Ninadhani suluhu itakayokata mzizi wa fitina ni kuwa na serikali ya majimbo ambayo Zanzibar itakuwa jimbo lenye Gavana wake kama majimbo mengine. Hii itawapa Wazanzibari wasaa mzuri wa kuamua mambo yao wenyewe katika ngazi ya jimbo na vile vile itatoa haki sawa kwa majimbo mengine.