MAMMAMIA
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 3,811
- 1,603
mammamia nakubaliana na wewe,ni kweli kuna wanaojiuza lakini hawa wanafanya hivi kwa sababu hawana means yoyote ya kupata income,kwa hiyo ili kuepukana na hili solution yake sio kuanza kukimbizana na makahaba mtaani ,solution ni kuwa na mikakati ya kumsomesha mwanamke popote pale alipo nchini Tanzania kwa gharama yoyote ile.
IVUGA, sikukusudia wanaojiuza moja kwa moja, hawa kwa upande mmoja ninawaheshimu kwani angalau wanapambana na maisha; na kwa upande mwengine ninawahurumia kwani wengi wao hawafanyi hivi kwa kupenda, kama wakiwezeshwa kielimu na kimahitaji wanawacha.
Lakini niliowakusudia ni wale ambao ama peke yao au kwa kushirikiana na wanaume wanaendesha biashara ya ukahaba. Hawa wanakuwa "middle woman" au mameneja, wanamiliki maduka ya ngono na "wanasukuma" wasichana wadogo kuingia katika ukahaba. Sijui hili ninalozungumzia hapa litakuwa na ukweli kiasi gani kwa Tanzania, na nitafurahi kusikia kama bado halijafika, pia tujiandae kulizuwia. Huwa ninawaona wasichana wa Kiafrika hasa kutoka Afrika ya Kaskazini na Magharibi, Ulaya ya Mashariki, Asia na Amerika ya Kusini wakiwa wameingizwa bila ya ridhaa yao katika ukahaba. Wanalazimishwa kila siku walipe kiasi gani na wasipolipa wanachezea mkong'oto.