Majorie Mbilinyi sii walazendo mara nyingi kuliko hawa wenye rangi nyeusi wanotuibia?
 
AF,
Mbona nilisikia watu wengine wanaofanya HAHIELIMU wanasema kuko poa? Hata maslahi sii mapaya?
Usije ukakuta hayo wanayoongea ni majungu!
Kwani Mhindi sii Mtanzania?
Unataka kuniambia if you have a barometer kupima uzalendo- Prof. Issa Shifji na Majorie Mbilinyi sii walazendo mara nyingi kuliko hawa wenye rangi nyeusi wanotuibia?

Mzalendo,
I believe the source of information was ok.
Alisema watu na qualifications zao za kueleweka walikuwa wakiondoka/wakiacha kazi kwa karaha nyingi za pale. Even the source of inf. left long time ago. Si unajua walio juu juu hujipendelea kwa hili na lile? Kazi kwa the low cadre staff. Si unajua haya mambo?
AF.
 
Back
Top Bottom