KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 86
Mbunge: HakiELimu itaidondosha serikali
na Tamali Vullu, Dodoma
WABUNGE wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameitaka serikali kuichukulia hatua taasisi isiyo ya kiserikali ya HakiElimu kwa maelezo kuwa matangazo yake yamekuwa yakibeza juhudi za kuendeleza elimu nchini.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti bungeni mjini Dodoma jana, mmoja wao alifikia hatua ya kuionya serikali kuwa makini na taasisi hiyo ambayo alisema isipoichukulia kwa umakini inaweza ikaingoa madarakani kama ilivyotokea nchini Zambia.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi jana, Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai (CCM) alisema, matangazo yanayotolewa na HakiElimu yamekuwa yakibeza juhudi za serikali.
Ndugai alionyesha kushangazwa na lengo hasa la HakiElimu kiasi cha kufikia kuhoji taasisi hiyo ipo upande gani na akasema iwapo inafanya kazi zake kisiasa, ni vema ikaandikishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa.
Aliishauri serikali kuwa macho na taasisi hiyo na kuitaka kutoendelea kukaa kimya, kwani inaweza kujikuta pabaya baada ya muda.
Akitoa mfano, Ndugai alisema kuwa hali inayofanana na hii, iliwahi kutokea huko Zambia miaka kadhaa iliyopita na kusababisha serikali iliyokuwa madarakani kungolewa.
Mbunge mwingine Janet Masaburi (Viti Maalumu-CCM) naye aliunga mkono hoja hiyo ya Ndugai kwa kusema kuwa, matangazo yanayotolewa na taasisi hiyo iliyojipatia umaarufu mkubwa miaka ya hivi karibuni, yanajenga chuki miongoni mwa wananchi dhidi ya serikali yao.
Masaburi alisema anaamini si vyema kwa serikali kuchezewa, wakati ikijulikana wazi kuwa imekuwa ikifanya juhudi kubwa kukuza kiwango cha elimu nchini.
Hoja hizo za wabunge zimekuja miezi kadhaa sasa tangu serikali ipige marufuku matangazo ya asasi hiyo isiyo ya kiserikali kabla ya kuifungulia kuendelea na shughuli zake.
Aidha, uamuzi kama huo pia umewahi kuchukuliwa na Serikali ya Awamu ya Tatu ambayo pia, ilipiga marufuku kurushwa katika redio na televisheni kwa matangazo ya taasisi hiyo yaliyokuwa yakihimiza kuhusu haja ya kutoa elimu bora.
Wakati fulani serikali iliwahi kuifungia taasisi hiyo kutoa matangazo yake kwa maelezo kuwa yanakejeli juhudi za serikali katika kukuza sekta ya elimu nchini.
Awali, akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo jana asubuhi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Margaret Sitta, alisema kuwa, serikali imepanga kuajiri walimu 14,490 na watumishi wasio walimu 397, sambamba na kuidhinisha maombi ya ajira za walimu 6,000 raia wa kigeni kwa ajili ya shule siziso za serikali.
Alisema wizara hiyo pia itathibitisha kazini watumishi 1,000 na kupandisha vyeo watumishi 10,486 ambao wamekaa katika madaraja waliyonayo kwa muda mrefu.
Sitta alisema wizara hiyo inaandaa mpango ambao utaratibu mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi wake 2,110.
Tutatoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa wakuu wa vyuo shule/vyuo, wakaguzi wa shule na waratibu wa elimu ya sekondari wa kanda za Kusini, Nyanda za Juu Kusini, Ziwa na Magharibi kuhusu haki na masilahi ya watumishi, sheria, kanuni na taratibu za utumishi, alisema Waziri Sitta.
Waziri Sitta alisema katika kufuta ujinga na kujiendeleza katika mfumo usio rasmi, wizara itaendelea kutoa mafunzo kwa vijana nje ya shule, wafanyakazi na watu wazima ambao hawakupata nafasi ya kujiendeleza.
Alisema katika mwaka wa fedha 2007/2008, wizara hiyo itatoa mafunzo ya stashahada ya juu kwa walengwa 244, stashahada ya kawaida kwa watumishi 293 na cheti cha sheria kwa watu 225.
Alisema katika kutoa elimu bora na inayoendana na wakazi, wizara hiyo itaimarisha mitaala na mihtasari ya elimu ya awali, msingi, sekondari, ualimu na elimu maalumu.
Katika kufanikisha hilo, Waziri Sitta, alisema watarekebisha mitaala na kuandika mihtasari ya ualimu ngazi ya cheti, ili iendane na mabadiliko ya mitaala.
Pia alisema watabuni na kuandaa mtaala wa mafunzo ya ualimu unaotumia teknojia ya kisasa (e-learning), ili kuwafikia wadau wengi.
Alisema pia kuwa serikali inatarajia kujenga nyumba za walimu 1,500 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2007/2008, na kiasi cha sh bilioni 13.5 zimetengwa kwa ajili hiyo.
Alisema nyumba hizo zitajengwa katika shule za sekondari za serikali, hususan kwenye maeneo yenye mazingira magumu.
Alisema, katika kipindi hicho, serikali itachangia ujenzi wa hosteli 10 kwa ajili ya wasichana katika maeneo ya wafugaji na yaliyo nyuma kielimu pamoja na kuchangia ujenzi wa madarasa 800 na vyoo 76 katika shule za sekondari.
Waziri alisema pia katika kipindi hicho, wizara hiyo itagharamia wanafunzi 42,710 wa kidato cha kwanza hadi cha nne na wanafunzi 3,352 wa kidato cha tano na sita wanaotoka kwenye familia zenye kipato duni.
Mafanikio makubwa ya ujenzi wa shule za sekondari zinazojengwa kutokana na mwitiko mkubwa wa wananchi zimesababisha mahitaji makubwa ya walimu, vifaa vya kufundishia, na kujifunzia, nyumba za walimu, maabara, madarasa na majengo ya maabara.
Baadhi ya wanafunzi kuishi mbali na shule kunaweza kusababisha ongezeko la mdondoko wa wanafunzi ikiwa ni pamoja na kupata mimba, hivyo kusababisha mahitaji makubwa ya hosteli, alisema.
Kutokana na hali hiyo, Waziri Sitta, alisema wizara itaibua mjadala wa kitaifa kuhusu tatizo la mimba kwa wanafunzi, kukazia sheria ya kuwaadhibu wanaowapa mamba na uwezekano wa kuwarejesha shuleni baada ya kujifungua.
Alisema wizara hiyo pia itapitia upya andiko la Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) kwa lengo la kuzingatia upanuzi wa shule za kidato cha tano na sita na vyuo vya ualimu, ili kukidhi mahitaji ya sasa.
Pia alisema watatoa mafunzo kazini hasa kwa walimu wa masomo ya hisabati na sayansi, ili kuinua kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa masomo hayo.
Waziri Sitta, alisema serikali itaendelea kutoa vibali vya kuanzisha shule za sekondari za seriakli 5,000 zinazoajengwa kwa nguvu za wananchi na kusajili shule zisizo za serikali pamoja na kukusanya takwimu za walimu walio kazini kwa ajili ya kuwasajili kutoka halmshauri 47.
Pia, alisema wataratibu na kufuatilia ukarabati wa miundombinu katika shule zenye wanafunzi wenye ulemavu; Moshi Ufundi, Moshi Sekondari, Lugalo, Mpwapwa, Korogwe, Iringa na Kazima.