Haki za Raia anapokamatwa na Polisi: Je Dr. Ulimboka Alizijua?

Sijui kama mleta mada anajua anachokileta hapa, kweli JF imevamiwa kama ndiyo great thinkers mimi naogopa
 
Lakini bado kuna kitu cha kujifunza hapa.
Kwenye hali ya mgomo unaohusishwa kundi la watu wengi, viongozi wasiwe warahisi kukubali vikao visivyo rasmi na watu wasio rasmi, japo haindoi kwa asilimia mia moja hatari ya kutekwa.
Na muda, mishale ya saa sita usiku!

Kama walivyosema wachangiaji wengine thanks to his sloppiness now we know what kind of government we have
 
Kichuguu,

..Je, raia wana haki ya kukataa[right to remain silent] kutoa maelezo kwa vyombo vya dola??
Yeah kwasababu chochote utakachosema kitatumika kama ushahidi, uzuri wa kipengele hiki ukae kimya ili mwanasheria wako ndo aongee na kama huwezi kumudu gharama za mwanasheria serikali ina jukumu la kukupatia mwanasheria
 
JF ni darasa kubwa sana, miaka minne iliyopita, kuna mwanachama mmoja alitupa somo hapa kama ifuatavyo

(1) Je kuna yeyte kati yetu amewahi kufikiria ku-exercise rights zake mbele ya polisi?

(2) Ilikuwaje Dr. Ulimboka alikubali kukamatwa na polisi bila kuzingatia haki zake hizo? hasa zile tatu za kwanza? Inawezekana hakuwa anazijua; tujitahidi tujifunze mambo mengine yaliyok nje ya taaluma zetu, hasa sheria.

(3) Inawezekana alikuwa anazijua lakini hakuwa na nafasi ya kuzi-exercise kwa vile askari walimfuata wakiwa wamemshikia bunduki, lakini je iwapo askari wakikushikia bunduki mbele ya watu ukanyamaza unategemea mtakapokuwa peke yenu watakuwa na huruma kwako? Kwa marekani kuna kitu kinaitwa miranda rights, ambazo kwa Tanzania usipojibu swali la polisi utapata kipigo kikali sana hasa iwapo utakuwa peke yako pamoja na askari hao. Salama yako mbele ya askari wa Tanzania ni kuhakikisha kuwa una shaidi mwingine independent.

Si tunaambiwa Ulimboka alipigwa ngwara na kubebwa mzega mzega hadi ndani ya gari la watekaji? Je sasa angeuliza maswali saa ngapi?
 
JF ni darasa kubwa sana, miaka minne iliyopita, kuna mwanachama mmoja alitupa somo hapa kama ifuatavyo

(1) Je kuna yeyte kati yetu amewahi kufikiria ku-exercise rights zake mbele ya polisi?

(2) Ilikuwaje Dr. Ulimboka alikubali kukamatwa na polisi bila kuzingatia haki zake hizo? hasa zile tatu za kwanza? Inawezekana hakuwa anazijua; tujitahidi tujifunze mambo mengine yaliyok nje ya taaluma zetu, hasa sheria.

(3) Inawezekana alikuwa anazijua lakini hakuwa na nafasi ya kuzi-exercise kwa vile askari walimfuata wakiwa wamemshikia bunduki, lakini je iwapo askari wakikushikia bunduki mbele ya watu ukanyamaza unategemea mtakapokuwa peke yenu watakuwa na huruma kwako? Kwa marekani kuna kitu kinaitwa miranda rights, ambazo kwa Tanzania usipojibu swali la polisi utapata kipigo kikali sana hasa iwapo utakuwa peke yako pamoja na askari hao. Salama yako mbele ya askari wa Tanzania ni kuhakikisha kuwa una shaidi mwingine independent.

Wanajamvi mwenye "Traffic Act" atuwekee hapa tujijuze tunyooshane kwa haki na hawa matrafik dhaifu.
 
JF ni darasa kubwa sana, miaka minne iliyopita, kuna mwanachama mmoja alitupa somo hapa kama ifuatavyo

(1) Je kuna yeyte kati yetu amewahi kufikiria ku-exercise rights zake mbele ya polisi?

(2) Ilikuwaje Dr. Ulimboka alikubali kukamatwa na polisi bila kuzingatia haki zake hizo? hasa zile tatu za kwanza? Inawezekana hakuwa anazijua; tujitahidi tujifunze mambo mengine yaliyok nje ya taaluma zetu, hasa sheria.

(3) Inawezekana alikuwa anazijua lakini hakuwa na nafasi ya kuzi-exercise kwa vile askari walimfuata wakiwa wamemshikia bunduki, lakini je iwapo askari wakikushikia bunduki mbele ya watu ukanyamaza unategemea mtakapokuwa peke yenu watakuwa na huruma kwako? Kwa marekani kuna kitu kinaitwa miranda rights, ambazo kwa Tanzania usipojibu swali la polisi utapata kipigo kikali sana hasa iwapo utakuwa peke yako pamoja na askari hao. Salama yako mbele ya askari wa Tanzania ni kuhakikisha kuwa una shaidi mwingine independent.

Kama umeangalia zile clip zake za youtube walimvamia na kumbeba kinguvu maana alipigwa mtama na kudondoka alivyoanza kuwahoji tena walikua watu watano waliokua na silaha so its not easy to implement democracy in that situation.Bongo hakuna sheria za raia labda uwe ulaya tu ndo unaweza pata hizo haki
 
Kichuguu,

..Je, raia wana haki ya kukataa[right to remain silent] kutoa maelezo kwa vyombo vya dola??

Sidhani kama Tanzania kuna sheria ya aina hiyo, ila sijui ukweli wenyewe. Hata kama ipo, nadhani inakuwa overridden na nguvu za kipolisi. Kuna sheria inayomtaka raia atoe ushirikiano na polisi wakati wowote anapotakiwa; kukataa kutoa maelezo inaweza kufasiriwa ni kukataa kutoa ushirikiano na polisi.

Again; sina uhakika na uwepo wa sheria hiyo.
 
Kama umeangalia zile clip zake za youtube walimvamia na kumbeba kinguvu maana alipigwa mtama na kudondoka alivyoanza kuwahoji tena walikua watu watano waliokua na silaha so its not easy to implement democracy in that situation.Bongo hakuna sheria za raia labda uwe ulaya tu ndo unaweza pata hizo haki

Taarifa zilizokuwa zimetolewa mwanzoni zilionyesha kuwa walijitambulisha kama polisi, na walikuwa anampeleka kituo cha polisi; ndiyo maana rafiki yake Deo alitangulia Central kuangalia uwezekano wa kumdhamini. Post yangu hiyo ilikuwa based kwenye hizo taarifa za awali.
 
  • Raia ana haki ya kuwaeleza polisi ama Maafisa wa Kuzuia Rushwa kwamba lolote atakalosema linaweza kutumiwa kama ushahidi mahakamani, na asiburuzwe kuandika tu.
Awaambie kwamba "asiburuzwe kuandika tu," kwa hiyo akibembelezwa kuandika akubali?

Wanasheria wetu wanapata tabu sana na Kiswahili chetu kwa kweli... hahahaaa...

Sura ya 20 ya Sheria ya Tanzania
Sheria ya 9 ya mwaka 1985
Kifungu cha 53 (c) (i)
WAJIBU WAKATI WA KUMSAILI MDHANIWA

Wakati mtu yuko chini ya ulinzi, ofisa wa polisi hatamuuliza maswali yeyote, au kumwambia afanye jambo lolote, kuhusiana na uchunguzi wa kosa, isipokuwa kama:

Mtu huyo atakuwa ametahadharishwa na ofisa wa polisi katika namna hii, kwa kumtaarifu au kusababisha apate taarifa, katika lugha anayoifahamu mtu huyo, kwa maandishi yaliyo kwenye fomu maalum na, kama ikiwezekana, kwa matamshi, kwamba hana wajibu wa kujibu swali lolote atakaloulizwa na ofisa wa polisi, zaidi ya maswali kuhusu taarifa za jina lake na anwani.
 
Mimi nafikiri wale aliokuwa nao walikuwa wanaijua issue yenyewe. Hata huyo rafiki yake alihusishwa kwenye dill. Itakuwaje uko na mtu akamatwe halafu usifuatilie anapelekwa wapi wala usihangaike kumwekea dhamana?

Taarifa kamili ya tukio ipo humu JF. Jaribu kujipa nafasi ya kusoma kwanza tukio zima kabla hujaanza kuchangia.

Kwa kifupi huyo mwenzake alifika kituo cha polisi akaambiwa hakuna mtu aliyepelekwa pale na pia lazima utofautishe kutekwa na kukamatwa.

Kutekwa hakuna dhamana.

Kama wewe una mbinu za kuweka dhamana msitu wa pande unaweza kusaidia kuziweka hapa ili siku utekaji mwingine ukitokea ziweze kutumika.

Asante kwa maoni
 
Kichuguu,

..Je, raia wana haki ya kukataa[right to remain silent] kutoa maelezo kwa vyombo vya dola??

Jokakuu inategemea umekamatwa na afande nani...
Afande Msangi au Kibelaaa...kama ni afande Msangi utaongea tu!
 
Hili ni somo zuri sana lakini sidhani kama lina apply kwa Dr ulimboka kwa sababu moja kubwa hakukamatwa bali alitekwa. hakuna sheria inayosimamia utekaji.
 
Hizi ni haki za raia na zinakoswa kufuatwa na raia.

Kunatakiwa somo jipya mashuleni linalohusu haki za raia. Hili litakuwa ni jukumu la waziri mpya wa Elimu mwaka 2015 chini ya serikali itakayoongozwa na CHADEMA.

Waziri mpya wa mambo ya ndani wa serikali itakayoongozwa na CHADEMA mwaka huo wa 2015, ataliangalia hili na vyombo vyote vya kusimamia sheria kuanzia polisi, mahakama na hawa TAKUKURU na zitaundwa upya na kuwa na watu wanaojua majukumu yao.
 
Back
Top Bottom