Waridi
JF-Expert Member
- Mar 30, 2008
- 1,025
- 172
Mkuu Kahangwa,Ndugu Waridi,
Ahsante kwa pongezi. Nakubali jukumu ulilonipa la kufafanua zaidi.Ni vizuri basi yangeulizwa maswali hapa ili iwe rahisi kwangu kutambua mahali pa kutolea ufafanuzi.
Kuhusu baraka za wanaJF,naona mpaka sasa michango iliyotolewa hadi huu wa kwako ni positive,basi tusaidiane kuueneza ujumbe wake kwa watu wengi zaidi.
Ujumbe tuliueneza na tunaendelea kuueneza. Wakati huo huo tukikabiliwa na kani kinzani ya watawala, ambao wameamua kuiendea dhuluma, ili wanufaike wao wachache kwa kuliangamiza taifa.
Leo nami nina swali kwako; Je, wewe uko tayari wananchi wakutume uhamishe maneno yako ya haki kuinua taifa katika vitendo, uko tayari kulitumikia taifa kama kiongozi kitaifa, kwa HAKI pasipo chembe ya dhuluma, hila na uongo?