Haki Huinua Taifa

Ndugu Waridi,
Ahsante kwa pongezi. Nakubali jukumu ulilonipa la kufafanua zaidi.Ni vizuri basi yangeulizwa maswali hapa ili iwe rahisi kwangu kutambua mahali pa kutolea ufafanuzi.
Kuhusu baraka za wanaJF,naona mpaka sasa michango iliyotolewa hadi huu wa kwako ni positive,basi tusaidiane kuueneza ujumbe wake kwa watu wengi zaidi.
Mkuu Kahangwa,
Ujumbe tuliueneza na tunaendelea kuueneza. Wakati huo huo tukikabiliwa na kani kinzani ya watawala, ambao wameamua kuiendea dhuluma, ili wanufaike wao wachache kwa kuliangamiza taifa.
Leo nami nina swali kwako; Je, wewe uko tayari wananchi wakutume uhamishe maneno yako ya haki kuinua taifa katika vitendo, uko tayari kulitumikia taifa kama kiongozi kitaifa, kwa HAKI pasipo chembe ya dhuluma, hila na uongo?
 
Kahangwa

Inabidi ufanye juhudi ya kufahamu mfumo wa haki zaidi ya hichi ulichokiweka hapa;

Sura ya nne: umeongelea haki na dini; lakini sijaona references za bible ila watu maarufu wa kanisa katoliki..Pili unatakiwa usome na Quran kujua mfumo wa haki katika dini ya uislamu pia...vinginevyo sura ya nne siyo comprehensive au kisomi tunaita "iko biased" as if wakatoliki maarufu ndio dini wanayoeleza haki kuliko biblia na Quran..(hapo kuna gaps nyingi unahitajika kujaza ninaweza kukusaidia)

1st of all: mfumo wa haki wa kiuchumi, sheria na siasa ni very ambiquous as long as utaruhusu watu fulani wajifungie mahali watunge mifumo (bunge, wataalamu etc) yote hapo huwezi kupata haki ila haki ya waliotunga..huo mfumo

2nd, mfumo wa haki muasisi wake Muumba wa mbigu na Ardhi, mfumo ambao muasisi wake ni binadamu hauwezi kuwa wa haki hata siku moja

Unataka mfumo wa haki kusanya vitabu vya Muumba: Tourati, Injili na Quran; tafuta sheria za biashara, uchumi, mfumo wa kikatiba na sheria za kutawala watu..kama hizo zitakuwa source of legislation hapo ndio haki itasimama duniani na taifa litainuka..

Kwasababu mfumo ambao source of legislation ni Muumba hakutakuwa na clause inayosema Rais hashatakiwi akiwa madarakani huo ni mfumo usiokubali haki bali rais anakuwa juu ya sheria; kwakuwa walioshiriki kutunga ni wenzake..

Haki huanza ni source of our legislationss..
 
Ndugu Tropical,
Nakushukuru sana kwa ushauri na mchango wako mzuri sana. Nikiri kuwa sijawahi kupata fursa nzuri ya kusoma maandiko matakatifu yaliyomo katika Quran. Muda mrefu nimetamani sana kuelimishwa katika maandiko hayo. Nakusihi usisite kunielimisha, na panapo uwezekano naomba aya za Quran, zinazozungumzia haki.
Mada hii ya haki, niliiandika nikiitazama Tanzania na nini unapaswa kuwa mwelekeo wa taifa letu. Kwa kuwa yaweza kuwa kwa manufaa hayo, wewe, mimi na wasomaji wote, tukishirikiana katika kuboresha nilichokiandika litakuwa jambo jema sana.
 
Mkuu Kahangwa,
Ujumbe tuliueneza na tunaendelea kuueneza. Wakati huo huo tukikabiliwa na kani kinzani ya watawala, ambao wameamua kuiendea dhuluma, ili wanufaike wao wachache kwa kuliangamiza taifa.
Leo nami nina swali kwako; Je, wewe uko tayari wananchi wakutume uhamishe maneno yako ya haki kuinua taifa katika vitendo, uko tayari kulitumikia taifa kama kiongozi kitaifa, kwa HAKI pasipo chembe ya dhuluma, hila na uongo?

Ndugu Waridi,
Ahsante kwa maswali, mimi ni Mwalimu na Mwanafunzi vilevile. Naamini katika nafasi hizo nalitumikia taifa pasipo ukengeufu katika kutenda haki.
 
asante kwa mada nzuri. na refreshing.
ulitaka maswali naomba niulize wakati tunaendelea.
- unadhani ni kwa kiwango gani haki kama unavyoielezea inapatikana Tanganyika kwa miaka hii ya karibuni?
- katika quotations zako ipi ni ya karibuni zaidi? je kuna ya muafrika? na kuna mwandishi mwanafilosofia aliaendiika kuhusu haki miaka ya karibuni?- 1-10 iliopita
- je katika hili wajibu unaendana vipi na hii haki?
otherwise asante sana
 
Ndugu Haika,
'Haika' sana kwa maswali yako. Naomba nikujibu japo kwa kifupi kama ifuatavyo;

Qn.I; Kwa sasa hatuna Tanganyika. Kama unaizungumzia Tanzania, kiujumla matendo ya haki katika nchi hii yamefunikwa na wingi wa matendo ya dhuluma na maasi. Kiwango cha ufisadi katika siasa biashara na uchumi ni kikubwa sana. Wanasiasa na maswaiba wao wenye fedha wanawanyonya wanyonge, jamii imegubikwa na vitendo vya ukatili dhidi ya akina mama na watoto, rushwa inatamalaki katika kila sekta, vyombo ambavyo vinapaswa kuongoza katika utoaji haki (mahakama na polisi) ndivyo kitakwimu vinaongoza kwa rushwa.
Aidha, hapana shaka umepata kusikia juu ya sheria 40 zinazotumika Tanzania ambazo ni mbaya (kwa maneno mengine hazitendi haki)

Qn. 2 Utaona kwamba niliandika mada hii mwaka 2008, katika rejea nilizozitumia, zilizokuwa za hivi karibuni zaidi ni

  • Deus Caritas Est (2006), na
  • Compendium of the Social Doctrine of the Church (edition ya 2006)
Kwa pamoja tunaweza kutafuta maandiko ya kiafrika kuhusu haki. Nilichokiandika mimi, inshallah, siku moja naweza kukiboresha hadi ngazi ya kuchapishwa katika kitabu.

Qn. 3 Zipo haki ambazo huendana na wajibu, yaani ni kama vile pande mbili za sarafu moja, Mfano mfanyakazi anayo haki ya kulipwa ujira, lakini sharti atimize wajibu wake wa kufanya kazi. Hata hivyo zipo haki ambazo ni stahiki kwa mtu kupewa bila hata kumwuliza kwanza maswali juu ya wajibu wake, matharani haki ya kuishi.
 
Back
Top Bottom