Hadithi ya mjukuu kifuani mwa babu na Lissu anayecheza na akili za watu majukwaani

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
2,948
1,988
Hakuna mahali salama kwa mjukuu wa chini ya miaka miwili kulinganisha na kifuani kwa babu yake anapolala baada ya kuzidiwa na usingizi unaotokana na utamu wa hadithi ndefu. Huwa wajukuu wanasinzia upesi mno na mara nyingi hadithi haifiki hata nusu ya urefu wake, wao wakiwa wameshasinzia.

Mtoto mtu anayetazama hiyo taswira machoni mwake huwa anajichekea tu akikumbuka namna Babu yule yule aliyembeba mjukuu wake namna alivyokuwa akiwacharaza wakati wa utoto. Haamini kwamba ni mzee yule yule aliyemkumbatia mjukuu muda huo ndio aliyewatandika bila huruma wao watoto, baada ya kutotii amri za wazazi.

Kila kitu huwa na awamu yake. Hata uongozi wa nchi huheshimiwa wakati ukiwa umeshaondoka. Hakuna awamu kati ya tano zilizotangulia iliyosifiwa na kupigiwa makofi wakati Rais akiwa bado yupo ikulu, haipo!.

Julius Nyerere tulimlaani sana wakati tukila ugali wenye rangi ya njano na kuvaa mashati ya kupika na vidabwada. Mzee Mwinyi licha ya kupunguza makali ya maisha kulinganisha na miaka ile ya themanini mwanzoni nae tulimlaani kwa kuuza Loliondo na masuala ya udini kushamiri serikalini na kwenye taasisi mbalimbali.

Mkapa aliyeanzisha TRA na mifuko kadhaa inayofanya kazi nzuri hadi leo hii na yeye tulimlaumu kwa yaliyotokea kule Zanzibar mwaka 2001 mwanzoni. Kikwete licha ya kujenga barabara nchi nzima tunalikumbuka kosa lake la kuanzisha mitandao na namna wizi ulivyoshamiri wa ESCROW.

Kwa ufupi rais mzuri ni yule aliyekwisha kustaafu, akiwa pale ikulu ni sawa na ndoo ya kuwekea takataka, kila mwenye mdomo hamuachi salama, ni lazima amtukane, amkosoe na wengine huenda mbali zaidi kwa kuamua kumtukana matusi ya nguoni.

Tundu Lissu huyu huyu aliyeondoka pale uwanja wa ndege kwenda Ulaya akiwa anatembea ubavuni mwa mabalozi ili asikamatwe ndiye huyu huyu anayesema hayati JPM alikuwa ni kiongozi mzuri kumlinganisha na Samia!.

Lissu huyu huyu aliyelala hospitalini akiondolewa risasi mmoja baada ya nyingine na kwenda kujuliwa hali na Rais Samia leo hii anasema afadhali ya yule aliyekwisha kutangulia mbele ya haki!, kuwa uyaone ni msemo wa marehemu Mama yangu miaka ile nikiwa nakula ugali wa bure pembeni yake.

Lissu huyu huyu aliyehangaikiwa mpaka akalipwa mafao yake halali ya ubunge leo hana hata haya anasema Rais SSH hana afadhali kwa kumlinganisha na hayati JPM aliyepambana mpaka akahakikisha bunge la kuanzia 2021 lina mbunge mmoja tu wa CHADEMA!.

Ni kweli tupo kwenye ulimwengu wa uwazi, wa vyama vingi. Lakini tukumbuke kusutwa na nafsi zetu kabla hatujapanda majukwaani na kuanza kuongea.

Urais wa nchi unafanana na mapenzi ya Baba kwa watoto wake. Wanapotandikwa bakora za nguvu utotoni wanamchukia sana mzazi wao lakini wanaitunza ile picha au video fupi ndani ya simu zao ambayo inamuonyesha Babu [Baba yao] akimbembeleza mjukuu wake [mtoto wao] mpaka anasinzia kifuani mwake.

Ubaya na uzuri wa Baba mzazi ni tafsiri binafsi ya mtoto kadri anavyozidi kukua na kuifahamu dunia vizuri zaidi.
 
Sijui wenzangu humu muna miaka mingapi au mumeanza lini kufuatilia harakati/Siasa za Lissu, ukweli ni kwamba Lissu hajawahi kuwa na upande hasa linapokuja suala la maslahi ya Taifa, hembu chimbueni history kidogo tangu enzi ya Mkapa na uwekezaji wake kwenye Migodi, njooni kwa Kikwete mpaka Magufuli na sasa Mama Samia, hakuna mtawala wa Nchi hii hajapelekewa vumbi na Lissu, na kote huko alipokuwa anapiga kelele niambieni ni wapi tuliwahi pata faida kama sio kuibiwa na sisi kuendelea kuwa ombaomba.

Tuwekeni ushabiki pembeni, hata kwa dakika moja tufikirie mali zetu zinamnufaisha nani hasa, watoto wetu watapata nini sisi tukiwa tumelala mazima, au havituhusu kwa vile tutakuwa hatupo?

Tuje kwenye ukweli, kama kweli Lissu angekuwa anahongeka, ni nani anafaa kuhongeka kwa ushawishi kati ya hawa chawa na Lissu, nani anaweza kutetea hoja zaidi kati ya waandishi uchwara na Lissu? bila shaka wahusika wakuu wa hili sakata wangetamani kumhonga Lissu awatetee zaidi ya hawa wanaohangaika huku mitandaoni.

Tulipigwa ESCROW, EPA, RADA, BUZWAGI, Mruma kaaibika na kuaibisha Taifa juzi na kamati yake, sasa tunajiandaa kupigwa DP World, bila shaka kwa aibu kubwa mbele ya safari.

Time will tell, wasi wasi wangu ni kwamba mpaka huo muda unafika hali itakuwaje.
 
Back
Top Bottom